Jengo hili refu la ghorofa CCM wameshindwa kumaliza liwe kitega uchumi?

Halo JF siasa.

Ktk pitapita zangu nimefika Singida mjini. Kuna jengo refu zaidi ya yote hapo mjini lina ghorofa zaidi sita.
Jengo hili naambiwa ni Mali ya CCM na lilianza kujengwa mwanzoni mwa miaka ya 1980's.

Naambiwa lilijengwa pamoja na uwanja wa mpira wa miguu wa Namfua, enzi hizo RC Namfua ndiye mkuu wa mkoa Singida.
Naambiwa wajanja walikula hela sana na jengo halikuisha hadi Leo. Pia uwanja japo sikufika naambiwa haujaisha vizuri.

Hakika jengo hili likiisha litaupendezesha mji wa Singida kwani ndilo refu kuliko zote na linaonekana kwa mbali na kwa jinsi lilivyo linaufanya mji kuonekana choka mbaya.

Wenyeji wanadai Billionaire Mo Dewji hakujiangaisha ktk kipindi chake cha ubunge kushughulikia likamilike. Pia wanahoji je Mwl Mussa Sima ambaye ni mbunge wa sasa na naibu waziri Mazingira na Muungano atalikamilisha ikiwa Mo Dewji alishindwa?

Pia wanahoji Rais Magufuli aliyetelekeza Maabara shule za secondary na kuwa Magofu ataliweza au ataangazia zaidi ndege, Reli, bandari, barabara, vituo vya Afya nk?
Mali ya urithi huwa haina uchungu... upole wa kutohoji wa watanzania ndio uliosababisha ccm kupora na kujimilikisha mali ambazo wananchi walijitolea kuzijenga... mwisho wa siku zinawashinda kutunza. Tazama kuanzia viwanja vya mpira mpaka majengo wanavyomiliki watuambie walitoa wapi pesa za kununulia mali hizo... kama wana uchungu navyo kwanini vijae nyufa na kuchakaa?
 
Mali ya urithi huwa haina uchungu... upole wa kutohoji wa watanzania ndio uliosababisha ccm kupora na kujimilikisha mali ambazo wananchi walijitolea kuzijenga... mwisho wa siku zinawashinda kutunza. Tazama kuanzia viwanja vya mpira mpaka majengo wanavyomiliki watuambie walitoa wapi pesa za kununulia mali hizo... kama wana uchungu navyo kwanini vijae nyufa na kuchakaa?
Shida kubwa ni kutojali sambamba na upigaji
 
Majengo na viwanja vyote vimekuwa vikijengwa kwa fedha za serikali na michango ya wananchi kwa nguvu bila ridhaa yao! Hivi sasa ni ngumu kuwalazimisha watu kuchangia na pia si rahisi sana kuchota fedha za serikali ingawa kwa ujenzi wa uwanja wa Chato imewezekana!
Kuchota inawezekana bila shida wala kuhoji.
 
Ngoja tutengeneze "uhaba feki" wa sukari au mafuta ya kupikia,kampuni ya chama iagize,hizo hela tumalizie majengo yetu, yapo mengine kama Ali Hassan Mwinyi Stadium,Tabora, Kagera pia kuna jengo halijaisha
Upigaji kwenda mbele, wapo waliojenga majumba yao kupitia miradi hiyo.
 
Back
Top Bottom