Mama ajiandae Unguja padogo.Akihojiwa na kipindi cha BBC kinachorushwa na television ya star TV tarehe 7 mwezi huu kuhusu mapinduzi ya Guinea, Jenerali Ulimwengu amesema yeye haoni ajabu Kwa yale yaliyotokea Guinea.
Na akatabiri pia kuwa hali hiyo ya kimapinduzi ya kijeshi itafika Kwa Kwa haraka sana ktk nchi zote zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Alipoulizwa kwanini anawaza hivyo alisema kuwa kilichokuwa kinafanywa na Alpha Conde ya ukandamizaji, dhurumati, kutokujali demokrasia, na uvunjifu wa haki za binadamu ,vitendo hivyo viovu vinafanywa pia na baadhi ya Serikali zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara na nchi zetu za Afrika Mashariki.
Jenerali aliendelea kushangaa kuona AU na ECOWAS wakilaani mapinduzi hayo huku wakiwa walishindwa kukemea matendo mabaya ya Rais Conde.
Alisema hali hiyo ya kimapinduzi ya kijeshi hayana muda mrefu itafika ktk nchi zetu wakati wowote kuanzia sasa.
Jenerali Ulimwengu ambae kwasasa ni mtu mzima na mwenye busara ni mtu asiyependa unafiki na hupenda kusema ukweli na maneno yake mara nyingi hutimia kama anavyotabiri.