esther mashiker
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 616
- 552
JENGO la tatu la abiria (Terminal III) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam linatarajiwa kutengeneza ajira lukuki, zikiwamo 245 za moja kwa moja litakapoanza kutumika Mei mwaka huu.
Aidha, maandalizi yanaendelea kufanyika kwa ajili ya matumizi ya jengo hilo la tatu ambalo litakuwa maalumu kwa abiria wa kimataifa huku jengo la pili likiwa la abiria wa ndani ya nchi. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Julius Ndyamukama aliliambia gazeti hili jana kwamba maombi ya kibali cha kuajiri wafanyakazi yameshapelekwa kwenye mamlaka zinazohusika.
“Hizo ni ajira za moja kwa moja, achilia zile za maduka, hoteli na kadhalika,” alisema Ndyamukama na kufafanua kuwa wameomba kuajiri wafanyakazi watakaohudumu katika maeneo mbali mbali. Ndyamukama alisema kibali kilichotoka ni cha ajira 135.
Taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo la tatu iliyotolewa kwa Bodi ya Wakala wa Barabara (Tanroads) iliyofanya ziara JNIA hivi karibuni ilisema TAA inakamilisha mchakato wa kupata watoaji wa huduma mbalimbali katika jengo na mhandisi mshauri wa uendeshaji na uhamisho wa uwanja wa ndege (ORAT).
Vile vile taarifa ilisema TAA wameanza kujifunza kutoka kwa mkandarasi juu ya matumizi na jinsi ya kufanyia matengenezo vifaa na mifumo mbalimbali ya jengo hilo jipya. Ndyamukama alithibitishia gazeti hili kwamba mkandarasi wa mradi, BAM International anaendelea na kazi hiyo ya kutoa mafunzo. “Kila mfumo ukifungwa wafanyakazi wanapewa mafunzo juu ya matumizi,” alisema Ndyamukama aliyekuwa Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam kabla ya uteuzi wa hivi karibuni kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAA.