Jenerali Ulimwengu kanena: Huwezi kujadili katiba mpya bila kuujadili muungana

Nguli wa tasnia ya habari nchini tanzania ama hakika amenena vema juu ya mustakabali wa nchi yetu na katiba mpya! Watanzania tuungane wote na mawazo haya jengefu ya ulimwengu.
 
Wakati mataifa makubwa ya ulaya wana fanya juhudi ili muungano wao wa EU uweze kushamiri na huku sisi waafrica tuna fikiria kubomoa hiyo miungano iliyopo. Je tutafika.......?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa ni kikwazo cha maendeleo hata ya EAU. Yatupasa tusahau tofauti zetu na tutafute mbinu ya kuudumisha huu muungano ajili ya maedeleo na usalama wa taifa letu.

Utakapo vunjika faida itakuwa kwa mabeberu na hasara itakuwa kwa watanzania.

Ni juu ya viongozi kukubaliana na wananchi juu ya aina ya muungano utakao tuwezesha kukabiliana na mafisadi.

Walio wengi (mimi mmoja wao) hatukatai muungano tunataka nafasi ya kuujadili na hasa muundo wake. Kwa kweli wenye nia nzuri hawatoi maoni kama yako
 
wanaotaka Muungano ujadiliwe na katiba are myopic, mamlaka ya rais yatajadiliwa vipi? Makamu? Muundo wa mahakama? Mfumo wa sarafu? Think hard
 
Wakati mataifa makubwa ya ulaya wana fanya juhudi ili muungano wao wa EU uweze kushamiri na huku sisi waafrica tuna fikiria kubomoa hiyo miungano iliyopo. Je tutafika.......?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa ni kikwazo cha maendeleo hata ya EAU. Yatupasa tusahau tofauti zetu na tutafute mbinu ya kuudumisha huu muungano ajili ya maedeleo na usalama wa taifa letu.

Utakapo vunjika faida itakuwa kwa mabeberu na hasara itakuwa kwa watanzania.

Ni juu ya viongozi kukubaliana na wananchi juu ya aina ya muungano utakao tuwezesha kukabiliana na mafisadi.

Hivi bara na visiwani wapi kuna mafisadi zaidi na ni kwa nini?
 
kati ya kero wananchi wanazihitaji kujadili ni pampoja na muundo wa muungano,madaraka ya raisi na uwajibikaji
 
Wakati mataifa makubwa ya ulaya wana fanya juhudi ili muungano wao wa EU uweze kushamiri na huku sisi waafrica tuna fikiria kubomoa hiyo miungano iliyopo. Je tutafika.......?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa ni kikwazo cha maendeleo hata ya EAU. Yatupasa tusahau tofauti zetu na tutafute mbinu ya kuudumisha huu muungano ajili ya maedeleo na usalama wa taifa letu.

Utakapo vunjika faida itakuwa kwa mabeberu na hasara itakuwa kwa watanzania.

Ni juu ya viongozi kukubaliana na wananchi juu ya aina ya muungano utakao tuwezesha kukabiliana na mafisadi.

