Jenerali Zawadi Madawili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jenerali Zawadi Madawili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kichuguu, Sep 27, 2012.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Maj. Gen Zawadi Madawili ni mwanamke ambaye binafsi nimekuwa namheshimu sana maisha yangu yote tangu nimfahamu wakati aliopongoza mbio za mwenge mwaka 1975 akiwa luteni wa jeshi la wananchi wa Tanzania. Baada ya mimi binafsi kupitia mafunzo ya kijeshi ndipo nilipozidi kumheshimu sana mama huyo.

  Serikali ya Tanzania ingefanya jambo moja la maana sana kwa kumpa nafasi pekee Jenerali Madawili baada ya kustaafu kwake jeshini awe na jukumu kubwa sana katika nchi hii kuhusu haki za wanawake. Wanawake wengi Tanzania wanaonewa sana kijinsia na waajiri wao ama kabla ya kupewa kazi au baada ya kupewa kazi. Ingawa mama Madawili hsiyo mwanasheria, ana jina kubwa sana ambalo angeweza kulitumia kwa kusaidiwa na wanasheria kuhakikisha kuwa anawake wote wa Tanzania wanapewa haki na heshima kama bionadamu wengine.
   
 2. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,770
  Likes Received: 2,505
  Trophy Points: 280
  edit thread yako! mbayaaaaaaaaaaaaa alafu aieleweki
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mimi naomba nitofautiane na wewe!
  Namheshimu sana pia Mama Zawadi Madawili!
  Kuwa na Mwanamke Mjeshi kwenye nafasi ya juu uraiani hakutafanya vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake vikome!
  Kitakachowaokoa wanawake ni Elimu tu!...unaelewa kwanini wanawake wengi wasomi hawaolewi(chunguza huko Botswana)?....the thing is just that they went to school and can take care of themselves without needing some flag-career pals!
  Kama ni misimamo wanayo akina Ananilea Nkya bana!...pamoja na kazi zao, do you see any significant difference though?
   
 4. bigcell

  bigcell JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45  naungana na wewe mkuu, elimu ndo tatizo.
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wapo wengi mkuu ila wamestaafu na wameachwa tu.............!!
  Mfano mwingine ni Maj. Gen Samwel Kitundu ........!!
  Huyu bado ni nguvu kazi katika nyanja za kibalozi.....!! na ana uzoefu kem kem...
  Alishaliwakilisha jeshi la Tanzania kama Muambata huko China kwa Miaka 7..............!!!
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Sure huyu mama General ana elimu gani? Au ni wale walipata vyeo zamani kwa kulenga shabaha na kuhudhuria Monduli? Kama hakufunguka akaingia darasani basi atabaki na cheo chake hicho kwa sasa!!! Angepewa say ubalozi atauweza? Maana itahitaji tena aajiriwe mkalimali kwa ajili yake (double cost). Kwa kweli sijamsikia kabisa mama mkubwa huyu, au tuseme wanaume wa vyeo kama chake wanamfunika? Anatakiwa afurukute pia si kubebwa tu!!! Mbebaji mwenyewe 2015 hatakuwepo tena.
   
Loading...