Jenerali Ulimwengu ni mmoja wa viongozi wa gazeti la RAIA Tanzania? mbona halimfananiye?

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Moja kati ya vitambulisho vikubwa vya jenerali ulimwengu ni fikra zake,misimamo yake,usomi wake,umakini wake,kukaa mbali na wapuuzi na upuuzi,kutoshabikia ujinga.

Misimamo hii ilimpa misukosuko mpaka akafikia hatua ya kunyanganywa uraia wake. Kipindi chake cha "jenerali on Monday" kilikuwa na umaarufu sana nafikiri kikifuatia kipindi cha hotuba ya mwezi ya rais mkapa.

Raia Tanzania kwa habari zangu finyu ni mali ya jenerali,lakini kinachoandikwa na gazeti hilo hakifanani na jenerali ulimwengu.wakati mwingine huwa nalisoma najiuliza,hivi hizi habari mzee ulimwengu na yeye alizipitia akazipitisha? Habari zinazofaa kuandikwa na gazeti la uwazi,kiu na ijumaa wikenda?

Labda mzee kaona ni upuuzi kuwasemea watanzania wasiojielewa naye kaamua kufanya biashara ya habari,masuala ya jenerali on Monday kayatupa kule?

Hakika gazeti la raia Tanzania linashusha hadhi ya mzee wetu.
..bodi ya uhariri ya gazeti hili inabidi pia ihaririwe
 
Usishangae hayo si kuna Uhuru,Tanzania daima,Mtanzania,Mwananchi,bila kusahau jambo leo yote hayo wahariri wana kadi za vyama wavipendavyo na wanatekeleza matakwa ya mabosi wenye kampuni zao
 
Nimeongelea RAIA Tanzania ,naona kama wanamdhalilisha huyu mzee kabisa bila aibu
 
Moja kati ya vitambulisho vikubwa vya jenerali ulimwengu ni fikra zake,misimamo yake,usomi wake,umakini wake,kukaa mbali na wapuuzi na upuuzi,kutoshabikia ujinga.

Misimamo hii ilimpa misukosuko mpaka akafikia hatua ya kunyanganywa uraia wake. Kipindi chake cha "jenerali on Monday" kilikuwa na umaarufu sana nafikiri kikifuatia kipindi cha hotuba ya mwezi ya rais mkapa.

Raia Tanzania kwa habari zangu finyu ni mali ya jenerali,lakini kinachoandikwa na gazeti hilo hakifanani na jenerali ulimwengu.wakati mwingine huwa nalisoma najiuliza,hivi hizi habari mzee ulimwengu na yeye alizipitia akazipitisha? Habari zinazofaa kuandikwa na gazeti la uwazi,kiu na ijumaa wikenda?

Labda mzee kaona ni upuuzi kuwasemea watanzania wasiojielewa naye kaamua kufanya biashara ya habari,masuala ya jenerali on Monday kayatupa kule?

Hakika gazeti la raia Tanzania linashusha hadhi ya mzee wetu.
..bodi ya uhariri ya gazeti hili inabidi pia ihaririwe
Acha ubazazi wewe, mliishi kwa kulishwa habari za uongo naona zilishakuwa tamu hamtaki kuziacha. Safari hii kila anayeleta habari za uongo zenye kuleta machafuko au kuvuruga amani yetu LAZIMA ASHUGHULIKIWE KINAGAUBAGA!! Gharama ya Amani ni kubwa sana, ni bora kuondoa wasaliti wachache ili nchi iendelee kuwa na neema!
 
Raia mwema ni gazeti ambalo limejaa habari za utafiti, huwa wanatambua umuhimu wa kuwapa nafasi wanazuoni. Siku unaweza kulinunua ukakutana na hoja za Prof Shivji na wasomi wa kiwango chake.
Ni gazeti ambalo linatambua nguvu za hoja walizonazo watu walioelimika. Tofauri kabisa na mwanahalisi na udaku mwingine, magazeti ambayo hayana habari za kichunguzi, magazeti yenye kuendeshwa kwa kutegema kashfa za watu, yaani kusipokuwa na kashfa yanadoda kwenye meza za wauza magazeti.
 
Raia Mwema ndiko aliko Jenerali Ulimwengu. Raia Tanzania lilianzishwa maalum ili kujaribu kufuta nyayo za Jenerali na Gazeti la Raia Mwema.
Sio kweli; Raia Mwema na Raia Tanzania ni magazeti yanayomilikiwa na kampuni moja ambayo Jenerali Ulimwengu ni mmoja wa wakurugenzi na ndiye mwenyekiti wa bodi. Mimi pia huwa natilia mashaka weledi wa wahariri hasa katika gazeti la Raia Tanzania. Kuna wakati zinaandikwa habari za ajabu ajabu ambazo kwa kweli hazifanani na hadhi ya Jenerali Ulimwengu!
 
Raia mwema ni gazeti ambalo limejaa habari za utafiti, huwa wanatambua umuhimu wa kuwapa nafasi wanazuoni. Siku unaweza kulinunua ukakutana na hoja za Prof Shivji na wasomi wa kiwango chake.
Ni gazeti ambalo linatambua nguvu za hoja walizonazo watu walioelimika. Tofauri kabisa na mwanahalisi na udaku mwingine, magazeti ambayo hayana habari za kichunguzi, magazeti yenye kuendeshwa kwa kutegema kashfa za watu, yaani kusipokuwa na kashfa yanadoda kwenye meza za wauza magazeti.
Kuliko UHURU na MZALENDO?
 
Acha ubazazi wewe, mliishi kwa kulishwa habari za uongo naona zilishakuwa tamu hamtaki kuziacha. Safari hii kila anayeleta habari za uongo zenye kuleta machafuko au kuvuruga amani yetu LAZIMA ASHUGHULIKIWE KINAGAUBAGA!! Gharama ya Amani ni kubwa sana, ni bora kuondoa wasaliti wachache ili nchi iendelee kuwa na neema!
Ushawapikia chai wanene wa lumumba?
 
Kuliko UHURU na MZALENDO?
Hayo uliyotaja ni magazeti kongwe lakini katika issue ya nguvu ya hoja Raia Mwema wako vizuri sana. Siku zote wanapenda kufanya kazi kwa kutegemea investigative journalism, tofauti na magazeti mengi ambayo yamejaa waandishi makanjanja kama MWANAHABARI HURU na wengine wa aina yake.
 
Hayo uliyotaja ni magazeti kongwe lakini katika issue ya nguvu ya hoja Raia Mwema wako vizuri sana. Siku zote wanapenda kufanya kazi kwa kutegemea investigative journalism, tofauti na magazeti mengi ambayo yamejaa waandishi makanjanja kama MWANAHABARI na wengine wa aina yake.
Naona wewe hutaki kupata udc
 
Raia mwema ni gazeti ambalo limejaa habari za utafiti, huwa wanatambua umuhimu wa kuwapa nafasi wanazuoni. Siku unaweza kulinunua ukakutana na hoja za Prof Shivji na wasomi wa kiwango chake.
Ni gazeti ambalo linatambua nguvu za hoja walizonazo watu walioelimika. Tofauri kabisa na mwanahalisi na udaku mwingine, magazeti ambayo hayana habari za kichunguzi, magazeti yenye kuendeshwa kwa kutegema kashfa za watu, yaani kusipokuwa na kashfa yanadoda kwenye meza za wauza magazeti.
Mleta hoja anazungumzia Raia Tanzania, sio Raia Mwema wala Mwanahalisi!
 
Sio kweli; Raia Mwema na Raia Tanzania ni magazeti yanayomilikiwa na kampuni moja ambayo Jenerali Ulimwengu ni mmoja wa wakurugenzi na ndiye mwenyekiti wa bodi. Mimi pia huwa natilia mashaka weledi wa wahariri hasa katika gazeti la Raia Tanzania. Kuna wakati zinaandikwa habari za ajabu ajabu ambazo kwa kweli hazifanani na hadhi ya Jenerali Ulimwengu!
Umeona eeh! wakati mwingine unaweza kuhisi umeuziwa gazeti feki
 
Mleta mada, Raia Tanzania lilishauzwa halipo kwenye himaya ya Jenerali Ulimwengu. Rai Tanzania lipo chini ya kampuni ya TSN ile ya mafuta na ofisi zake zipo pale Bamaga kwenye kituo cha mafuta kuna jengo la gorofa moja. Raia Mwema ndio lipo chini ya himaya ya Ulimwengu na Johnson Mwambo na ofisi zao zipo Kinondoni karibu na Bar ya MK. Usichanganye.
 
Raia mwema ni gazeti ambalo limejaa habari za utafiti, huwa wanatambua umuhimu wa kuwapa nafasi wanazuoni. Siku unaweza kulinunua ukakutana na hoja za Prof Shivji na wasomi wa kiwango chake.
Ni gazeti ambalo linatambua nguvu za hoja walizonazo watu walioelimika. Tofauri kabisa na mwanahalisi na udaku mwingine, magazeti ambayo hayana habari za kichunguzi, magazeti yenye kuendeshwa kwa kutegema kashfa za watu, yaani kusipokuwa na kashfa yanadoda kwenye meza za wauza magazeti.

uko sahihi kabisa...na kuna kipeperushi kimoja kinaitwa UHURU...sidhani kama huwa wanauza hata kopi tano kwa siku
 
Back
Top Bottom