chademaistheway
Senior Member
- Aug 18, 2010
- 100
- 86
NIMESEMA kwamba tunafanya makosa kama taifa na wala hakuna jambo la kushangaza katika kutenda makosa. Kila mtu hufanya makosa maishani mwake na kila taifa pia. Ni jambo la kawaida.
Jambo ambalo si la kawaida ni pale mtu mwenye akili timamu anapofanya kosa na asijue kwamba kafanya kosa, ama akafanya kosa na akajua kwamba kafanya kosa na kisha akajisahau na kuja kulifanya kosa lile lile.
Jamii zenye kujali uendelevu hujifunza kutokana na makosa ziliyoyatenda huko nyuma ili zisiyarudie. Jamii zisizojali uendelevu huishi kwa kuangalia kilicho mezani hii leo na zisijali kilichotendeka jana wala juzi. Hizi jamii za aina hii zinaweza zikawa zinarudia makosa yale yale siku hadi siku na mwaka hadi mwaka mpaka ikawa ndiyo hulka ya jamii hizo.
Ili kukumbuka ni mahali gani zilikosea katika historia yake, jamii za mapokeo (kabla ya maandiko) ziliweka simulizi, hadithi na ngano ili kuwajuvya vijana wake mambo yaliyotendeka zama za kale kama mafundisho kwa watoto na vijana. Siku hizi mambo kama hayo huwekwa ndani ya vitabu.
Laiti kama tungekuwa tukiandika mambo tunayoyafanya, mazuri na mabaya, tungekuwa tumejijengea hazina ya ujuzi katika mambo mengi. Kwa bahati mbaya hatuna hazina hiyo kwa sababu tunaishi siku hadi siku na hatuna kumbukumbu ya mambo tuyatendayo. Matokeo yake ni kuwa na watu kama ‘Balozi Mstaafu' ambaye kazi yake kuu ni kusema kwamba kila kitu kimekwenda sawa na hakuna cha kubadilisha, ambayo ni falsafa ya Profesa Pangloss wa Voltaire.
Katika mfululizo huu nimeandika kwamba tumewahi kufanya makosa ambayo yangetulazimu tujifunze kutokana nayo. Nimezungumzia jinsi tulivyoshindwa kabisa kuisoma vyema hali ya Angola mwaka 1964-65, na jinsi tulivyojikuta tukiwa kama vile tuko upande mmoja na Makaburu wa Afrika Kusini katika kukataa kuitambua serikali ya MPLA na Agustino Neto.
Nimeeleza ni jinsi gani Mwalimu Julius Nyerere alijaribu kuisahihisha hali hiyo hadi akawa mtetezi mkuu wa serikali hiyo. Lakini leo hii sidhani kwamba wanadiplomasia wetu, pamoja na ‘Balozi Mstaafu' wamesoma ni nini kilichotendeka mpaka tukawa na msimamo wa hovyo na ni jinsi gani Jonas Savimbi aliweza kuiingilia Serikali ya Nyerere kiasi hicho. Hatutaki kuangalia tulikotoka, na kwa jinsi hiyo hatupati mafunzo muhimu kutokana na historia yetu. Tunakuwa ni watu wa kuanza upya siku zote.
Hata hivyo ni kweli kwamba serikali ya Tanzania haikuwakilishwa na mjumbe hata mmoja katika sherehe ya Uhuru wa Angola mjini Luanda na hili halitafutika milele. Inaelekea ‘Balozi Mstaafu' halijui hili, na wala wenzake hawalijui, na wala hawataki kulijua.
Tulifanya makosa katika kuisoma Afrika Kusini na harakati zake za ukombozi. Tulishindwa kuiona African National Congress (ANC) kwamba ndiyo ngome kuu ya harakati hizo na tukajiruhusu kupumbazwa na hisia hafifu za watu waliokuwa hawana uwezo wa kuangalia mbali na pua zao. Leo hii Afrika Kusini ni nchi pekee, pamoja na Angola, ambako, miongoni mwa nchi za kusini zilizokombolewa miaka ya hivi karibuni, hakuna alama ya mtaa au jumba au kitongoji, linakoonekana jina la Tanzania au Nyerere. Hatujiulizi.
Natumai kwamba si ‘Balozi Mstaafu' aliyesaidia kuandika hotuba ya Mheshimiwa Rais wetu katika mazishi ya Nelson Mandela mwezi uliopita. Kwamba kiongozi wetu alikosea hata mwaka wa ujio wa Mandela nchini Tanganyika (siyo Tanzania) lilikuwa ni kosa muhimu. Lakini pia aliyeandika hotuba hiyo ya Rais alisahau kutaja sababu za Mandela kuja Tanganyika na msimamo wa Tanganyika wakati huo ndani ya Jumuiya ya Madola (Ama Afrika Kusini iondoke ama sisi, Tanganyika tutaondoka).
Inanikumbusha jinsi mwakilishi mmoja wa nchi yetu (hakuwa mtu wa serikali lakini aliiwakilisha nchi hii) alivyosemwa kwenye mazishi ya wapiganaji wa ANC miaka kadhaa ilyopita aliposema kwamba sasa ndiyo nafasi ya kuunganisha ubongo wa weupe na misuli ya weusi kuijenga nchi mpya! Hili nalo hatulikumbuki.
Tunazungumzia diplomasia ya kiuchumi, lakini binafsi sielewi hii ina maana gani wakati naona mabalozi wakiteuliwa kama shukrani kwa fadhila hii au ile. Najiuliza ni diplomasia gani watafanya watu wanaopewa zawadi kwa jambo hili au lile. Najiuliza pia iwapo kuna nchi inayoitwa ya Kiafrika ambayo tunayo maslahi nayo kama Algeria, ni kwa nini hatuna ubalozi nchini Algeria, nakosa jibu.
Hivi sasa, tunao makumi ya wanafunzi wa Tanzania wanasomeshwa bure, bure! nchini Algeria katika fani muhimu kama uganga, dawa, uhandisi wa gesi na mafuta. Lakini ubalozi wetu unaoshughulikia Algeria uko Paris! Hatuoni haya kuwawekea wananchi wa Algeria ubalozi wetu nchini Ufaransa. Mkoloni aliyewatawala na kuwatesa hadi kuua watu milioni moja unusu!
Source: Raia Mwema