Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu

GreenHouse

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
280
262
Nauza Materials na kusadia ujenzi wa Greenhouse za ukubwa mbali mbali.

Kwa sasa nina materials zinazoweza kucover greenhouse ya ukubwa wa mita nane kwa mita kumi na tano (8x15m), Zina uwezo wa kuzuia jua, kuzuia wadudu na vihatarishi mbali mbali vya mazao.

Bei ni Mil2.5 kwa materials pekeyake yaani 1/8 of an ancre drip lines, Polythene Cover (UV400 Protected sheets), 70% Micron insect Netting...Hizi zitakuwezesha kujenga Greenhouse yako bila matatizo. Kitakachohitajika kutoka kwako ni Wooden Poles (nguzo kama zinazojengewa baa za makuti nk), tanki la lita 500 la maji na maji ya uhakika.

Ntakupatia mafundi na muongozo mzima wa kujenga greehouse yako ili kufanikiwa.

Faida za kulima katika greenhouse ni nyingi mno, ikiwemo matumizi mazuri na sahihi ya ardhi, kwani kiwanja cha ukubwa wa mita 8x15 kinaweza kukupa Nyanya hadi Tani 10 kwa mwaka, Pilipili hoho tani 8 kwa mwaka na mazao mengine mengi yanayolimwa katika controlled environment.

Kuna wataalamu wa kutosha hivi sasa hapa Dar es Salaam wanaoweza kukupa muongozo, mbegu bora na fertilizers za uhakika tuwasiliane kwa simu namba 0785 409821 ili kupeana muongozo.

Karibuni sana.
Ili uweze kufanikiwa katika kilimo hiki, unahitaji maji ya uhakika minimum lita 200 kwa siku kwa ajili ya kumwagilia nyanya kwa matone, Nitakupatia mabomba (driplines) zitakazokuwezesha kufanikisha hili.

NB: Kumbuka Greenhouse inajengwa kwenye eneo lililo wazi, lisilo na miti mirefu inayozuia jua.

Pia ni muhimu kufanya Soil Test na Water Test ili ujue ni kipi unahitaji kuongeza kwenye ardhi yako ili upate mazao ya uhakika naweza kukusaidia kufanya soil na water test kwa gharama nafuu kabisa kutoka nchi ya Jirani (kenya). Gharama ni 250,000 kwa huduma hii pekeyake (Complete Soil analysis & Water Test).

NB::: UJENZI WA GREENHOUSE YA MFANO UMEKAMILIKA. IPO MIKWAMBE KIGAMBONI::: KARIBUNI SANA.

Greenhouse-4.jpg Greenhouse-11.jpg Greenhouse-12.jpg Greenhouse-10.jpg Greenhouse-13.jpg Greenhouse-14.jpg

Kuna watu wengi sana wamenipigia na kuomba niwasaidie kufanya mchakato wa kuandika mchanganuo wa kuomba mkopo bank (bankable business plans and proposals) au taasisi za fedha ili wafanikishe mradi huu.

Habari njema ni kwamba, tumeingia makubaliano maalumu na kampuni moja hapa nchini (Biznocrats consulting enterprise) inayojihusisha na kuandika michanganuo ya kibiashara, ushauri wa kifedha, accounts nk na wamekubali kuwaandikia wateja wetu wote michanganuo hiyo kwa gharama ya asilimia moja tu (1%) ya mkopo Minimum 500,000 na wanakuhakikishia hautokosa mkopo wa aina yoyote.

Kama unahitaji huduma hii, tuwasiliane ili tuweze kufanikisha hili pamoja.

Karibuni sana.
 
mama na kwa hapo Dar kuna sehemu umeshajenga hayo mabanda?tuweze kushudia kwanza?
 
Last edited by a moderator:
Safi mama na, me ntakua mteja wako siku si nyingi ngoja nimalize miche yangu niliyopanda kwenye open field. Safi sana na gharama yako ni nafuu compared na ya Barton

Sent from my BlackBerry 9930 using JamiiForums
 
Safi mamaNa, me ntakua mteja wako siku si nyingi ngoja nimalize miche yangu niliyopanda kwenye open field. Safi sana na gharama yako ni nafuu compared na ya Barton

Sent from my BlackBerry 9930 using JamiiForums

Kilichonifanya nianzishe hii project ni baada ya kwenda balton na kuambiwa gharama ni 6.2m without tax, nikatafuta supplier wa material na kuanza kujenga mwenyewe. nimefanikiwa kupunguza gharama kwa asilimia 50. Pia greenhouse inaguarantee ya kuishi miaka 10.

Nb: usitumie miche iliyotoka open field kuilima kwenye greenhouse. the whole concept of a controlled enviroment itakuwa haipo. utahamisha worms na backteria kutoka nje uwalete kwenye greenhouse yako ukose kupata mafanikio tarajiwa.
Hakikisha unakuza miche kwa kutumia nursery set maalumu na udongo maalumu (potting mix) ndani ya greenhouse. kwa kufanya hivi utakuwa na uhakika asilimia 100 ,miche yako iko salama.

Karibu sana.
 
Hahahahha, karibu sana katika ushindani wa biashara. tukiwa wengi tutawalazimu wasambazaji wa material kutushushia bei huko asia.
 
Kilichonifanya nianzishe hii project ni baada ya kwenda balton na kuambiwa gharama ni 6.2m without tax, nikatafuta supplier wa material na kuanza kujenga mwenyewe. nimefanikiwa kupunguza gharama kwa asilimia 50. Pia greenhouse inaguarantee ya kuishi miaka 10.
Kweli kabisa balton wako juu mno kama kupunguza gharama

ni bora umtafute fundi muajiriwa pale balton umlipe yeye atoe utaalamu tu alafu wewe unamtafutia vijana wa kumsaidia kucompose system nzima.

