Jenerali Sarakikya: Utajiri wa watumishi serikalini unatisha!

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Mirisho Sarakikya, ameshangazwa na tabia ya baadhi ya watumishi wa serikali kuibuka na utajiri baada ya kufanya kazi kwa muda mfupi tu. Alisema huko nyuma watumishi waliitumikia serikali kwa miaka mingi na kustaafu wakiwa watu wa kawaida.

Alisema kuwa kwa siku za karibuni amekuwa anashangazwa na baadhi ya watu kujenga majengo makubwa yasiyolingana na mapato halali wanayolipwa na kuongeza kuwa anafahamu mishahara ya watumishi wa umma hakuna mwenye uwezo wa kujenga majengo hayo na kwa muda mfupi.
Jenerali Sarakikya alitoa kauli hiyo mjini Arusha jana, alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania (Muwawata).

“Mimi mwenyewe nilikuwa Mbunge, kisha nikawa waziri na kumalizia ubalozi na kustaafishwa rasmi na Jeshi mwaka 2004, bado sikuweza kujenga nyumba ya kifahari, bali nimejenga kibanda tu cha kuishi tena kwa miaka 10, iweje watu wajenge majengo hayo kwa muda mfupi?” Alihoji Jenerali Sarakikya.

Katika hatua nyingine, Jenerali Sarakikya ameilalamikia serikali kwa kulipa kiwango kidogo cha posho ya pensheni kwa wanajeshi wastaafu ya Sh. 300,000 baada ya miezi sita sawa na Sh. 50,000 kwa mwezi.

Jenerali Sarakikya alisema posho hiyo haiwezi kufanya kitu chochote kulingana na hali halisi ya maisha kwa sasa na wengi wao hujikuta katika wakati mgumu. Alisema kwa mujibu wa taratibu za jeshi, wanajeshi wengi hujikuta wanastaafu kwa vyeo vyao na sio kwa umri, jambo ambalo alisema wengi wao wanastaafu wakiwa bado wana nguvu za kutumikia taifa katika nyanja mbalimbali.

Nipashe
 
Hawa ndio waliofanya kazi tangu enzi za Nyerere na wanashuhudia madudu yanayotendeka ndani sirikali yetu tukufu ambayo mtoto wa mkulima anasema serikali iko makini sana na inafuata utawala wa sheria.
:majani7:
 
Mwanajeshi akistaafu analipwa tshs elfu hamsini kwa mwezi?aise
Kuhusu viongozi kuwa matajiri kwa muda mfupi,nadhani tatizo ni ile sera ya chukua chako mapema,fainali uzeeni.unategemea nini kama kiinua mgongo chenyewe ni elfu 50 kwa mwezi??
 
Sarakikya alikuwa ni zaidi ya mwanajeshi. Mkuu wa majeshi na balozi
 
Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Mirisho Sarakikya, ameshangazwa na tabia ya baadhi ya watumishi wa serikali kuibuka na utajiri baada ya kufanya kazi kwa muda mfupi tu.

Alisema huko nyuma watumishi waliitumikia serikali kwa na kustaafu wakiwa watu wa kawaida.
Alisema kuwa kwa siku za karibuni amekuwa anashangazwa na baadhi ya watu kujenga majengo makubwa yasiyolingana na mapato halali wanayolipwa na kuongeza kuwa anafahamu mishahara ya watumishi wa umma hakuna mwenye uwezo wa kujenga majengo hayo na kwa muda mfupi.
Jenerali Sarakikya alitoa kauli hiyo mjini Arusha jana, alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania (Muwawata).
“Mimi mwenyewe nilikuwa Mbunge, kisha nikawa waziri na kumalizia ubalozi na kustaafishwa rasmi na Jeshi mwaka 2004, bado sikuweza kujenga nyumba ya kifahari, bali nimejenga kibanda tu cha kuishi tena kwa miaka 10, iweje watu wajenge majengo hayo kwa muda

mfupi?” Alihoji Jenerali Sarakikya.

