Jengo la ghorofa kati ya Bamaga Petrol Station na Maryland Bar barabara ya Posta-Mwenge kulikoni?

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,619
2,567
Ndugu wana JF, kuna jengo la gorofa kati ya Kituo cha Mafuta cha Bamaga na Maryland Bar upande wa kushoto kama unatokea Posta kwenda Mwenge liko hatua za mwisho. Yaani, karibu litafunguliwa. Cha kushangaza ni kwamba wanajenga 'car park' sehemu ya hifadhi ya barabara (yaani, wameacha tu kama mita 5 hivi kutoka barabarani. Je, ujenzi huu haukukiuka sheria za nchi za kujenga kwenye hifadhi ya barabara? Je, wamiliki wote walio karibu na barabara wanaweza pia kutumia sehemu ya hifadhi ya barabara kama alivyofanya mmiliki wa jengo hili au ndicho kile kinachoitwa "money speaks"? Naomba tujadili kama ujenzi kama huu ndio Dr Magufuli anaoutaka na kama siyo je, atakuwa na ubavu wa kuwaambia wabomoe hiyo 'car park'? Nawasilisha!
 
Ni sawa kabisa, naomba ubadilishe post weka ghorofa na si golofa ....

Mkutano wa wakandarasi unaoendelea ni forum muhimu kuadress vitu kama hivi na vinginevyo vinavyofanywa na wataalamu walioweka pesa mbele
 
Na lile la is it NSSF? pale makutano ya Bibi Titi na Morogoro Rd. Linakera kweli kweli.
 
ni kweli sheria inazuia kujenga ndani ya hifadhi ya barabara ila inazuia kujenga

1- permanent structure

2- kujenga bila kuwa na kibali cha tanroads na kibali ili kipitishwe inabidi uwasilishe michoro ya hicho unachotaka kujenga

3- unajenga au kuendeleza eneo la hifadhi ya barabara kwa ruhusa ya tanroads ..na sio kuwa unalimiliki wewe still litatumika na public kama kawaida ila wewe unakuwa ni kama "guardian angel" wa eneo hilo

4- ukijenga hizo temporary development na preferably isiwe jengo..i mean landscape both soft and hard landscape features pia ukiombwa kuzibomoa ufanye hivyo na kwa gharama zako

nimewasilisha kadiri ya uelewa wangu wa kitaalamu....
 
OK. Kumbe hizi 'reserved areas' za barabarani zinaweza kuendelezwa provided mtu ana kibali cha Tanroads na anakuwa 'guardian angel' wa eneo husika. Kama ni hivyo, mbona Dr Magufuli anakuja juu? Si angewaomba tu wahusika waombe vibali na wawe 'guardian angels' wa maeneo yao kama atakavyofanya mwekezaji huyu kama amepata hiyo ruhusa?
 
Hii nchi ime
avatar29297_6.gif
iwa
 
Ndugu wana JF, kuna jengo la gorofa kati ya Kituo cha Mafuta cha Bamaga na Maryland Bar upande wa kushoto kama unatokea Posta kwenda Mwenge liko hatua za mwisho. Yaani, karibu litafunguliwa. Cha kushangaza ni kwamba wanajenga 'car park' sehemu ya hifadhi ya barabara (yaani, wameacha tu kama mita 5 hivi kutoka barabarani. Je, ujenzi huu haukukiuka sheria za nchi za kujenga kwenye hifadhi ya barabara? Je, wamiliki wote walio karibu na barabara wanaweza pia kutumia sehemu ya hifadhi ya barabara kama alivyofanya mmiliki wa jengo hili au ndicho kile kinachoitwa "money speaks"? Naomba tujadili kama ujenzi kama huu ndio Dr Magufuli anaoutaka na kama siyo je, atakuwa na ubavu wa kuwaambia wabomoe hiyo 'car park'? Nawasilisha!
Acha umbea Umetumwa?
 
Ni sawa kabisa, naomba ubadilishe post weka ghorofa na si golofa ....

Mkutano wa wakandarasi unaoendelea ni forum muhimu kuadress vitu kama hivi na vinginevyo vinavyofanywa na wataalamu walioweka pesa mbele

Lakini si ulishamuelewa?
 
Acha umbea Umetumwa?

Afterall, sijui jengo lenyewe ni la nani: sijui kama ni la manispaa, la serikali au mtu binafsi. Anyaway, kama kusema nilichoona ndiyo kutumwa basi wasiosema wanachoona au wanaosema wasichoona hawajatumwa! Na wewe ni mmoja wao - unasema usichoona na kama ukiona huwezi kukisema ulichoona. Ni wazi kuwa ukiona mtu ananyanyasika na ukaulizwa kama umeona nini ili usije ukaambiwa umetumwa na ili kuonesha hujatumwa utasema hujaona kitu. Hauko peke yako. Nchi yetu imejaa watu wa aina yako! Keep it up if you profit from not saying what you see!
 
Angalia vizuri, anachofanya huyo jamaa ni garden tu na wala sio parking. Ni sawa na jarini zake wanaouza maua na miti. Mi nadhani ni vyema kwani anapendezesha eneo hilo. Ni kama pale Nakiete House
 
nadhani ambalo ni kero zaidi ni lile la pale opposite na pegeut house maana naona kama liko barabarani na hata jinsi ya kuingia pale kutakuwa na usumbufu sana ...... lile jengo pale bamanga wizara inasubiri wamalize ili waje wabomoe baadhi ya sehemu ya parking ili waonekane wanafanya kazi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom