Jenerali Ulimwengu amfananisha Pinda na mbwa wa PAVLOV

Ulimwengu amesema lkn tatizo la wana-magamba hilo itakuwa nongwa kwao coz hawasomi alama za nyakati! Kwa pinda ni ngumu kufanya miujiza ukizi ngatia kamfumo kaukiritimba waliojiwekea ccm hapa solution ni cdm watake wastake!!!!!
 
Hata kama hawaelewi, ukweli ni lazima waendelee kuambiwa. Ni ukweli usiopingika kuwa watawala wa nchi hii wamejigeuza miungu watu, wakiendelea kupuuza kila kelele ya kuwataka warudi kwenye mstari.
 
Kuvimbiwa kwa watawala: Jibu si kuvua gamba


Jenerali Ulimwengu
22 Jun 2011
Toleo na 191


Waswahili husema usiangalie ulipoangukia bali chunguza ni wapi ulipojikwaa, kwani anguko lako ni matokeo ya kujikwaa kwako, ambako usipoangalia unaweza ukakusahau ukiangalia tu pale ulipoangukia. Gharama mojawapo inayolipwa na mwangukaji asiyejua ni wapi alipojikwaa ni kuiona ardhi alipoangukia kama ndilo tatizo lake.
.........
Naamini kwamba zoezi hili lina umuhimu wake kama tunataka kuepukana na zahma za kutupiana lawama, na hata kuumizana, kwa sababu ama hatutaki, ama hatuwezi kufanya tafakuri ya masafa marefu, na hamasa zetu zisizo na mafunzo zinatutuma kutafuta majibu mepesi mepesi na majibizano yasiyosumbua akili.

Kwa kuwa mjadala huu hauna budi kuingia katika mijadala mipana inayoendelea kuhusu umuhimu wa kubadili kwa kina namna tunavyoendesha shughuli zetu za kitaifa, masuala kama vile ya Katiba mpya na mipangilio mipya ya kisiasa na kiutawala, bila shaka yataibuka mara kwa mara, na hivyo ndivyo ilivyo katika mjadala wo wote ambao unaangalia masuala kwa mtazamo kamilifu (holistic). Kwa jinsi hii tuanweza tukatambua mti mmoja mmoja na pia tukatambua msitu ambamo ndani yake ndimo inapatikana miti hiyo.
........
Uvuaji gamba

Leo hii ningependa nijiunge na wale wanaojadili suala la chama-tawala kufanya kila kilichopachikwa jina la ‘kuvua gamba’. Nisingependa kuingilia mijadala ya kishabiki na mabezo mengi yaliyotolewa katika vyombo vya habari kuhusu uteuzi wa nahau ya kuvua gamba(very good!),

Mimi nitakwenda katika dhana yenyewe ya kutaka kujisafisha kwa kuwaondoa katika nafasi za uongozi wanachama watatu,au watano, au 10, au 20, au 40, au hata 100. Nimekuwa nikifuatilia mijadala (nyingi zikiwa ni kelele) kuhusu ‘mapacha’ ambao wanatakiwa ‘watoswe’ ili ‘kukinusuru chama.’

Inaelekea mantiki iliyotumika ni kwamba hawa watu wamekipa chama-tawala jina baya machoni mwa Watanzania kwa sababu wao ndio wanaosemwa sana kwamba wanahusika na ufisadi, na kwa hiyo ikiwezekana ‘kuwatosa’ chama kitakuwa kimejitakasa mbele ya wananchi, nao wananchi wataanza kutuamini tena na kuturuhusu tuwaongoze.

Utaalamu wangu mdogo wa masuala ya kisiasa haunipi taswira ya chama ambacho kwa kuwaondoa watu watatu au wanne, au hata 100, kinakuwa kimejisafisha kwa kufanya hilo tu. Sijasikia chama hicho kikijadili au kupendekeza mapitio ya misingi ya kifalsafa na kiitikadi ndani ya chama hicho; mijadala ya programu za kisiasa; marejeo ya sera za chama kuhusu utekelezaji wa programu hizo za kisiasa; wala miundo yake itakuwa ipi ili kubeba programu hizo na kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika inavyopasa; wala maandalizi ya makada wenye uangavu wa msimamo unaowawezesha kutekeleza programu hizo.

Ninachosikia, na ambacho kinachosha kama walivyochoka wanaokiendeleza, ni ‘kuvua gamba’, ni kupambana hadi ‘tone la mwisho la damu’ na mambo mengine ambayo, kusema kweli, mimi nayaona ni ya kipuuzi. Hao ‘mapacha’ wana nguvu gani ndani ya chama ambayo wamejilimbikizia kwa kuipora bila wanachama na mifumo ya chama hicho kujua?

