Jengo la Simba larudishiwa Umeme baada ya zaidi ya Miaka 10

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,302
4,681
Hatimae lile jengo lililokuwa linatia aibu katikati ya mji yaani jengo la KILABU cha simba limerudishiwa umeme baada ya kusota gizani zaidi ya miaka 15.

Jengo hilo linalosifika kwa uchafu hapa Dar limerudishiwa umeme mapema leo na kumeonekana na shamrashamra za watu wa eneo hilo.

kurudishwa umeme kwa jengo hilo kunatokana na kelele zilizopigwa na wanachama wanaopenda maendeleo wa CLUB ya Yanga waliokuwa wanawashinikiza kila kukicha viongozi na wapenzi wa KILABU cha Simba.

Zoezi linalofuata sasa ni kushinikiza uongozi na washabiki wa Simba waweze kupaka rangi jengo lao, kuzibua vyoo, kurudisha maji na marekebisho mengine.
 
amka2.gif
MWENYEKITI mpya wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amesikitishwa na uduni wa jengo la klabu hiyo kukosa umeme kwa muda mrefu baada ya kukatwa kwa deni la sh mil. 3.7, licha ya klabu hiyo kuingiza zaidi ya sh bil. 5 ndani ya miaka 15! Rage aliyechaguliwa juzi usiku kwa kura 785 akimbwaga Othman Hassan Hassanoo, aliyasema hayo jana katika ofisi za makao makuu ya klabu hiyo baada ya kiongozi huyo kufanya ziara na kuahidi kuweka mambo sawa mara moja kuanzia jana.
Rage aliyewahi kuwa mchezaji wa Simba kabla ya kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF wakati huo FAT), alisema dosari hizo zitashughulikiwa ili majengo hayo yafanane na hadhi ya klabu hiyo.
Mbali ya kuboresha makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Mtaa wa Msimbazi, Rage alisema uongozi wake utatafuta eneo jingine kwa ajili ya kujenga ofisi za muda ili majengo ya makao makuu yatumike kibiashara zaidi.
Kwa lengo la kudumisha umoja na mshikamano ambao ni moja ya nyenzo ya mafanikio, jana mchana Rage alipanga kukutana na kundi la ‘Friends of Simba' katika chakula cha mchana huku akimwalika mwenyekiti aliyemaliza muda wake juzi, Hassan Dalali na Mwina Kaduguda.
Baada ya kikao hicho na Friends of Simba, baadaye jioni Rage alipanga kukutana na viongozi wenzake wa kamati ya utendaji na viongozi wa matawi yote ya klabu hiyo, yote hiyo ni kujitambulisha na kuanza kuweka mambo sawa.
Aidha, kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano, Rage alisema watafikiria uwezekano wa kumrejeshea haki ya uanachama, Michael Wambura aliyesimamishwa kutokana na kufungua kesi mahakamani kupinga uchaguzi mkuu baada ya kuenguliwa kwa madai ya kukosa uadilifu.
Kauli ya Rage imetokana na hatua ya Wambura kumpongeza Rage kwa ushindi na kuahidi kushirikiana na uongozi mpya na kwamba atafuta kesi zote zilizofunguliwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mahakama Kuu
 
Hatimae lile jengo lililokuwa linatia aibu katikati ya mji yaani jengo la KILABU cha simba limerudishiwa umeme baada ya kusota gizani zaidi ya miaka 15.

Jengo hilo linalosifika kwa uchafu hapa Dar limerudishiwa umeme mapema leo na kumeonekana na shamrashamra za watu wa eneo hilo.

kurudishwa umeme kwa jengo hilo kunatokana na kelele zilizopigwa na wanachama wanaopenda maendeleo wa CLUB ya Yanga waliokuwa wanawashinikiza kila kukicha viongozi na wapenzi wa KILABU cha Simba.

Zoezi linalofuata sasa ni kushinikiza uongozi na washabiki wa Simba waweze kupaka rangi jengo lao, kuzibua vyoo, kurudisha maji na marekebisho mengine.

Tehe teh...........haya ni mambo ya 'samjo' Rage ama????
 
Mambo mengine ni aibu tupu
 
I hope si nguvu ya soda hii Rage. Kinachonisikitisha hautapita muda utasikia tayari migogoro sijui nani kafanya hivi mara huyu kafanya vile uswahili mtupu..Simba haikutakiwa kuwa choka mbaya kiasi kile ila hao aina ya viongozi wanaotafuta maisha klabuni ndio tatizo...
 
Hilo ni funzo kwamba timu zinatakiwa kuwa makini katika kuchagua viongozi makini na kuacha ushabiki na kufahamiana
 
Siasa tu hizo baada ,ndio mbinu zinazotumiwa na viongozi wa bongo
 
Hii ni aibu kuba sana kwa viongozi wote wa Simba walioongoza miaka hiyo ni wezi watupu. hata wanachama wa Simba walioko Dar nao wana walakini. Inawezekanaje Klabu kubwa kama ya Simba kuwa duni zaidi ya Kilabu cha Kangara. Shame!
 
big up lage! but why wambura was objected on ground of credibility.Hivi kati ya rege na wambura kwa wazi tu nani mwenye rekodi ya usafii!tanzama historia kiduchu tu!
 
Shukrani si za Rage.
Shukrani ni za washabiki wa Yanga waliokuwa wakiweka wazi uozo wa KILABU cha Simba.

Na huyo Maharage anajishaua tu.
Kwani yeye hilo tatizo la umeme hakuliona hapo awali??
Msidanganyike kitoto
 
Teh teh vizee vya simba vinapishana koridoni huku kila mmoja akiwa kashika chaja yake ati anakwenda kuchaji simu...teh teh teh kweli we ukisema cha nini mwenzako asema ntakipata lini?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom