Jengo jipya la Bunge la Tanzania

Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,160
1,720
68201.jpg
Najua kama kawaida wengi wetu tutapiga kelele saaaana kuhusina na hili jengo, ila limeshajengwa!

Mimi ningependa kusikia hoja za mtu YEYOTE YULE tafadhali, anayeweza kueleza huu umati sababu za kugharamikia ma millioni ya fedha ili kujenga hili jengo la kifahari!

Sawa tutalalamika, lakini nakataa kukubali kwamba viongozi wetu ni wajinga, na wabinafsi kwa kiasi kile ambacho sisi humu ndani tuna waelezea! Hivyo basi natoa wito kwa yeyote yule aje na ku justify this one move by the government. (Ila hii ilipitishwa wakati wa BWM)

fikiraduni, mzee wa kuangalia pande zote, pande ya pili ya hii kitu ni nini? Viongozi hawawezi kuwa wanyama hivi!

Inauma sana kwasababu hospitali hapo hapo siko hivi...
04.jpg
 
Inasikitisha, ila sasa tutafute njia au namna ya kufanya huko mbele

Jengo lishajengwa kulalamika haisaidiii

FD
 
Ni kweli FD,
ninamini njia mojawapo kuu ya kuweza kujua lakufanya sasa kwa ajili ya huko mbeleni ni kuweza kuelewa utofauti kati yetu na viongozi wetu kwenye fikra.

Hawa viongozi si ndio sisi sisi huko kesho, kwanini basi maamuzi yao ni yakijinga?

Kitabu cha the Art of War by Sun Tzu kinasema:
"Know thy self, know thy enemy. A thousand battles, a thousand victories.”

I want to know these "enemies"!
 
Nyamgluu said:
.....Najua kama kawaida wengi wetu tutapiga kelele saaaana kuhusina na hili .....YEYOTE YULE tafadhali, anayeweza kueleza huu umati sababu za kugharamikia ma millioni ya fedha ili kujenga hili jengo la kifahari!.....lakini nakataa kukubali kwamba viongozi wetu ni wajinga, na wabinafsi kwa kiasi kile ambacho sisi humu ndani tuna waelezea! Hivyo basi natoa wito kwa yeyote yule aje na ku justify this one...
Inauma sana kwasababu hospitali hapo hapo siko hivi..

Hapa nadhani tukubaliane kuwa ubinafsi ndo unawapeleka huko kwenye uongozi na wala si kutenda haki kwa waTZ wote.

Kitu kingine ni kuwa je ushaona kiongozi akienda japo kufanya checkup kwenye hospitali zetu???....Kama mambo yenyewe ni kama kwenye hiyo picha ya hospitali unadhani watadhubutu??...mambo yote, hata kupimwa miwani wanafanyia majuu...

Hospitali hizi ni zetu sisi. Yaani walengwa wa hizi hospitali ni sisi, wala siyo wao. Walengwa wa hilo jengo ni wao wala siyo sisi!
 
Back
Top Bottom