Tuiache Zanzibar iende kwa amani

Innocent Nganyagwa
Wasiliana na Mwandishi

+255 752 227 594

Tuma barua-pepe

NASHINDWA kuelewa ni kwa nini wahusika wamekuwa wakiilazimisha Zanzibar iendelee kubakia katika Muungano uliozaa Tanzania wakati wenyewe wameonyesha kuwa hawaridhiki na jinsi Muungano huo ulivyo.
Kwa wahusika hapa namaanisha Serikali ya Muungano pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwa upande mmoja, serikali ya Muungano ndio mlezi mkuu wa Muungano huu na CCM ndicho chama pekee ambacho kimeonyesha kuutaka Muungano kwa sura yake ya sasa ya serikali mbili, ambayo nayo imekuwa ni chanzo cha malalamiko kutoka Zanzibar.
Zanzibar wanazo sababu nyingi tu za kuonyesha kutoridhishwa na Muungano jinsi ulivyo ambazo wao wanaamini kuwa ni za msingi. Wahusika wanaweza wasizione sababu hizo kuwa za msingi lakini hilo nalo halizuii Zanzibar kujiondoa katika Muungano.
Kimsingi, Zanzibar in mbia katika Muungano huo na kwa maana hiyo ina haki ya kuamua kuendelea kuwapo ndani ya Muungano au kujitoa.
Hata kama sababu za kutaka kujitoa hazitaonekana kuwa za msingi sana kwa upande wa pili, lakini hiyo haiondoi haki yao ya kutaka kujitoa kwenye Muungano pale wanapoamini kuwa Muungano huo hauwanufaishi tena.
Inashangaza kuwa kwa miaka sasa Zanzibar imekuwa ikipaza sauti kuwa hairidhiki na jinsi Muungano unavyoendeshwa. Lakini, wahusika walichokifanya, na ambacho wamekuwa wakiendelea kusisitiza kukifanya, ni kiini macho walichokipa jina la kutatua kero za Muungano.
Kinachowafanya waonekane kuwa ni majuha ni kuwa kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakiendelea na kiini macho hicho cha kutatua kero za Muungano lakini badala ya kwisha, kero zimekuwa zikiongezeka.
Ajabu ni kuwa wanaonekana kuwa hawaoni kuwa kero zinaongezeka badala ya kupungua licha ya juhudi zao za kushughulikia kero za Muungano.
Kwangu mimi, ilichokifanya Zanzibar mpaka hivi sasa ni njia za kuonyesha kistaarabu kuwa hairidhishwi na Muungano kwa sababu Wazanzibari wanaamini kuwa hauzingatii masilahi ya Zanzibar. Na walichokifanya wahusika ni kutumia nguvu kuwanyima Wazanzibari haki yao ya kujiamulia mambo yao.
Walianza kudai kwa maneno tu, wakaonekana hawana hoja, wakakataliwa. Kwa kuwa walidhamiria kuendelea kudai kile wanachoamini kuwa ni haki yao, wakaanza kufanya baadhi ya vitu kwa vitendo.
Wakabadilisha sheria kadhaa ambazo kimsingi zinakiuka kabisa makubaliano ya Muungano kama ilivyopo sasa. Walipoona upande wa pili haujashtuka, wakaamua kubadili na Katiba kabisa. Lakini, inaonekana bado wahusika hawaelewi hawa jamaa wanataka nini.
Kitakachotokea sasa, sidhani kama ni kosa la Wazanzibari kwa sababu kama ni onyo walishalitoa na wakadharauliwa.
Upo msemo kuwa paka akibanwa kwenye kona, anaweza kugeuka kuwa chui. Hilo ndilo litakalotokea kwa Zanzibar. Kwa sababu imebanwa sana katika azima yake ya kutaka Muungano ambao una masilahi kwake, sasa itageuka kuwa mbogo kweli kweli. Na dalalili zimeanza kuonekana.
Zipo chockochoko za chini kwa chini ambazo zinawahusisha watu wa kawaida tu hivi sasa. Wapo watu wenye asili ya Tanzania Bara huko Zanzibar ambao wameanza kunyanyaswa na watu wa kawaida tu wa Zanzibar.
