Jengo la Mahakama ya Rufaa Kubomolewa kupisha Upanuzi wa Hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jengo la Mahakama ya Rufaa Kubomolewa kupisha Upanuzi wa Hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rare, Feb 22, 2011.

 1. R

  Rare JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimedokezwa kuwa eti jengo la forodhani ambalo ni Jengo la Kihistoria liko hatarini kubomolewa na Mmiliki wa Kilimanjaro apewe eneo hilo apanue hoteli yake na kisha Kempiski wawajengee mahakama ya rufaa.
  Kinachonisikitisha ni kuwa kama alivyosema magufuli kuwa ameapa ili kulinda katiba na sheria. Jengo hilo liko katika orodha ya Majengo ya Kihistoria yaani national heritage ambayo yanafaa sana kwa kuwakumbusha watu matukio mbalimbali yaliyoambatana na nchi hii.
  Lakini cha ajabu ni kuwa huyo tajiri anaruhusiwa kuvunja sheria na walinda sheria? Na watajengewa jengo jipya lilotokana na kuvunja sheria?
   
 2. G

  Gathii Senior Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Habari ndo hiyo,
  wala siyo tetesi hilo liko njiani,na mkulu analifahamu hilo..ajabu na kweli sijui wapi tunakwenda.Inauma halafu inauzi.

   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mahakama ya Rufaa tujengewe na Mwekezaji....ama kweli wanasema kuishi kwingi kuona mengi. Ila kwangu mimi kuna mengine nadhani hakuna haja ya kuyaona.
   
 4. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mmiliki wa Kempiski ni nani hasa?
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  na hiyo symbol ya national antiques wataipata wapi .... huu ni uhujumu wa uchumi
   
 6. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 4,018
  Trophy Points: 280
  makeke na matunda ya Mohamed Chande Othman yanaanza kuonekana nathani wale wanaolilia fursa sawa kwa Waislam wangelilia pia na jengo hilo lisivunjwe maana hata miezi sita hajafikisha na sidhani kama ana uwezo wa kupinga kinachotaka kufanyika
   
 7. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sio mchezo owner wa Kilimanjaro lazima atake expansion, "he makes money in that hotel" ....nilipita hapo siku moja nikakuta baadhi ya wageni niliokwenda kuwaona imebidi walale nje kwenye hotel nyingine (Southern Sun) kwa sababu Kilimanjaro ilikuwa FULL.....Nashangaa kwa nini wasimpe Embassy hotel au/na Motel Agip zinazokaa zinaoza tu badala ya kubomoa historic building.
   
 8. R

  Rare JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unajua baada ya kupata tetesi hiyo ilibidi nitafute wadau wa sekta hiyo. Mungu wangu kumbe kinachofanyika ni kufuru kwa watz. Ikabidi niende kwenye katiba 27(1) inasema " Kila Mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, kulinda Mali ya mamlaka ya nchi, mali inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, pia kuheshimu mali ya mtu mwingine. Tena inabainisha 27(2) Watu wote wanatakiwa na sheria kutunza vivuri mali ya mamlaka nchi na ya pamoja, kupinga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye"
  Maneno muhimu i) Kila mtu ii) kulinda ii) mali ya umma iii) watu wote iv) sheria v) mali ya mamlaka ya nchi vi) Uharibifu na ubadhilifu vii kuendesha uchumi kwa makini viii) waamuzi wa baadaye. Nitafafanua wakati mwingine madhara ya kuvunja majengo ya kihistoria kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  TETESI ZA KWELI

  PLANS are underway to demolish the historical building now housing the Court of Appeal in Dar es Salaam, to pave way for the expansion of former Kilimanjaro Kempinski Hotel, which was recently renamed Hyatt Regency, sources say.

  Sources told the 'Daily News' that the government has de-gazetted the building which first appeared in the Government Notice (GN) 498 of 1995 as an historical building.

  The revelation comes few days after the weeklong celebrations of the 50 years of the Ministry of Natural Resources and Tourism which, among others things, unveiled the Dar es Salaam City Tourism Exploration Trail that include the ancient building.

  The building protected under the Antiquities Act No. 10 0f 1964 and its amendments No. 22 of 1979 is among landmark features along the trail.

  Conservationists have expressed concerns over the move, saying it will ruin the Kivukoni Front view where several historical buildings including the High Court, Tanzania Bureau of Statistics and the High Court Commercial Division are located.

  "The government has exchanged the building with the Kempinski Hotel's (Hyatt Regency) owner who will have it demolished and erect a new structure as part of the hotel expansion," said an official with the Ministry of Natural Resources and Tourism who preferred anonymity.

  It is said that the new structure will comprise several presidential suites. The hotel owner is to build a new building in the city where the Court of Appeal will relocate, the sources said.

  Some officials have called the decision inconsiderate as it did not respect the fact that the building is regarded as one of the city's landmarks.

  "If the matter is expansion of the hotel, let it be done somewhere else, the building should not be tampered with," said another source.

  The Permanent Secretary in the Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development, Mr Patrick Rutabanzibwa, admitted to have heard the plans, but said his office was not officially informed.

  "I heard that there were talks between the government and the Kempinski (Hyatt Regency) owner over the change in the use of the building but I am not aware on the conclusion," he said.

  Mr Rutabanzibwa noted that the building's location suits the city's plans, adding that any move to demolish the structure will interfere with the plans.

  "It would be better that the building remains the same with or without changes in the use because that is how it is supposed to be according to the city plan," he said.

  Another official in the ministry noted that if the trend was to be entertained, all historical buildings in the city would be demolished. The Salamander building was also a historical building, but an investor pulled it down.

  "The Court of Appeal building, former Forodhani Hotel, housed the first hotel in the city before independence. It was then known as Dar es Salaam Club," said the ministry's official.

  The Minister for Natural Resources and Tourism, Mr Ezekiel Maige, said all the information on the matter would be given by the ministry's Permanent Secretary, Ms Maimuna Tarishi.

  When reached for comments, Ms Tarishi promised to respond on the matter in writing.

  The Hotel's Communication Officer identified by one name as Nasra declined to comment on the matter, saying she has no authority to speak on the iisue.

  Source : Dailynews

  Jamani si achukue na Ocean Road Hosp, huyu bwana wa Kempiski ni Mkali kachukua iliyokuwa ofisi ya usajili wa vizazi na vifo haikutosha kaja hapa anachukua mahakama walahi Ocean Road inaondoka sasa hivi. Ettiens nayo imekwenda na historia yake.

  Viongozi wetu, hawana uchungu hata kidogo na watu waliowachagua uchungu wao uko sana kwa wawekezaji, na sisi kama mazoba tunaangalia tuu na kuchelea, the history of Dar Es Salaam is being rubbed very fast.
   
 10. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  ccm hoiiiiiiiii
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Aliyefanya Mchezo mchafu Kilimanjaro, halafu Zanzibar na Sasa mahakama ya Rufaa, Hatuna uhakika sana juu ya Bilila lodge
   
 12. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Jengo la kihistoria la Mahakama ya Rufaa litabomolewa kupisha upanuzi wa hoteli ya zamani ya Kilimanjaro Kempinski ambayo imebadilishwa jina hivi karibuni na kuitwa Hyatt Regency – Kilimanjaro. Jengo hilo lilikuwa linatambulika kama jengo la kihitoria kupitia Gazeti la Serikali Namba 498 la mwaka 1995. Hata hivyo serikali imeamua kutolitambua jengo hilo tena kama la kihistoria

  Hata hivyo, baadhi ya watu wanalalamika kuwa kuvunjwa kwa jengo hilo la kihistoria kutaadhiri mwonekano ya Kivukoni Front ambapo pia kuna majengo mengine ya kihistoria yakiwemo yale ya Mahakama Kuu, Tanzania Bureau of Statistics na Mahakama Kuu ya Biashara. Msemaji kutoka Wizara Utalii na Maliasili ambaye hakutaka jina lake litajwe ameliambia gazeti la Daily News kuwa serikali imekubali mmiliki wa eneo la hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro kubomoa jengo hilo la kihistoria na kujenga jengo jipya ili kupanua hoteli hiyo. Jengo jipya litakuwa na presidential suites nyingi.

  Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Bw. Rutabanzibwa, amesema amesikia mpango wa kuboa hilo jengo hilo lakini bado hajataarifiwa kiofisi. Hata hivyo, amesema ingekuwa vizuri kama jengo hilo lingebakia kama lilivyo ili kuendana na plan ya jiji la Dar Es Salaam. Msemaji mwigine ndani ya wizara hiyo amesema kama jengo hilo la kihistoria litabomolewa, basi itabidi majengo mengine ya kihistoria nayo yabomolewe.

  Alipoulizwa Waziri wa Wizara ya Utalii na Maliasili, Mh. Ezekiel Maige, alisema taarifa zote zinapatikana kwa katibu wake, Bi. Maimuna Tarishi. Alipofuatwa Bi. Tarishi alisema atatoa habari kimaandishi. Afisa Mawasiliano wa hoteli ya Hyatt Regency anayejulikana kwa jina moja Nasra alipoulizwa alisema hana mamlaka ya kuongelea hili suala.
   
 13. s

  samoramsouth Senior Member

  #13
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  naichukia ccm, nachukia serikali inayoundwa na ccm, nachukia matendo yao machafu ya kuiuza nchi. Hakika mwisho wao uu karibu., hawa ni wakoloni ndani ya nci yao wenyewe,.
   
 14. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Tz kila kitu kinawezekana.
   
 15. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Usishangae kusikia Ikulu inabomolewa kupisha upanuzi wa jengo la EL. Kwa mtindo huu pengine sitaweza kurudi tena bongo. Bongo biwe kiumbe kisichokuwa na home
   
 16. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,080
  Likes Received: 1,116
  Trophy Points: 280
  Wanabomoa hili
  mahakama.jpg

  Wanajenga hili

  jipya.jpg

  Hii itasikitisha kama mpango huu utakamilika, haya ni majengo ya kwanza kabisa ya kihistoria kujengwa jijini na wakoloni
   
 17. 911

  911 Platinum Member

  #17
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Imefika hatua ambapo hakuna aina ya madudu yanaweza kufanyika Tanzania yakanistaajabisha!
   
 18. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Siyo muda mrefu ujao tutakuwa hatuna majengo yoyote ya kihistoria katika mji huu maana imekuwa kama kuna jitihada binafsi za KUFUTA HISTORIA YA JIJI HILI HASA KATIKA MAJENGO.........

  Hilo jengo lenyewe si majuzi tuu walilifanyia marekebisho makubwa???KODI YETU inazidi kuungua kama fegi!!!!! HAKIKA NCHI HII SHAMBA LA BIBI.....
   
 19. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #19
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,789
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  kwa nchi inayowajali na kuwasikiliza wawekezaji zaidi kuliko raia wake hilo kwao ni sahihi.kama anataka kujenga hotel si aende kilwa kivinje?
   
 20. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Tena hawa kubomoa ingekuwa poa maana hili jengo jirani wanasema LINATISHIA USALAMA WA IKULU...Kama vile wakati wanajenga kuliukuwa na KIZA na limekuja onekana wakati wanafunga A/Cs....
   
Loading...