Ndugu wana JF, kuna jengo la gorofa kati ya Kituo cha Mafuta cha Bamaga na Maryland Bar upande wa kushoto kama unatokea Posta kwenda Mwenge liko hatua za mwisho. Yaani, karibu litafunguliwa. Cha kushangaza ni kwamba wanajenga 'car park' sehemu ya hifadhi ya barabara (yaani, wameacha tu kama mita 5 hivi kutoka barabarani. Je, ujenzi huu haukukiuka sheria za nchi za kujenga kwenye hifadhi ya barabara? Je, wamiliki wote walio karibu na barabara wanaweza pia kutumia sehemu ya hifadhi ya barabara kama alivyofanya mmiliki wa jengo hili au ndicho kile kinachoitwa "money speaks"? Naomba tujadili kama ujenzi kama huu ndio Dr Magufuli anaoutaka na kama siyo je, atakuwa na ubavu wa kuwaambia wabomoe hiyo 'car park'? Nawasilisha!