Hivi mtu akikufanyia vitu vya hovyo halafu ukamkenulia meno, mtu wa hovyo zaidi ni yupi??
Nadhani watanzania tunahitaji kuelewa hili!!
kwenye demokrasia watu wanapata serikali inayofanana nao. Watanzania wavivu, waoga wa maamuzi magumu, wanafiki (leo unamsema EL kesho ukimuona kanisani unakenua na kumsifia sana kwamba hamna mwingine kama yeye na unamtakia kila la heri katika mapambano yake ya Utawala wa juu). watanzania wanapenda mzaa na upuuzi kama alivyosema Jenerali hata kwenye kazi za muhimu, Watanzania wana chuki na maendeleo ya wenzao na hawapendi kushirikiana kwenye mambo ya maana ya kujenga maisha, kama wazairwaa tunapenda miziki yao, hulka zao, tunaiga majina yao kuitaana papaa nani sijui kwa sababu na sisi tukijiangalia kwenye kioo tunajiona hatuna tofauti nao sana.
Katika mazingira haya wezi wanashamiri na wanasifika na kuonekana ni mfano kwa jamii, wazalendo wanavunjika moyo na wenyewe wanakua wezi kwa sababu ya unafiki wetu, na viongozi tunaotengeneza wote wanakua wa sampuli hii.
Kitu kimoja tu Mungu alitupendelea ni kutupa Nyerere kama Rais wetu wa kwanza vinginevyo tungekua kwenye vita kama Kongo.