Jenerali Ulimwengu: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina zaidi ya wanachama milioni 8, lakini kina mawazo ya kufikiri yasiyozidi matatu

Askofu wa Chadema Benson Bagonza nae ana kiherehere sana, si agombee tu ubunge maana kaacha kutoa verses za dini sasa kazi yake ni siasa kila kukicha. Benson hajui yeye ni askofu, kachanganikiwa, sasa ni mwanasiasa wa Chadema. Anakesha kutunga sentensi na tungo tata za siasa against CCM tu.
Wewe kinakuuma nini? Si uende kwa Gwajima ukamuulize kwanza? Yaani akili zenu finyu kama za mjusi kafiri mnachowaza ni kupangia watu cha kupost humu.
 
Nahitaji watu wenye sifa zifuatazo;

1. Wazalendo
2. Wazalendo
3. Wazalendo
4. Wenye kutafuta suluhisho badala ya kulalamika
5. Walio tayari kuwekeza kwenye long time plans.

NB
Wajumbe watafanyiwa usaili kabla ya kupewa jukumu.

Komenti yako hapa au njoo DM.
 
MWANDISHI wa Habari Mkongwe, Jenerali Ulimwengu leo Septemba 21,2021 amezindua Kitabu chake RAI YA JENERALI jijini Mwanza na kuhudhuriwa na Askofu Benson Bagonza.

๐—›๐—”๐—ฌ๐—” ๐—ก๐—œ ๐—•๐—”๐—”๐——๐—›๐—œ ๐—ฌ๐—” ๐— ๐—”๐—ก๐—˜๐—ก๐—ข ๐—ฌ๐—”๐—ช๐—”๐—Ÿ๐—œ๐—ฌ๐—ข๐—ญ๐—จ๐—ก๐—š๐—จ๐— ๐—ญ๐—” ๐—ช๐—”๐—ž๐—”๐—ง๐—œ ๐—ช๐—” ๐—จ๐—ญ๐—œ๐—ก๐——๐—จ๐—ญ๐—œ ๐—›๐—จ๐—ข....

"Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina zaidi ya wanachama milioni 8, lakini kina mawazo ya kufikiri yasiyozidi matatu" - Jenerali Ulimwengu

"Hakuna uwezekano wa kizazi chetu kupata maendeleo na kupiga hatua ikiwa kitaendelelea kufundishwa kwa lugha wasioijua na pia wale wanaowafundisha nao hawaijui hiyo lugha"- Jenerali Ulimwengu

"Hakuna swali la kijinga ila majibu ndo ya kijinga"- Jenerali Ulimwengu

๐—”๐˜€๐—ธ๐—ผ๐—ณ๐˜‚ ๐—•๐—ฒ๐—ป๐˜€๐—ผ๐—ป ๐—•๐—ฎ๐—ด๐—ผ๐—ป๐˜‡๐—ฎ

"Mwalimu Nyerere aliwahi kusema marais wazuri waongoze kwa vipindi viwili ili waondoke na uzuri wao, lakini marais wabaya wao wataondolewa na wananchi" - Askofu Bagonza

"Tabia ya watu kusifia viongozi waliopo madarakani kufanywe kama kosa la jinai ili kupunguza watu kujipendekeza kwa viongozi kupata uongozi"- Askofu Bagonza

"Watanzania wanahitaji katiba yenye uwezo wa kuweka na kuwaondoa viongozi madarakani badala ilivyo kwa sasa" - Askofu Bagonza

"Muujiza wa elimu ya Tanzania kiongozi akichaguliwa leo akiwa hajui kitu, akishaingia madarakani kesho yake anakuwa anajua kila kitu"- Askofu Bagonza

"Tunaupungufu mkubwa katika Taifa letu la watu wenye Fikra na Uthubutu; Wapo wenye Uthubutu lakini hawana Fikra, kuna watu unawaona wana Fikra lakini hawana Uthubutu. Makundi haya yanahitaji daraja kuyaunganisha" - Askofu Bagonza

"Aslimia 60 ya wabunge wa CCM waliopo bungeni kwa sasa hawakushinda kura za maoni ndani ya chama chao, hata wanachama wao wanajua na wanaona kabisa hawakuwachagua na hivyo wanaona siyo wa wabunge wao"- Askofu Bagonza

"Bunge la sasa lina utata, kuna mabunge mawili (2), moja lipo mdomoni mwa watu na lingiine lipo mioyoni mwa watu," -Askofu Bagonza

Chanzo; Nipashe Mwanga Wa Jamii #NipasheHabari
Hawa wataishia kuwa wanafalsafa tuu
 
Miaka 6 chama kimeshindwa kuwapa nyongeza ya mishahara watumishi wa umma.Je kuna fikra tena hapo?
 
"Tunaupungufu mkubwa katika Taifa letu la watu wenye Fikra na Uthubutu; Wapo wenye Uthubutu lakini hawana Fikra, kuna watu unawaona wana Fikra lakini hawana Uthubutu. Makundi haya yanahitaji daraja kuyaunganisha" - Askofu Bagonza
 
Back
Top Bottom