Jenerali Ulimwengu aongezwa kwenye jopo la Mbowe

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
Wakili, na Mwanahabari mkongwe nchini Jenerali Ulimwengu ameongezwa kwenye jopo la mawakili wataomtetea Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kuongezeka kwa Ulimwengu kunafanya idadi ya mawakili kwenye kesi hiyo ya kikatiba namba 1/2017, kufikia 10.

Vyanzo vya kuaminika ndani ya CHADEMA vimethibitisha taarifa hiyo. Mawakili wengine kwenye jopo hilo ni Peter Kibatala, Tundu Lissu, John Mallya, Albert Msando, Jeremia Mutobesya, Omary Mseto, Faraji Mungula, Frederick Kihwelo, na Hekima Mwamsipu.
 
hawa mawakili wangekuwa wanadai tume huru ya uchaguzi tz ingekuwa Poa sana

Au wangefanya mobilization kutaka Ben Saanane apatikani inhekuwa poa sana. Masikini Ben, hata wale waliokuwa wanaandika 'we want our Ben Back' wameshtuka, wameacha kuwadai mabosi wao wamrudishe Ben
 
Matumizi mabovu ya pesa ya serikali inayotolewa kama ruzuku kwa hiki chama. Hiki chama kumekuwa ni gulio la madalali wa DEMOKRASIA nchini wafuasi wa fedha za wananchi.
 
Ulimwengu,kutokana na umaarufu wake ndani na nje ya nchi,atakuwa na kishindo kikubwa katika kesi hiyo
 
Hao wote ilitakiwa wawe mawakili wa serikali kesi za dowans sijui Tanesco tungeshinda hatuwatumii kisa wapinzani na huku tunaingia hasara...
Mawakili wa serikali kazi yao kubwa ni kupiga madili tu.

20170227_042445.jpg
 
Wakili, na Mwanahabari mkongwe nchini Jenerali Ulimwengu ameongezwa kwenye jopo la mawakili wataomtetea Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kuongezeka kwa Ulimwengu kunafanya idadi ya mawakili kwenye kesi hiyo ya kikatiba namba 1/2017, kufikia 10.

Vyanzo vya kuaminika ndani ya CHADEMA vimethibitisha taarifa hiyo. Mawakili wengine kwenye jopo hilo ni Peter Kibatala, Tundu Lissu, John Mallya, Albert Msando, Jeremia Mutobesya, Omary Mseto, Faraji Mungula, Frederick Kihwelo, na Hekima Mwamsipu.
thanks for the info. nieleweshe kidogo. wanamtetea kwenye kesi alioifungua yeye au katika kesi dhidi yake? na je kesi hiyo ni ngumu kiasi hicho au ni jinsi tu ya kuonyesha mshikamano?
 
thanks for the info. nieleweshe kidogo. wanamtetea kwenye kesi alioifungua yeye au katika kesi dhidi yake? na je kesi hiyo ni ngumu kiasi hicho au ni jinsi tu ya kuonyesha mshikamano?
Mbowe amefunguwa kesi ya kikatiba. Kama wewe ni mkristo ibada ikiongozwa na mapadre saba au kumi nadhani unajuwa inanogaje na haichoshi maana kila mmoja anashika kipande chake.

Kesi ya kikatiba si ndogo ndio maana Albert Bashite anarukaruka tu kama Bata Bukini.
 
Back
Top Bottom