Jengo la gorofa nane lasimamiwa na aliemaliza darasa la saba

Hakuna lililowezekana Tanzania!! Ndiyo maana wawekezaji fake wameshatugundua. Wanakuja na mikataba tata, wakijua wakiyumbisha lugha kidogo chali!!! Wachina usiombe, watatuua.

Hivi mwenye jengo sitashangaa kuwa ni msomali!!!! Siku yale maghorofa ya Kariakoo yataanza kudondoka moja baada ya jingine itakuwa kizaaza.
 
Mimi nasema kama huyu bwana amelifikisha lile gorofa mpaka ya 8 na elimu yake ...wasimdharau wamempeleke veta hivi ni vichwa vilivyoitaji elimu vikaikosa mungu anawainua mwishon mwishoni ....so huyo mwenye mali kimbizaneni nae ila huyu kijana ningepata namba yake kesho yuko veta

Hakuna kitu mkuu, amelifikisha ghorofa ya nane lakini limeanguka.. so effort ni zero, kwa maana nyingine hafai kabisa. Fikiria kama lingeanguka wakati watu wameshaanza kulitumia je ungendelea kusimamia msimamo huo?
Mkuu science sio siasa ni either pass or fail hakuna cha kusema kajaribu wakati mmiliki keshapoteza mamilioni. Cha kushangaza wahitimu wa vyuo hawana kazi wakati jamaa la saba tu ni Boss wa mradi .... utani huu. Ujenzi sio tu kuweka tofali moja juu ya lingine.. kuna mavitabu na mavitubu just to about how to construct a good building foundation achilia mbali construction ya jengo zima.

Watu wanasoma na kusoma kwa ajili ya kazi hizo leo analeta jamaa wa std 7 lazima jengo lirudi chini just to remind us importance respecting others professional.

But angalau mhindi atakuwa kajifunza kuwa kile mtu anaweza kufikiri ni nafuu ukweli halisi ni kuwa ni ghali. Chukua Ma engineer walipe vizuri wakufanyie kazi yako kwa kadri ya viwango
 
Kuanzia mwaka juzi sithubutu kwenda Kariakoo naogope nisije kuangukiwa na maghorofa ya mchanga yanayoota kama uyoga pori!
 
nyie mnashangaa hiyo..!mi nilishaona jengo la shule ambalo tayari lina wanafunzi likijengwa kwa staili ya mwenye shule hiyo kumchorea injinia ambaye nadhani pia std 7, kwa mguu ardhini,yaani alikuwa anachora chora kwa mguu kumuelekeza huyo fundi jinsi anavyotaka liendelee!
 
magorofa ya kariakoo kama DOMINO,siku yataanza kuanguka mwanzo hadi mwisho wa mtaa.....in short ni accident waiting to happen!!!
 
ukishangaa ya firauni utaona ya musa, hawa jiji waliruhusuje ujenzi kuanza bila vigezo vinavyotakiwa kukamilika.? huko nako kuna matatizo
 
Back
Top Bottom