Jenga gorofa moja kwa gharama nafuu

Kila siku maghorofa yanachipua kama uyoga, nikihitaji ushauri nitaomba huko…. humu wengi hata kodi ya pango mtihani tunastahili vipi kujadili ghorofa?
😁😁 Kwamba maghorofa yanachipuka Kama uyoga?hebu jaribu kulichipua na Lako fasta fasta mkuu tuje tusafishie nyota.
 
Wengi wanaogopa sana kujenga ghorofa wakizani labda mpaka uwe na pesa nyingi ndio ujenge. Ukiamua hakuna kinachoshindikana, kama umeweza kujenga nyumba ya chini,jua una uwezo pia wa kujenga ghorofa. Fanya yafuatayo kutimiza ndoto zako:-
  • Weka kwenye michoro wazo la nyumba yako (jichoree mwenyewe unavyotaka)
  • Tafuta injinia akuandalie BOQ (idadi ya matirio yatakayotumika),michoro, na ramani
  • Tafuta kibali cha ujenzi- itategemea na eneo uliopo
  • Anza kununua mawe, kokoto nyeusi, mchanga, matofari ya kuanzia, nondo. simenti-kwa ajili ya msingi
  • Nenda maeneo yanapojengwa magorofa, na umchukue fundi unayemuona anapiga kazi
  • Ingia makubaliano na huyo fundi-akupatie gharama ya msingi, ikiwezekana mkubaliane kwa siku.
  • Anza kazi ya msingi.
  • Weka rafu/ zege kwenye msingi
  • Anza kupandisha nguzo na tofali kwa awamu awamu kutokana na mzunguko wako wa pesa- unaweza kumtumia yule fundi wa mwanzo au ukatafuta mwingine
  • Ukifika kwenye lenta-inabidi upumzike
  • Anza kukusanya nondo,kokoto nyeusi, simenti,misumari
  • Angalia pa kukodi 'plate' au 'marine board',kwa siku gharama yake huwa ni sh. 400/= kwa moja, pia kukodi mirunda, mbao; inategemea na sehemu ulipo.
  • Mwite fundi kwa kazi ya 'slab'- hapa ndipo huwa pagumu sana kwenye ghorofa
  • Akishamaliza slab, pumzika utafute nguvu
  • Endelea na ujenzi wa juu
  • Paua mjengo wako
  • Endelea na hatua zingine za 'finishing'
  • Baada ya hapo jipongeze....kwa kutembelea mbuga za wanyama
Kuna haja gani kujenga ghorofa?
 
Nataka kujenga mnara wa kuweka tank za maji za litte 5000 mbili, yaani 10000 litres.

Nitatumia mbinu maana maelekezo ni mengi na yanatishia budget saana.. yaani msingi tu million tatu
 
Nataka kujenga mnara wa kuweka tank za maji za litte 5000 mbili, yaani 10000 litres.

Nitatumia mbinu maana maelekezo ni mengi na yanatishia budget saana.. yaani msingi tu million tatu
Gharama kubwa sana ukifikia hatua ya kuya fanyia installation matank nistue nita kufanyia kwa ubora na kwa bei nafuu sana
 
Msikatishane tamaa palipo na nia lolote linawezekana. Hata hao walimu na manesi wanaweza kujenga hivyo vighorofa vya kuzeekea.
 
Back
Top Bottom