Vifaa vinajulikana na vinapatikana hapa nchini tena kwa ruzuku ya serikali hata ukitaka kuimport bado bei ni cheap.

kama ni soil analysis na water test maafisa ugani wa serikali wanaifanya hiyo kazi bure labda uwalipe fadhila tu.

Lakini hiyo ni moja kati ya huduma za bure kwa mkulima

Ukifanya hivi unasave zaidi ya 50% ya price ya balton.
 
Mkuu soil analysis na water test wanafanya kupitia lab ya nani??? Mamlaka ya maji pale ubungo wanafanya water test kwa 150,000 na majibu ni baada ya wiki sita. Kenya bei hiyo hiyo majibu wiki moja.

Soil analysis nilishaenda mpaka sua, majibu hakuna. ni longo longo kwenda mbele... utakaa hata miezi nitatu usipewe jibu la uhakika katika suala hili ni bora uingie gharama kwani ndio msingi mzima wa greenhouse unapolala compitition ya vyakula kwa mimea ni kubwa sana kwenye condensed enviroment.

Hivyo ni lazima ujue udongo una mapungufu gani ili uweze kuulisha chakula (fertilizers) zinazostahili maji pia kama ph level imekosewa unaweza kujikuta unaunguza nyanya zako zote kwa acid na mbolea kuna mzee hakusikiliza huu ushauri akanunua ya balton, sasa hv kageuza greenhouse yake stoo.

Nb: mafundi wa balton wana install steel tunnels, hawajui wooden ones...
Nimeshapita kote huko na mwisho nimeamua kushirikiana na wakenya....
Kuhusu gharama za films, kuwa makini sana na mchujo wa uv rays, usijekuuziwa nylon...
Otherwise, ni kweli kabisa ukijenga mwenyewe unasave 50%.

Karibuni sana.
 
Kweli mamaNa ni muhimu kujua acidity na alkaline ya maji pia macro na micro nutritious minerals kwenye udongo ili kubalance mahitaji ya mmea kuendana na soil profile and texture.

Lakini kuna lab flani walifungua Oxfarm Arusha sielewi maeneo gani kuelekea manyara hii process walikuwa wanaifanya bure nafkiri ata selian na SUA wanafanya.

Ila sio kwa gharama kubwa kama balton.
Point yangu ni unafuu.
 
Najenga demo site sasa hivi hapa Dar, ikikamilika ntaupdate uzi huu.
Ntafatilia kuhusu oxfam pia, asante kwa taarifa. Tanzania imeoza sasa hivi, ni muhimu sana kuwa makini na kuchagua repolutable people to work with mbegu feki, mbolea feki na madawa feki yamejaa sana nchini hapa, imekuwa ni vilio na mayowe ya kila siku kwa wakulima.
 
Najenga demo site sasa hv hapadar, ikikamilika ntauodate uzi huu.
Ntafatilia kuhusu oxfam pia, asante kwa taarifa. Tanzania imeoza sasa hv, ni muhimu sana kuwa makini na kuchagua repolutable people to work with...mbegu feki, mbolea feki na madawa feki yamejaa sana nchini hapa, imekuwa ni vilio na.mayowe ya kila siku kwa wakulima.

Nchi zetu wanazoziita third world ingenuine products za zimemeza soko kwa kutokuwa na regulative borders kuzuia hizi products na sio industrialized kwenye kila jambo ndo mana tunadharaulika kwa kuletewa bidhaa fake mpaka radar, ndege ya Rais.
 
Hahaha kweli bwana, tulinunua radar used kwa pound mil 38, mpaka wazungu wakatuonea huruma na kutuambia tumepigwa pound mil 26, na wakaturudishia masimbi yetu...
 
Kilichonifanya nianzishe hii project ni baada ya kwenda balton na kuambiwa gharama ni 6.2m without tax, nikatafuta supplier wa material na kuanza kujenga mwenyewe. nimefanikiwa kupunguza gharama kwa asilimia 50. Pia greenhouse inaguarantee ya kuishi miaka 10.

Nb: usitumie miche iliyotoka open field kuilima kwenye greenhouse. the whole concept of a controlled enviroment itakuwa haipo. utahamisha worms na backteria kutoka nje uwalete kwenye greenhouse yako ukose kupata mafanikio tarajiwa.
Hakikisha unakuza miche kwa kutumia nursery set maalumu na udongo maalumu (potting mix) ndani ya greenhouse. kwa kufanya hivi utakuwa na uhakika asilimia 100 ,miche yako iko salama.

Karibu sana.
Nilipita pia balton nikaambiwa huo mlolongo wa gharama nikaahirisha kwa muda vipi majadiliano ya gharama yapo ikiwa mtu atataka kufanya nawe kazi?
 
Nilipita pia balton nikaambiwa huo mlolongo wa gharama nikaahirisha kwa muda..... vipi.. majadiliano ya gharama yapo ikiwa mtu atataka kufanya nawe kazi?
Gharama za materials ni none negotiable kwasababu sizitengenezi mimi, Lakini kwenye installation cost gharama inazungumzika kwasababu ni makubaliano kati yangu na mafundi. Pia Kama una mbolea yako au unaweza kupata lorry la mbolea sehemu, ni moja kati ya savings, au kama unaweza kuwa na tank la lita 200-500 ni vema zaidi lakini hiyo 2.5m ni ya kununua materials muhimu (polythene films, insect netting, drip lines na nursery set kwa ajili ya kukuzia miche ndani ya greenhouse)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom