Ki Mun
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 3,443
- 4,386
Katika Makala yake ya "Rai ya Jenerali Ulimwengu" katika Gazeti la Raia Mwema la tarehe 27/4/2016 Jenerali Ulimwengu anatahadharisha juu ya mantiki na busara inayotumiwa na watawala wa CCM kuanzisha Mahakama ya Mafisadi,na anaandika hivi:
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Nimemsikia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitangaza rasmi kuanzishwa kwa “mahakama ya mafisadi.” Naelewa kwamba huo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Magufuli, lengo lake likiwa ni kujaribu kuharakisha kesi dhidi ya watu wanaodhaniwa na kutuhumiwa kuwa “Mafisadi”.
Sina budi kusema mwanzoni kabisa, kabla mahakama hii haijazinduliwa kwamba ninaipinga hatua hii kwa sababu ni hatua yenye hatari kubwa kwa mustakabali wa nchi yetu. Mahakama kama hizi zinaweza kutumika kuwakomoa watu wasio na hatia kwa sababu tu kuna mahali wamewaudhi wakuu wenye uwezo wa kuwaumiza. Kwa maana nyingine mahakama hii inaweza kugeuzwa kuwa “kangaroo court” ambayo kazi yake itakuwa ni kutafuta wachawi na kuwapeleka “mchakamchaka” hadi jela bila kujali umadhubuti wa mashitaka dhidi yao.
Tukianza na “mahakama ya mafisadi” ambayo ni mahakama ya makosa ya jinai, ni kwa nini tusianzishe mahakama nyingine kwa ajili ya makosa mengine ya jinai??? Kwa mfano mahakama mahsusi kwa makosa ya ubakaji, unajisi, usafirishaji haramu wa binadamu, ugaidi, dawa za kulevya, na kadhalika?
Utawala wetu leo unauona ufisadi kama ndilo kosa kubwa kuliko yote kiasi cha kutaka kuuundia mahakama. Sawa. Lakini miaka michache ijayo, mathalan, tukikuta kwamba tunakabiliwa na janga kubwa la ugaidi, tutaanzisha mahakama ya ugaidi? Na baadaye, nyingine ya mihadarati, na kadhalika?
*See more at: Raia Mwema - Tufanye hadhari na mahakama ya mafisadi