Jengo la Makao Makuu ya TANESCO Ubungo kubomolewa wakati wowote kupisha ujenzi wa 'Interchange'

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli amesema kuwa Jengo la Makao Makuu ya TANESCO lililopo Ubungo litabomolewa wakati wowote kuanzia sasa ili kupisha ujenzi wa Ubungo Interchange yenye ghorofa 2 mpaka 3 hali itakayopunguza msongamano wa magari kwenye eneo hilo.

Rais Magufuli amesema kuwa Serikali imepata shilingi Bilioni 67 kwa ajili ya ujenzi huo hivyo wakati wowote jengo hilo litabomolewa kwa vile lipo kwenye hifadhi ya barabara.

Hongera sana Rais Magufuli kwa kukumbusha tena suala hilo ambalo uliahidi miaka kadhaa iliyopita japo liliwekewa kizuizi na Rais Kikwete. Kwa sasa wewe ndiwe mwenye Rungu hivyo naamini kuwa hilo litatekelezwa ili kuondoa Double Standard.
 
Time will tell
 
Isije tukafika sehemu wakasema milima ya Uluguru nayo isawazishwe ili yawe mashamba na kifusi kiletwe Jangwani ili pageuzwe makazi maana viwanja ni haba!
Hivi ukiangalia majengo yaliyo mkabala na jengo la Tanesco (nadhani paitwa maji) ni wapi ambapo ukivunja hasara inakuwa kidogo!? Inabidi tukubaliane kwamba serikali zilizotangulia hasa awamu ya pili, tatu na nne ambazo zote zilikuwa chini ya chama kile zimevurunda. Sio katika viwanja tu bali karibia kila kitu, na cha kuchekesha zote huwa zinaanza na mkwala mzito kama 'fagio la chuma', 'cleanliness', 'mwendo-kasi mpya' na sasa 'hapakazitu'.
Kwa hiyo suluhisho ni hawa waliofanya makosa haya (kama bado wako hai) waje hadharani na kutueleza ni kwa nini walifanya hivyo na waombe msamaha, watakaoeleweka wasamehewe na 'wasioeleweka' tuwapeleke mahakamani! Hapo ndpo tunaweza kwenda mbele badala ya bla bla za kila uchao!
 
Naona alishindwa kulibomoa chini ya Kikwete sasa kafanikiwa ......

Lakini ni sawa kama faid ni kubwa kuliko hasara hakuna tatizo........
Ni kweli Mkuu. Faida itakayopatikana kutokana na kubomoa jengo hilo ni kubwa sana kuliko likiendelea kubaki
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli amesema kuwa Jengo la Makao Makuu ya TANESCO lililopo Ubungo litabomolewa wakati wowote kuanzia sasa ili kupisha ujenzi wa Ubungo Interchange yenye ghorofa 2 mpaka 3 hali itakayopunguza msongamano wa magari kwenye eneo hilo.

Rais Magufuli amesema kuwa Serikali imepata shilingi Bilioni 67 kwa ajili ya ujenzi huo hivyo wakati wowote jengo hilo litabomolewa kwa vile lipo kwenye hifadhi ya barabara.

Hongera sana Rais Magufuli kwa kukumbusha tena suala hilo ambalo uliahidi miaka kadhaa iliyopita japo liliwekewa kizuizi na Rais Kikwete. Kwa sasa wewe ndiwe mwenye Rungu hivyo naamini kuwa hilo litatekelezwa ili kuondoa Double Standard.
Haituhusu,kawaambie makada wenzio
 
Kuna ile sheli nayo iko ndani ya hifadhi ya barabara, walimbembeleza aiache nadhani aipitie na yenyewe. Ila hapo Tanesco Mramba awe makini zaidi atakwenda na jengo
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli amesema kuwa Jengo la Makao Makuu ya TANESCO lililopo Ubungo litabomolewa wakati wowote kuanzia sasa ili kupisha ujenzi wa Ubungo Interchange yenye ghorofa 2 mpaka 3 hali itakayopunguza msongamano wa magari kwenye eneo hilo.

Rais Magufuli amesema kuwa Serikali imepata shilingi Bilioni 67 kwa ajili ya ujenzi huo hivyo wakati wowote jengo hilo litabomolewa kwa vile lipo kwenye hifadhi ya barabara.

Hongera sana Rais Magufuli kwa kukumbusha tena suala hilo ambalo uliahidi miaka kadhaa iliyopita japo liliwekewa kizuizi na Rais Kikwete. Kwa sasa wewe ndiwe mwenye Rungu hivyo naamini kuwa hilo litatekelezwa ili kuondoa Double Standard.
Umeongeo uongo sana, na inaonekana uwezo wa kuelewa mambo ni mdogo sana. Mh Rais jana alikuwa anazungumzia sheria ya na mabadiliko yake mpaka 2007. Na akasema sheria ilishapitishwa na bunge upana wa barabara, kwahiyo hao wanaolalamika wakati wako ndani ya hifadhi ya barabara hakuna jinsi. Ndio akatolea mfano kwamba kuna inter change itakayojengwa ubungo, huenda ikawa na gholofa mbii au tatu. Ujenzi utakapo anza ndio wataona kama kuna haja ya kulibomoa jengo la Tanesco, akimaanisha ubomoaji hauwahusu wananchi tu, hata majengo ya serikali. Sasa uelewa wako mdogo umekuja na hiyo thread ya udogo wa ufahamu wako wa akili. Pole sana, ndugu yetu Lisbon.
 
Ni kweli Mkuu. Faida itakayopatikana kutokana na kubomoa jengo hilo ni kubwa sana kuliko likiendelea kubaki
Serikali ya Ccm wakati inatoa kibali cha kujenga jengo hilo haikufahamu kuwa hiyo ni hifadhi ya barabara? Hapa sio suala la JK au Magu ni uzembe wa serikali hiihii ya Ccm isiyojua kutumia rasilimali zake vizuri na kusababisha hasara zisizo na msingi.
Ni kama vile enzi zile za waziri wa ujenzi kuamuru kituo cha mafuta Kule Mwanza kubomolewa na kulipa fidia bilioni kadhaa ya hela zetu kisha hakuna la maana lililo endelea. Au issue ya samaki
 
Naona alishindwa kulibomoa chini ya Kikwete sasa kafanikiwa ......

Lakini ni sawa kama faid ni kubwa kuliko hasara hakuna tatizo........
ili kujenga njia sita na 'change over' ni lazima ubomoe...hili lipo kwenye ramani na vipimo si swala unalosema...lilisubiri pesa tu za ujenzi wa barabara zipatikane.
 
Back
Top Bottom