Jenga tabia ya kuaga kila unapotoka kwa kutoa taarifa sahihi

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Habarini wakuu.

Ni vyema kuaga kwa kutoa taarifa sahihi kwa mtu/watu wako wa karibu kwa kutoa taarifa sahihi kila unapotoka/ kusafiri/ kuitwa kwenda mahali fulani.

1. Ukitoka out na washikaji aga na utoe taarifa sahihi

2. Ukisafiri aga na utoe taarifa sahihi

3. Ukiitwa na mtu/ watu kwa mazungumzo ya kibiashara/ kikazi aga na utoe taarifa sahihi

Unaweza kutoa taarifa sahihi kwa mtu wako wa karibu sana mfano mke/ mme, mzazi, mtoto, ndugu, rafiki yako...kutegemeana na maudhui ya unakokwenda na unachoenda kukifanya.

Taarifa za kuaga:
1. Jina la mahali unakokwenda

2. Mtu na address ya mtu unayeenda kukutana nae. Mtambulishe mwenzio aina ya mtu unayeenda kukutana nae

3. Muda utakaokuwa haupo


Taarifa hizi zitarahisisha upatikanaji wako pindi utakapopatwa na matatizo. Pia utawapunguzia watu gharama na kuokoa muda wa kukutafuta ama kukusaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengine kazi zao bila uongo,mambo hayaendi.

Ni lazima kuua wajomba,mashangazi,mabamdogo nk,vinginevyo hutoki kwenda kokote.

Hata hivyo bado ni muhimu kusema ukweli kwa unayemwamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom