Jenga mtazamo wako uanze kwa ushindi

mwakavuta

Member
Sep 22, 2020
99
301
Badili mtazamo wako uanze kwa ushindi.

perception.jpg


Kuna msemo wa kingereza unasema kuwa “if there is no enemy within outside enemy can do no harm” yaani kama hakuna adui ndani adui aliyeko nje hana madhara.

Unapanga kuanza kufanya nini, kwa njia gani, malengo yako ni nini na unapanga kuanza lini? Ni mara chache sana tunafanikiwa kujiuliza na kujibu maswali haya kwa usahihi kwa sababu wengi hawajui kuwa ni muhimu au hawajui kabisa kuwa yapo.

Malengo mengi tuliyojiwekea yanashindwa kufikiwa kwa sababu ya kukosa majibu ya maswali haya. Kwa mtazamo wangu maswali haya yanatuwezesha kujua adui ni nani na yuko wapi, nje au ndani. Asilimia tisini (90%) ya adui anayekwamisha mafanikio ya mtu yuko ndani ya mtu mwenyewe watu wanaotuzunguka wanakwamisha kwa asilimia kumi tu na si kila kitu wanapata nafasi ya kukwamisha.

Unataka kuanza biashara au mradi mpya unaanza kujiuliza kama kuna mtu anafanya biashara kama yako? Alifanikiwa? Kama hajafanikiwa unaacha kuifanya na malengo yako yanaishia hapo kwa sababu walijaribu kupita njia kama yako hawakufanikiwa. Hapa adui si aliyeshindwa kufanikiwa kwenye biashara au mradi unaotaka kuuanzisha ila ni wewe mwenyewe kwa kutafsiri Maisha yako kutokana na watu wengine.

Watu wengine kushindwa kufanikiwa haina maana kwamba na wewe utashindwa. Unachotakiwa ni kujenga mtazamo na tafsiri inayoendana na malengo unayojiwekea kutoka ndani yako na si kwa mtu mwingine. Hakuna sababu ya kutafuta kisingizio kinachoitwa kushindwa kwa mtu mwingine wewe ndio unahusika na kushindwa au kufanikiwa kwako.

Ni jambo la kawaida sana kukuta mtu amepata wazo la biashara au mradi wowote na kuomba ushauri kwa mtu kisha akapewa ushauri ambao unamkatisha tamaa kisha akaamua kuufuata na kuacha kabisa mipango yake. Hapa kosa si aliyetoa ushauri bali aliyeomba ushauri kwa sababu anayeombwa ushauri hana taswira halisi na maono yako wewe. Sipingi kuomba ushauri kwa watu wengine, ni jambo jema lakini ni muhimu kuchagua watu wenye itikadi na mitazamo kama yako ili wakusaidie.

Kuna msemo unasema kuwa ”huwezi kuomba ushauri wa kununua Ferrari kwa dereva wa Toyota” katika hali hii lazima dereva wa Toyota atakukataza kununua Ferrari kwa hana uelewa mzuri kuhusu Ferrari na hajui unachokitaka kwenye Ferrari. Majibu atakayokupa ni kuwa Ferrari inauzwa bei ghali, inakula sana Mafuta, hutapata vipuri au mafundi wazuri. Kumbe hilo sio tatizo kwako unachohitaji ni kuwa wa tofauti (unique), mwendo au usalama ambavyo vyote yeye havijui. Katika hali hii utajikuta unatafsiri Maisha yako ya kumiliki Ferrari kwa Maisha ya mmiliki wa Toyota.

Usisubiri muda ufike ili utimize ndoto zako kwa sababu hakuna muda sahihi wa kuanza kitu, muda sahihi ni pale unapofikiri kuhusu jambo husika na ndio wakati wa kuanza. Roma haikujengwa kwa siku moja lakini kila siku walikuwa wanafyatua matofali. Unachohitajika si kusubiri siku upate pesa za kutosha ndo uanze biashara au malengo yako bali kila siku vyatua matofali jenga ufahamu na mtazamo wako kuhusu malengo yako, tafuta ushauri kwa watu sahihi, usisubiri mambo yako yakae vizuri ndo uanze kufanya mipango yako.

Mwanzoni ni pagumu siku zote ili uanze unahitajika kuwa mgumu vilevile na kuamua kuanza hivyohivyo. Benjamin Bockowsk alisema kuwa “If you go, go all the way otherwise don’t even start” anza leo kwa ujasiri kila kitu kitakuwa sawa mbele ya safari. Jipe Imani kuwa hakuna kitakachoharibika na kama kitaharibika utakuwa tayari kujua chanzo cha tatizo na kurekebisha.

perception.jpg

#DESTINY_MAKERS #DARE_TO_DO #IT_IS_ALL_ABOUT_YOU
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom