Jenerali Ulimwengu: Mtanzania anamkagua vizuri zaidi mbuzi wa kuchinjwa kesho kuliko anavyomkagua kiongozi atakayemtumikia kwa miaka 5

Mr DC failure katika ubora wake.
Watu wengine wanapenda sana kupiga porojo wakati kazi halisi ziliwashinda.
 
Anachojaribu kusema Ulimwengu ni kuwa kwa Tanzania mbuzi ana thamani kuliko mwanasiasa.Lakini hiyo ni kwa dunia nzima vyakula vina thamani kuliko wanasiassa ndio maana kila nchi ziko mamlaka kibao za kusimamia ubora wa vyakula na uthibitisho wa ubora Kama TFDA,TBS nk kabla kuingia sokoni lakini hakuna mamlaka ya kusimamia ubora na viwango vya mwanasiasa popote duniani kuwa kabla kugombea kuwe na TBS au TFDA au ISO ya kuthibitisha ubora wake .Ndio maana hata migaidi inaingia kugombea baadaye inafunguliwa kesi

Atuombe samahani watanzania kote duniani ni hivyo
"...kwa dunia nzima vyakula vina thamani kuliko wanasiasa..." Na hapo ndo tulipofika!
Umesahau hayo maTFDA yanawekwa na nani, anayatumiaje, kwa manufaa ya nani ...nk. Alichozungumzia Ulimwengu ni kuwa, pamoja na umuhimu wa hayo maTBS, bado anayeyasimamia ni mwanasiasa na kuna uwezekano akayateua, yakatumika vibaya, watu wakaathirika kutokana na matumizi mabaya ya madaraka.
Hivyo kinacho zungumziwa ni zaidi ya maTBS, ni pamoja na ubora wa katiba... au hilo pia ni gumu?! Na kama TFDA inasimamia ubora wa chakula, basi kubali pia mchakato wa wanasiasa unahitajika kupitia chombo fulani...(au?)
Mapambio yanapozidi yanaleta athari hasi kwa walengwa, wanapoteza umakini...nk, ya kisiasa yanapozidi sana, yanatafsiriwa kuwa ni kujikomba-kwa lugha yoyote ile, laini au kali
 
Back
Top Bottom