Ni lini hasa walipoanza kuwa na nguvu hii, na wenzao ndani ya chama walikuwa wanafanya nini wakati wote huo, na leo ndiyo wanatanabahi wakati ‘mapacha’ wamekwisha kukiteka chama kizima kiasi kwamba nusura ya chama ni kwa hao ‘mapacha’ kuondoka?

Msimamo wangu
Nieleze msimamo wangu kuhusu hao ‘mapacha’ maarufu. Kwanza sidhani miongoni mwao yupo hata mmoja ambaye anazo sifa za kuwa kiongozi mkuu wa Tanzania, kama tunaitakia mema nchi hii.

Niseme ukweli wangu: Naamini hadi sasa, na hili nitaliamini hadi kufa, kwamba, kwa jinsi nchi ilvyovurugika, tunahitaji Julius Nyerere mpya, ambaye nitamweleza baadaye, ambaye ataongoza mapambano ya ukombozi mpya wa nchi hii na wananchi wake.

Katika hao wanaotajwa hakuna mtu wa aina hiyo, na kwangu mimi ye yote mwenye njozi za aina hiyo angefanya vyema kutia tamati na afanye mambo mengine.
............
Lakini si lazima waondoke katika chama-tawala kwa ajili eti ya kukisafisha. Kwa kuwa kwa njia hiyo hakisafishiki. Badala ya chama-tawala kuuelewa msimamo wa Kambarage na kufanya marekebisho ndani yake kwa kunoa falsafa yake na kutakasa itikadi yake, kikazidi kujichimbia katika kila aina ya uovu na kukaribisha kila aina ya wanachama wasio na nasaba yo yote na chama hicho.
.........
Chama cha makabwela (Baba kabwela UNO- kumbuka) kikageuka, kikawa ni chama cha wenye ‘vijisenti.’
.........

Baadhi yetu tulifadhaika kuona chama kilichoanzishwa chini ya siasa ya utu na udugu wa binadamu wote kikigeuka kuwa chama cha manyang’au wasiojali watu bali wanajali vitu, chama kilichosimamia misingi ya haki kwa wote kikige
uka chombo cha utetezi wa wenye nguvu dhidi ya wanyonge.

Chama kilichonasibika Afrika na dunia nzima kuwa ngao ya kutetea nchi na mali zake kikibadilika na kuwa chama-na-serikali-dalali cha kuuza nchi na rasilimali zake kila kinapopata fursa ya kufanya hivyo.

Sasa, na aseme mtu kwamba haya yote wamefanya mapacha wetu maarufu, na wakiondoka ndani ya chama hicho, chama kitarejea misingi yake ya kale, nami nitajiunga na maandamano ya kuwang’oa hao mapacha maarufu.Wenyewe wanajua lakini wanajifanya hamnazo.
(hapa umepiga nondo kichwani kabisa)

Ni kweli baadhi ya mambo yaliyofanywa na mapacha maarufu ni ya hovyo, na mengi hayahitaji mjadala, lakini je, ni wao peke yao? Tukiisha ‘kuwatosa’ (Waswahili kwa kupenda kutosana!) ndiyo tutakuwa tumemaliza kazi?

Hao ‘watosaji’ na wanaovua magamba bila mpangilio wanajua kwamba kwa muda mrefu chama chao na serikali yao vimetekeleza sera za ugawaji (‘uuzaji’ wanasema wasiojua Kiswahili) mali za Taifa kwa bure, bure! Mifano ni mingi: madini yetu na Benki ya Taifa, na sasa ardhi kwa ajili ya kilimo cha petroli. Nyerere alipopiga kelele kuhusu kuigawa benki yetu kwa Makaburu alipuuzwana kudharauliwa ungedhani aliyesema Jenerali miye.Kisa, wakubwa wa Washington wamesema, na watawala wetu wakiambiwa na wakuu hao ‘Ruka!’ wanachouliza watawala wetu ni ‘Hadi wapi?’

Mwenyekiti wa chama-tawala wakati huo aliamua kwenda mbali zaidi kwa kujizawadia mgodi mzima wa serikali, kama mjasiriamali-mamboleo(taratibu Jenerali!
Che-Nkapa asije sikia!).
Chama chake, kimya! Najiuliza hilo
gamba wanalosema wanajivua ni gamba lipi, mbona yako mengi?
Ubanaji posho za vikao
Sasa hebu tuangalie namna ya kujivua gamba hili jingine. Kama alivyotabiri Kambarage, kumbuka, chama kikuu cha upinzani kimeamua kuitikisa misingi mibovu ya matumizi ya fedha za umma kwa kuasisi wazo la kubana posho za vikao ambazo kinadhani si halali hata kama zinalipwa kwa utaratibu uliowekwa kisheria (kumbuka kila kinachofanyika kisherria si lazima kiwe halali; ndiyo tofauti kati ya legal au lawful na legitimate).
...........

Chama cha upinzani kitakuwa si chama cha upinzani kama kitashindwa kuliona hilo na kuwapiga nalo(CCM) watawala na kupata kuungwa mkono na wananchi.

Hongera sana Jenerali Ulimwengu kwa kuwa one of the Greatest Thinkers of our times.
Ni makala kama hizi ndio iabidi Nd Mukama aiangalie kwa makini ili think-tank ya CCM iweze kuamka toka usingizini.
 
Kudos Jenerali, wape vidonge vyao. Nimependa sana yatokanayo na ulafi. Nakumbuka makala yako ile ingine kwenye RAI original juu ya mijitu hiyo hiyo inavyopenda MI-VYAKULA, MI-NGUO, MI-SAFARI, MI-PILAU, MI-PUMBAVU et al.
 
Kweli hii nchi itajengwa na wenye moyo...mtoto wa mkulima naye anageuka kuwa mwizi wa mali za walalahoi wa nchi hii?...kweli nimeamini mavi huwa hayawezi kufanana na mnyaji
 
makaha hii haina cha kuongezea, amesema yote na aliye na masikio asikie. Hapa ni nguvu ya hoja si uchama.
 
Bwana Pinda asitudanganye yeye ni mtoto wa mkulima.......hivyo anatetea wanyonge.......hata kidogo! Watumisi wa serikali na Wabunge ambao wanaona mshahara hautoshi waachie hizo nafasi kwani kuna wengine wengi wako tayari kuzifanya bila ya kulipwa hizo posho!!

Ni kweli kuwa ni mtoto wa mkulima. Ila kuwa mtoto wa mkulima hakumfanyi mtu kuwa mkulima au hata kuakisi tabia za kikulima.
 
Asante ulimwengu, makala imetulia,
natamani kila m TZ angepata nafasi ya kusoma makala hii ili apate kuelewa nini kinaendelea na apate cha kujifunza,
endelea kutuletea vitu moto moto kama hivi watu wafunguke.
Well done.
 
Nashukuru sana bwana ulimwengu nadhani umetuweka bayana. nadhani pia next time utatueleza juu ya vyama vya kidicteta maana haya ya ccm twapata kwakuwa wapo madarakani twaomba utumegee na vyama ambavyo havipo madarakani ila tuwe na yakini ya uchaguzi wa viongozi wema. maana nilipata kusikia **** mkuu mmoja wa chama flani alichukua fomu ya urais na kurejesha then ndio wakaitisha uchaguzi wa kuteuwa nani agombee urais ndani ya chama hicho na kuna diwani wao mmoja wa chama hicho hicho huko namtumbo alifanya kama alivyo fanya mgombea uraisi. nikajiuliza kweli hii ndio demokrasia? nataraji mengi kutoka kwako
 
dah, imekaa vizuri na inavutia, lkn mizengo sio mzalendo hata kidogo, na hana cha utoto wa ukulima wala nn,,,ungebaki na ubunge wake tu, kisha kuwa kero.
 
Hakuna njia ambayo ninaweza kutumia kumfikishia haya makala mhe. PM Pinda.
Maana kwa jinsi alivyochoka kimwili na kiakili sidhani kama hata anao mda wa
kusoma Raia mwema zaidi ya Uhuru na Habari leo.

His email address please? au FB yake?

Wakuu tunatakiwa kuvaa viatu vya Pinda, kabla ya kuanza kum-judge. Can you imagine cabinet yetu ya sasa? try to compare it with that of Ben. Hao ndio watu anaofanya nao kazi Pinda, angalia JK na vision yake kwa Tanzania ( kama ipo), kama hakuna watu kwenye timu, kama hakuna malengo na strategy utafanya nini uwanjani, inabidi uwe unajifurahisha tu. Tusije tukadhani kuwa walioko serikalini ni wajinga sana, wanaona zaidi kuliko sisi tulio nje, lakini wamebanwa au hawataki kuonesha uzalendo kwa nchi, wanathamini chama zaidi.
 
Well, well campain manager wa ccm kipindi kile! Yaaa, kwa hiyo ccm ilipoteza dira 1998? Halafu ikiwa very unfortunate teacher akatuacha untimely 1999,a serious blow! Na kwa sababu itikadi ya chama c ujamaa na kujitegemea_TUMEKWISHA?
 
I salute ujumbe umefika,na hakika malezi uliyopata Ndugu J toka kwa mwalimu yanatuonyesha sisi kizazi kipya kuwa Mwalimu bado ana Wanafunzi, wanaoweza kutuonyesha njia. Ndio tunajua hauna nafasi kwenye vyombo vya maamuzi lakini kupita media na umekuwa na mchango mkubwa wa yale mazuri mliojifunza toka kwa Mwalimu japo na kubaki na msimamo wako kwa yale ambayo hamkuafikiana na Mwalimu na hivyo kutimiza kuwa binadamu tunatofautiana kimawazo na mitizamo lakini tukiafkiana kwenye ukweli.
 
Back
Top Bottom