Mwanagenzi
JF-Expert Member
- Sep 11, 2006
- 694
- 211
Jengo refu kuliko yote jijini Dar es Salaam limepewa jina la rais mstaafu Benjamin William Mkapa kinyume na matarajio ya wengi kuwa jengo hilo lingeendelea kuitwa Mafuta House.
Kwa wadadisi wa mambo ya kisiasa huenda jina hilo jipya likazusha gumzo kutokana na ukweli kwamba tangu rais Mkapa atoke madarakani na hususan kwa siku za karibuni amekuwa akituhumiwa na kuhusishwa na ubadhirifu na ukosefu wa maadili kama kiongozi mkuu wa nchi wakati wa utawala wake.