Kwa maelezo yanayotolewa, inaonyesha kuwa hilo ni suala la uhalifu wa kawaida tu ambao hata Tanzania bara upo, ingawa haulekezwi kwa Wazanzibari.
Lakini kwa wanaotaka kukiita kitu kwa jina lake halisi wanaelewa fika kuwa chokochoko hizi zina uhusiano ya kutoridhishwa kwa Zanzibari katika masuala ya Muungano. Wahusika hawataki kulikubali hilo lakini hiyo haibadilishi ukweli wa suala hilo.
Kwa kuwa tumeamua kuficha maradhi, tusubiri kifo kituumbue. Naamini kuwa Zanzibar haitachoka wala kuacha kudai haki zake ndani ya Muungano. Na kwa jinsi mambo yalivyo, wahusika wataendelea kukataa kutekeleza matakwa hayo.
Kwa kuwa suala hili limeshafika kwenye ngazi ya wananchi, ambao wameamka baada ya kuona kuna viongozi wao wengi tu ambao wana mawazo kama yao, tusitarajie kuwa litakwisha hivi hivi.
Nadhani wahusika wana hofu ya kuvunjika kwa muungano. Lakini wafahamu kuwa kuvunjika huko kwa Muungano kunaweza kuwa ndio suluhisho la kujenga Muungano mwingine utakaokuwa imara kwa sababu utajengwa chini ya maridhiano ya pande mbili zikikubaliana kuungana.
Lakini, kuna uwezekano mwingine kuwa ni kweli Zanzibar inabanwa sana kiuchumi ndani ya muungano na hivyo kuvunjika kwa Muungano kunaweza kuisaidia ikajitanua. Itaisaidia pia Tanganyika iwapo itakuwa na jirani tajiri.
Kuendelea kulazimisha Muungano huu kutatuletea maafa hapo baadaye. Imeshajidhihirisha kuwa Wazanzibari hawataacha kudai haki zao mpaka wazipate.
Na itafika wakati Watanganyika nao watakapochoka na chokochoko hizo na wao kuamua kuanza kudai haki zao kwa hila na kwa nguvu. Sijui kama wahusika watakuwa na nguvu za kutosha kukabiliana na Watanganyika na Wazanzibari watakapoamua kudai haki zao kila mmoja kivyake.
Kuna nafasi adhimu ambayo viongozi wetu wanataka kutukosesha bila sababu za msingi. Kwa mtu anayepima upepo, atagundua kuwa watu wengi hawaridhishwi na aina ya Muungano uliopo. Na kwa hakika kabisa, miongoni mwa watu hao ni viongozi wetu wengi tu.
Tatizo ni kuwa waliopo madarakani hawataki kuingia kwenye vitabu vya historia kuwa ndio walioshiriki kuua Muungano. Wana hofu kuwa Zanzibar ikiruhusiwa kutoka basi Muungano utakuwa umekufa. Ile fursa kuwa kuondoka kwa Zanzibar ni mwanzo mzuri wa kuunda Muungano imara wala hawajaiona.
Wamejawa hofu ya kihistoria iliyopatia upofu wa masuala dhahiri kuwa kwa kulazimisha Muungano, eti tu kwa sababu ulianzishwa na waasisi wa taifa, watakuwa wanadumisha utaifa. Lakini kama wakiamua kufungua macho, watabaini kuwa wanachokifanya kinaua utaifa.
Kama nilivyoeleza awali, Zanzibar haiwezi kuendelea kuvumilia kulazimishwa kuwepo ndani ya Muungano. Itafika mahali itageuka mbogo na kulazimisha kile inachokitaka. Itakuwa vigumu sana kuzuia na kudhibiti hali ya mambo wakati huo.
Kama tunataka salama, ni heri tukaiacha Zanzibar iondoke kwenye Muungano sasa hivi kwa amani na utulivu, nasi tutabaki salama huku tukiwa na uwezekano wa kuunda muungano mwingine wenye nguvu zaidi.
Lakini iwapo tutasubiri mpaka Zanzibar, au hata Tanganyika, ikaamua kujiondoa kwa nguvu, hatutabaki salama na wala hakutakuwa na uaminifu uliobakia wa kuwa msingi wa kuunda muungano mwingine wenye nguvu.


