Jenga gorofa moja kwa gharama nafuu

Wengi wanaogopa sana kujenga ghorofa wakizani labda mpaka uwe na pesa nyingi ndio ujenge. Ukiamua hakuna kinachoshindikana, kama umeweza kujenga nyumba ya chini,jua una uwezo pia wa kujenga ghorofa. Fanya yafuatayo kutimiza ndoto zako:-
  • Weka kwenye michoro wazo la nyumba yako (jichoree mwenyewe unavyotaka)
  • Tafuta injinia akuandalie BOQ (idadi ya matirio yatakayotumika),michoro, na ramani
  • Tafuta kibali cha ujenzi- itategemea na eneo uliopo
  • Anza kununua mawe, kokoto nyeusi, mchanga, matofari ya kuanzia, nondo. simenti-kwa ajili ya msingi
  • Nenda maeneo yanapojengwa magorofa, na umchukue fundi unayemuona anapiga kazi
  • Ingia makubaliano na huyo fundi-akupatie gharama ya msingi, ikiwezekana mkubaliane kwa siku.
  • Anza kazi ya msingi.
  • Weka rafu/ zege kwenye msingi
  • Anza kupandisha nguzo na tofali kwa awamu awamu kutokana na mzunguko wako wa pesa- unaweza kumtumia yule fundi wa mwanzo au ukatafuta mwingine
  • Ukifika kwenye lenta-inabidi upumzike
  • Anza kukusanya nondo,kokoto nyeusi, simenti,misumari
  • Angalia pa kukodi 'plate' au 'marine board',kwa siku gharama yake huwa ni sh. 400/= kwa moja, pia kukodi mirunda, mbao; inategemea na sehemu ulipo.
  • Mwite fundi kwa kazi ya 'slab'- hapa ndipo huwa pagumu sana kwenye ghorofa
  • Akishamaliza slab, pumzika utafute nguvu
  • Endelea na ujenzi wa juu
  • Paua mjengo wako
  • Endelea na hatua zingine za 'finishing'
  • Baada ya hapo jipongeze....kwa kutembelea mbuga za wanyama
Ni busara kumtafuta engineer yeye ndio akasimamia kazi yako..na yeye ndio unaweza muachia jukumu la kukutafutia fundi mzuri..client wengi hawana uelewa na ujenzi hivyo wanapaswa kuongozwa na wataalamu ujenzi.

Michoro huwa inaandaliwa na Architect, Quantity surveyor anaada gharama za ujenzi..then Engineers wana design ( Msingi, beams Nguzo, Slabs, Ngazi etc....Ujenzi wa ghorofa ni tofauti na nyumba yakawaida....

Msingi unatakiwa uwe imara kuishikilia nyumba...na aina ya msingi unakuwa selected kwa kuangalia aina ya udongo uliopo ( soil testing lazima ifanyike) yote haya hufanyika ilikujua ni aina gani ya msingi utatakiwa kujengwa.....

Ukijenga bila utaratibu ni kuweka hela yako at risk
 
Natamani Kuja Kujenga Ghorofa Hata Ya Flow Moja Ila Iwe Standard Sio Ili mradi....
Changamoto niliyo nayo ni nitaanzia wapi?kwa sababu wanatoa conditions gani ili upewe building permit ya ghorofa
 
Natamani Kuja Kujenga Ghorofa Hata Ya Flow Moja Ila Iwe Standard Sio Ili mradi....
Changamoto niliyo nayo ni nitaanzia wapi?kwa sababu wanatoa conditions gani ili upewe building permit ya ghorofa
Tafuta mtaalamu wa michoro na ramani, inaweza isizidi laki 2; baada ya hapo nenda halmashauri/manispaa kwa ajili ya kibali, haitazidi laki 2.. baada ya hapo nunua malighafi
 
Ni vizuri pia kuwa na nyumba ya ndoto yako, ingawa changamoto huwa bei ya malighafi; mfano mimi nondo nilikuwa nachukulia kiwandani ili kupunguza gharama, unakuwa unauziwa kwa tani.
Mkuu nondo ulinunulia kiwanda gani
 
Back
Top Bottom