Jengo la Mahakama ya Rufaa Kubomolewa kupisha Upanuzi wa Hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro

hizo presidential suites zinazoongezwa nadhani zimetarget wageni mashuhuri hasa wanadiplomasia na wawekezaji (wanunuzi wa nchi yetu) wanaotembelea TZ mara kwa mara na amabao huongezeka mwaka hadi mwaka. najisikia dalili za kusahau kabisa mpango wa serikali kuhamia dodoma!

OMG!
 
dah kwa kweli hii nchi haina uongozi ni uozo mtupu. wageni wanafanya wanachotaka! maskini nchi hii tunanyanyaswa tukiona, jengo la kihistoria linabomolewa!! kupisha ujenzi wa hoteli, Rais legelege na serikali legelege. tukiamka kesho utasikia pale posta ya zamani pameuzwa kwa mwekezaji!! anataka kujenga tena hotel. kweli tunachokozwa hivihivi tunaona. tukidai mali yetu tutitwa wachokozi.
 
haya ni majengo ya kwanza kabisa ya kihistoria kujengwa jijini na wakoloni

Kama wamejenga wakoloni sioni sababu yeyote ya kutunza historia hii, hata wao wakoloni waliondoa historia yetu. Vunja kila kitu cha mkoloni.
 
Chama legelege huzaa serikali legelege; serikali legelege huleta anarchy! Nyie subirini tu mtaona.
 
Jengo la kihistoria la Mahakama ya Rufaa litabomolewa kupisha upanuzi wa hoteli ya zamani ya Kilimanjaro Kempinski ambayo imebadilishwa jina hivi karibuni na kuitwa Hyatt Regency – Kilimanjaro. Jengo hilo lilikuwa linatambulika kama jengo la kihitoria kupitia Gazeti la Serikali Namba 498 la mwaka 1995. Hata hivyo serikali imeamua kutolitambua jengo hilo tena kama la kihistoria

Hata hivyo, baadhi ya watu wanalalamika kuwa kuvunjwa kwa jengo hilo la kihistoria kutaadhiri mwonekano ya Kivukoni Front ambapo pia kuna majengo mengine ya kihistoria yakiwemo yale ya Mahakama Kuu, Tanzania Bureau of Statistics na Mahakama Kuu ya Biashara. Msemaji kutoka Wizara Utalii na Maliasili ambaye hakutaka jina lake litajwe ameliambia gazeti la Daily News kuwa serikali imekubali mmiliki wa eneo la hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro kubomoa jengo hilo la kihistoria na kujenga jengo jipya ili kupanua hoteli hiyo. Jengo jipya litakuwa na presidential suites nyingi.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Bw. Rutabanzibwa, amesema amesikia mpango wa kuboa hilo jengo hilo lakini bado hajataarifiwa kiofisi. Hata hivyo, amesema ingekuwa vizuri kama jengo hilo lingebakia kama lilivyo ili kuendana na plan ya jiji la Dar Es Salaam. Msemaji mwigine ndani ya wizara hiyo amesema kama jengo hilo la kihistoria litabomolewa, basi itabidi majengo mengine ya kihistoria nayo yabomolewe.

Alipoulizwa Waziri wa Wizara ya Utalii na Maliasili, Mh. Ezekiel Maige, alisema taarifa zote zinapatikana kwa katibu wake, Bi. Maimuna Tarishi. Alipofuatwa Bi. Tarishi alisema atatoa habari kimaandishi. Afisa Mawasiliano wa hoteli ya Hyatt Regency anayejulikana kwa jina moja Nasra alipoulizwa alisema hana mamlaka ya kuongelea hili suala.

a SI JUZI JUZI TU HILI JENGO LIMEFANYIWA UKARABATI WA MAMILIONI YA SHILINGI ILI LIWE NA HADHI YA COURT OF APPEAL? LEO LABOMOLEWA KABISA. OOOH, TANZANIA. HISTORIA YAKO YAZIDI KUPOTEA. BAADA YA HAPO JENGO JEUPE LA MAGOGONI NALO PIA MAANA LILIJENGWA ZAMANI SANA NA WADOGO ZAKE KARL PETERS.
 
nchi hii kwisha kabisa, tunaambiwa huko mwanza mti wa kihistoria ambao ulitumika kunyongea makamanda wetu wameukata, hawajali kabisa.
 
Sioni tatizo lolote na huo mpango... kumbe historia yenyewe ya mkoloni, mi nilidhani yana preserve historia ya watawala wa kale kabla ya mkoloni... wangevunja na kujenga upya hata IKULU ikiwezekana,... Wafute kabisa alama za mkoloni, no problem with me. Tuache utumwa wa fikra.
 
Tanzania kila kitu kinawezekana, hivi watoto wetu watajivunia nini? watajifunza nini kutokana na vizazi vilivyopita??
 
Wanabomoa hili
View attachment 35035

Wanajenga hili

View attachment 35036

Hii itasikitisha kama mpango huu utakamilika, haya ni majengo ya kwanza kabisa ya kihistoria kujengwa jijini na wakoloni

Hili kama litakuwa na ghorofa si chini ya 16 vile. Hivi hili eneo halipo ndani ya Dar es Salaam Master Plan ya mwaka 1979, ambayo ina set six storeys as the maximum height for private buildings around State House? Kiusalama hii ikoje? I am sure ukikaa kama ghorofa ya 6 utaona magogoni. Then, upande wa pili lipo lile jengo lingine la ghorofa 19. Ikulu inazungukwa na majengo ya serikali kwa sababu za kiusalama.

Lakini some real estate and property management experts dismiss the security threat aspect in barring the undertaking of such projects near State House as unfounded. They say advances in security technology means that high-rise buildings should not be such a thorny issue.

state house.jpg
 
Halafu wakishabomoa hiyo mahakama ya rufaa wanawahamishia wapi? Au ndo kuanza tena biashara ya kupangisha jengo kwa bei ya ghali wakati walikuwa na jengo lao?na hao mahakama ya rufaa kwa nini wamekubali kuamishwa/kubomolewa? Na kwa nini hao Hyatt Kilimanjaro Hotel wasipatiwe nje ya mji wakajenga kwa nafasi wakatoa kitu cha ukweli?kwa nini kubanana kati ya mji? Wangepewa kama kule kigamboni au mbagala kwani wanasikia wateja wasingefika? Maswali mengi lakini majibu ndo hatutajakaa tuyapate....hmmmm
 
Rais Mwenyewe hakai nchini kwanini kujenga Presidential Suites? hana wageni wanaokuja kutembelea TZ labda marais wa East Africa
 
Ningependa kwenda juu kabisa kwenye hotel hiyo...nipate view nzuri ya magogoni nione wapi naweza tumia kama target point ya huyu jamaa pale...naona sasa hana sababu za kuwepo.
 
Rais Mwenyewe hakai nchini kwanini kujenga Presidential Suites? hana wageni wanaokuja kutembelea TZ labda marais wa East Africa

Nyingine watakaa wale viongozi ambao bado hawajapata nyumba.
 
Kama wamejenga wakoloni sioni sababu yeyote ya kutunza historia hii, hata wao wakoloni waliondoa historia yetu. Vunja kila kitu cha mkoloni.

Kama akili yako ndiyo hiyo basi utavunja ikulu, reli ya kati, city council, stesheni, bandari, barabara zote kubwa za mjini mfano sokoine, independency n.k kwa taarifa yako hivi vyote vilijengwa na mjerumani kati ya 1890 na 1914. Tutake tusitake historia ya Dar es salaam haiwezi kuongelewa bila kuwajumuisha wajerumani na majengo yao ni sehemu ya historia yetu.
 
Bado ikulu tu sasa mtambiwa iko kwenye busy area kwa hiyo ni vema ikahamishwa!!!!!!! hahah ahahah ahahah!
 
Kama akili yako ndiyo hiyo basi utavunja ikulu, reli ya kati, city council, stesheni, bandari, barabara zote kubwa za mjini mfano sokoine, independency n.k kwa taarifa yako hivi vyote vilijengwa na mjerumani kati ya 1890 na 1914. Tutake tusitake historia ya Dar es salaam haiwezi kuongelewa bila kuwajumuisha wajerumani na majengo yao ni sehemu ya historia yetu.

Reli na Barabara unaweza kuziacha ukilinganisha faida na hasara zake, lakini hilo li ikulu kama linahifadhi historia ya waafrika kudhalilishwa na wajerumani vunja tena haraka, jengo la city council nalo livunjwe tu. Kama kuna sababu nyingine ielezwe lakini sababu hii ya kutunza historia ya wakoloni ni ya kijinga kabisa. Natamani kumuonesha mtoto wangu historia iliyo tukuka ya waafrika sio mabaki ya nyenzo za unyanyasaji sitaki mtoto wangu arithi historia hiyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom