Jeneza Lenye Kichwa Cha Mbuzi Lakutwa nje ya Nyumba Mbezi Luis

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Jeneza Lenye Kichwa Cha Mbuzi Lakutwa nje ya Nyumba Mbezi Luis, Dar es Salaam

Mkazi mmoja wa Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, ameamka asubuhi na kukuta jeneza likiwa limewekwa mbele ya mlango wa kuingilia kwenye nyumba yake.

Tukio hilo limetokea huko Mbezi Luis nyumbani kwa Amina Mwakangale.

NIPASHE Jumapili ilishuhudia jeneza hilo lililofunikwa kwa kitambaa cheusi kwa juu na kufungwa kamba tatu, yaani upande wa mbele wa jeneza, katikati na mwishoni. Jeneza hilo la ukubwa wa kumwenea mtoto wa miaka sita hivi, lilikuwa limepakwa matope sehemu za juu kilipofunikwa kitambaa na pembeni kila upande.



Akisimulia, Mwakangale alisema alikuwa amelala kabla ya kuja kuamshwa na binti anayeishi naye na kuelezwa kilichokuwa mlangoni mwa nyumba yake. Bnti huyo alilazimika kumpa taarifa hizo baada ya kushindwa kufungua mlango kutokana na hofu baada ya kuliona jeneza hilo karibu kabisa na mlango, "Kama unavyoona, nimeamshwa asubuhi na kukuta hili jeneza, tulishindwa kutoka nje kupitia mlango huu mkubwa na hivyo kulazimika kupitia mlango mwingine," alisema Mwakangale.

Kutokana na hali hiyo, walipata hofu na kuamua kutoligusa jeneza kabla ya kutoa taarifa polisi. Kabla ya kuwapa taarifa polisi, walimjulisha mjumbe wa mtaa, Hussein Kigola, ambaye naye baada ya kufika eneo la tukio alishauri kutofanyika lolote mpaka polisi watakapofika, "Haya ni mambo ya kishirikina mwanangu, sijui ni nani huyu na nini anachotafuta kwangu, nimeona nisifanye lolote mpaka polisi waje ndio wafungue tuone kilichowekwa ndani," alisema Mama huyo kwa masikitiko makubwa.

Polisi wa Kituo cha Mbezi kwa Yusufu walifika eneo la tukio wakiwa na gari aina ya Toyota Landcruiser lenye namba za usajili PT 1412. Baada kumhoji kwa muda mfupi mama mwenye nyumba pamoja na mjumbe, polisi hao wakiwa na mkuu wao wa kituo walifungua jeneza kwa hadhari kubwa. Walilikata kamba za katani zilizofungwa na kuondoa kitambaa cheusi, ambapo ndani kulikutwa kichwa cha mbuzi mweupe chenye pembe ndefu, shina la mgomba pamoja na hirizi nyekundu.

Mwandishi wa NIPASHE Jumapili alishuhudia kichwa hicho cha mbuzi kikiwa upande wa mbele ndani ya jeneza, na nyuma yake shina la mgomba, huku pembeni ndiko ilikowekwa hirizi. Baada ya hapo Polisi walilibeba jeneza hilo na kuondoka na mama mwenye nyumba pamoja na mjumbe ili kwenda kuhojiwa kwa kirefu juu ya tukio hilo.

Aidha, mjumbe wa eneo hilo Kigola, alisema katika maisha yake yote anakaribia miaka 70 hajawahi kuona tukio kama hilo, huku majirani nao wakionekana wazi kushtushwa kwa kiasi kikubwa na tukio hilo.

Majirani hao waliohojiwa na NIPASHE Jumapili, walisema inashangaza jinsi watu hao walivyoweza kupita na jeneza hilo mpaka kwenye nyumba ya Mwakangale. Kushangazwa huko kunatokana mazingira ya eneo kwa vile usiku kuna walinzi wanaolinda mashine za umeme za kufyatulia matofali ambazo ziko hatua kama 20 toka nyumbani kwa Mwakangale lakini hakuna aliyeweza kuona watu hao.
 
Hawalipe wanaomdai au kama zamu yake ya kutoa mtoto kwa wachawi amtoe tu ndo solution.
 
Back
Top Bottom