By (InnocentNganyagwa) mtafiti wamaswala ya sanaa
 
Kweli wahenga walisema Wakati ukuta, hata jenerali ulimwengu anahoji uhalali wa muungano. Hata huko aliko mwalimu Nyerere atakuwa anajisikia vibaya kwamba hata jenerali aliemwamini sasa anataka muungano uvunjike. Rais hajazuia Watu kujadili mfumo wa muungano, alichosema hakuteua tume ya kuvunja muungano. Wanaolalama ni wale waliotaka kutumia mjadala wa katiba kuvunja muungano. Tunacho jadili ni katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, sasa tukivunja muungano, tuna jadili katiba ya nchi inaitwa nini? Jambo la kwanza katika katiba ni kutamka jina la nchi na mipaka yake kisha misingi na kuendelea. Sasa. Tuvunje nchi kisha tujadiliane kuhusu katiba ya nchi gani?
 
Zanzibar ni jimbo la Tanzania.Kwa hiyo kutaka kujitenga ni sawa na kutangaza vita.
Ila kama wanaweza vita, basi wataachiwa ili iwe nchi inayojitegemea.
Kwa hiyo japo sipendi muungano, sishangai serikali ya JMT kukataa kujadili muungano. It's normal.
 
Huu muungano ni kama kiini macho. Wanaofaidika na huu muungano ni viongozi wa ccm, na ndiyo maana hawataki ujadiriwe. Mimi maoni yangu,ingeundwa serikali moja. Serikali tatu ni mzigo tu kwa walipakodi na ni matumizi ya siyo na tija. Mf kutakua na waziri wa serikali ya Tanganyika,
waziri wa Muungano na bado east-africa. Kama serikali moja haiwezekani bora muungo uvunjike. Maana zaidi unawanufaisha viongozi wa kisiasa. Swala la muungano halikwepeke lazima lijadiriwe kwa uwazi ili wananchi watoe maoni ni muundo upi wa muungano wanaoutaka. Maana mwananchi wa miaka ya 60 tofauti na huyu wa sasa.
 
Mi nazani wakati wa kutoa maoni ndo mahala sahihi kwa kujadili muungano kwamba uweje ( kama twautaka ) au kuuvunja kama hatuutaki

Muungano hauvunjiki na wazanzibari hawatoki ngó kwenye muungano huu. Muungano wetu una njia moja tu ya kuingia hakuna kutoka. Sasa hivi tunaelekea kwenye serikali moja Zanzibar na Pemba intakuwa majimbo tu yakiongozwa na Magovernors. Kwa hiyo mnafikiria Zanzibar kujitenga ni ndoto za mchana tu hizo.
 
Muungano umo kwenye katiba hivyo ni muhimu kujadili katiba in its totallity. Kama hujadili muungano ina maana itakuwa ni kuweka viraka kwenye katiba kwa kuwa Ibara inayohusu muingano haitaguswa.

daah generali kimbunga umesahau kwamba hii pia ni ishu ya muungano na ulikana kabisa kuendelea kuzungumzia sula hili ingawa ni la msingi sana? Ni sula ambalo kwa namna yoyote ile si rahisi kuliweka kando katika mjadala wa kitaifa na hasa kwa wale waipendao Tanganyika yetu.
 
Kweli wahenga walisema Wakati ukuta, hata jenerali ulimwengu anahoji uhalali wa muungano. Hata huko aliko mwalimu Nyerere atakuwa anajisikia vibaya kwamba hata jenerali aliemwamini sasa anataka muungano uvunjike. Rais hajazuia Watu kujadili mfumo wa muungano, alichosema hakuteua tume ya kuvunja muungano. Wanaolalama ni wale waliotaka kutumia mjadala wa katiba kuvunja muungano. Tunacho jadili ni katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, sasa tukivunja muungano, tuna jadili katiba ya nchi inaitwa nini? Jambo la kwanza katika katiba ni kutamka jina la nchi na mipaka yake kisha misingi na kuendelea. Sasa. Tuvunje nchi kisha tujadiliane kuhusu katiba ya nchi gani?

Nadhani hata jina la nchiyetu tunalikosea miaka yote tangu tuungane. Nchi hii ilipaswa kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Si Jamhuri ya Muungano wa Tazania (nilishawahi kutoa thread inayohusu jina la nchi yetu) na katiba ilipaswa itambue hilo
 
Wengi tulishasema sana juu ya hili hapa:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...elewe-kwenye-maoni-ya-katiba.html#post3700947

Wala haiitaji mtu kuwa na elimu hata ya sekondari kuona umuhimu wa kujadili Muungano maana hii ni katiba ya Jamhuri ya Muungano ambao kwa 'bahati mbaya' unalalamikiwa sana hususani na wenzetu wa Zenj, nilisema.

"Tume mjiandae kutuweka ndani wengi maana tunasema waziwazi kuwa kwanza tunaomba kura ya maoni juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa Muungano na uwe wa aina gani kama tunaukubali. Sitaki tena na tena kutukanwa in the name of preserving our Union in which our partner has systematically decided to defile consistently in public.

SALA KATIKA WILAYA ZOTE ZA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Ehe Mungu nawaheshimu waasisi wa Muungano wetu , sikia kilio chetu na utoe funzo kwa watu wanaoamua kutukana sehemu moja ya Muungano bila sababu.

Fungua macho na mioyo ya Wakuu wetu wa sasa waone umuhimu wa kuwa wazi na kuwapa fursa Wananchi kujadili na kuamua mustakabali wa Muungano wao katika karne hii kama wote tunaridhia kuendelea.

Vinginevyo mapenzi yako yatimie na kila nchi ibaki kivyake tushiriane tu vizuri kama majirani wema wa historia na ndugu tuliozaliana wana hadi vitukuu kama Kenya, Uganda, Burundi n.k

Fisha na legeza nguvu zote za Dora zitakazo jaribu kumtesa yeyote anayetaka kutoa maoni yake juu ya Muungano kwenye Tume ya Marekebisho ya Katiba".:amen:
 
Katika hicho kipindi cha majadiliano Ulimwengu kaizungumzia EU kwa mtizamo na wa kwako ambao nami naafiki ni sahihi: kwamba katika EU kila nchi imebaki na identity yake na mamlaka yake isipokuwa kuna mambo ambayo wamekubaliana kushirikiana kimkataba. Akaendelea kusema Zanzibar inapokuwa na malalamiko yanayohusu muungano haina mwenza wa kumlalamikia maana Tanganyika waliyoungana nayo haipo. Haina mantiki kwa Za nzibar kuilalamikia serikali ya muungano maana si patner wake kwani Zanzibar ni sehemu ya serikali ya muungano.

......Hiyo point imenigusa hadi kwenye uvungu wa moyo wangu. There are only two options - Aidha tuunde serikali tatu au tuwe na serikali moja.
 
hawa wakubwa mbona wanakuwa waoga linapokuja suala la muungano? ipo haja ya suala hilo kujadiliwa na wananchi wote
 
Muungano hauko katika katiba ila katiba ni ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndiyo nchi inayohitaji katiba mpya. Hivyo watanzania wanataka nchi Yao JMT itawaliwe namna gani. Hoja hapa syo uvunje nchi kwanza kisha uanze kujadili katiba. Tunachohitaji ni katiba mpya siyo nchi mpya.
 
Nimekutana na hii - Kesho, Jumatano, Mei 2, 2012 kuanzia saa 3:00 asubuhi kutakuwa na hafla fupi ya kuikabidhi na kuitambulisha ofisi ya Tume ya Katiba inayoongozwa Joseph Warioba tayari kwa kuanza kazi. Hafla hii itafanyika katika Ofisi za Tume zilizopo katika Jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, mtaa wa Ohio, mkabala na Makao Makuu ya sasa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kwa kifupi, majengo haya yanafuatana, unaanza na la sasa ukitokea PPF Tower kuelekea Barclays Bank. Katibu Mkuu Kiongozi atamkabidhi Jaji Warioba ofisi hizo tayari kwa kuanza kazi. Mialiko imesambazwa kwa vyombo vya habari. Kazi imeanza.
 
Hilo ni lazima lifanyike,ili kupata ridhaa ya wananchi.mimi binafsi muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar siutaki napendekeza uvunjike kero sio kero tena sasa ni mateso ya muungano
 
Back
Top Bottom