Na Cynthia Mwilolezi

8th June 2011

CHANZO: NIPASHE
 
Nadhani hata Jeshi alilofanyia kazi miaa hiyo na sasa yana tofauti kubwa sana. Sasa hivi magenerali wa JWTZ wanauwezo wa kununua hata scania 10 kwa mwezi . teh teh teh
 
Labda ndio mbinu mpya za medani kwa watumishi wa leo? lakini kama Utajiri wa kupindukia kwa watumishi wa umma kama hauna maelezo anayo haki ya kuhoji.
 
kama wameanza kusema kuna siku watachoka na kupindua nchi hawa

...Hili suala la wanajeshi linaskitisha sana....na ukweli ni kuwa wanawaangalia tu wanasiasa wanavyoiba ...wanaumia moyoni.....Kama ukiona General anapata kiiunua mgongo kisichotamkika ,ni wazi kuwa wanavumilia sana na inaonekana wanasiasa wamejisahau na hii Amani yetu tuliyonayo....

Jeshini angalau hawa wenye cheo cha maj general hadi general wanaunafuu wa kuhudumiwa na jeshi ....na huwewa magari kila baada ya miaka 5.....lakini hawa wanaoanzia cheo cha Brigedia General hawapati huduma baada ya kustaafu ..ukweli ni kuwa kuna ninao wafahamu na wanavumilia taabu sana....ni vema serikali ikaliangalia hili mapema......,hasa kwenye JWTZ ambako kiwango cha ufisadi na rushwa kiko chini...hata kama ufisadi unafanyika ..wenye hiyo access ni wachache sana .....wengi hasa walio mipakani wanaishi kwa mishahara...ni tofauti kabisa na polisi ambao wanakamata watu ....na kuomba kitu kidogo.....

Majenereali wa miaka ya nyuma kina Sarakikya, Musuguri,Twalipo,na Kiaro.....na wenzao walikuwa chini yao hawakuwa na kashfa za ufisadi ....ni wazi hata hali ya ufisadi iliyoanza kujitokeza enzi za Mboma ....ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na huduma zisizoridhisha wanazopata wastaafu.....na kuwafanya walio kwenye service wajiandae kustaafu.........hata kwa kununua ndege mbovu,hewa,silaha mbovu,madawa feki.misamaha ya kodi..etc

Sasa kama hawa maaskari wajuu wakilalamika mnategemea hawa wa chini wasemeje????

Serikali haishindwi kuhakikisha kuwa kila askari anayestaafu anapata makazi stahili ya cheo chake........kama atakuwa akikatwa kidogo kidogo tangu anaingia jeshini ....ni wazi mpaka anamaliza atakuwa na nyumba.....hili limeonekana kuwa tatizo kuu la askari hasa wa chini ukizingatia wengi hawakai sehemu moja muda ,au wako makambi ya huko mipakani.......na mishahara yao huishia kwenye pombe kujiliwaza...Rwanda wamefanikiwa kuanzisha mradi wa nyumba nafuu kwa askari .....zinajengwa na jeshi [mfano wa jkt] na kila askari anakopeshwa.......

Tusijisahau!
 
Sarakikya alikuwa ni zaidi ya mwanajeshi. Mkuu wa majeshi na balozi

Nilimsikia akilalamika utafikiri hakuwa Mkuu wa Majeshi? Yeye ni Jenerali Mrisho Salakikya, anamuomba hela Luteni Kanali Mrisho Kikwete, badala ya kutoa amri ya halali ya jeshi kwa Luteni Kanali aongeze mafao la sivyo achukue uamuzi wa kijenerali yeye ana lialia. Aende huko atutaki walalamishi karne hii!
 
Labda watumishi wa serikali wa kizazi hiki wamekuwa 'wabunifu' sana...

Pia mbali na ubunifu, siku hizi wanalima na kufuga sana na kufanya biashara. Si anajua kuwa siku hizi jumamosi ruksa kujishughulisha?:majani7:
 
...Hili suala la wanajeshi linaskitisha sana....na ukweli ni kuwa wanawaangalia tu wanasiasa wanavyoiba ...wanaumia moyoni.....Kama ukiona General anapata kiiunua mgongo kisichotamkika ,ni wazi kuwa wanavumilia sana na inaonekana wanasiasa wamejisahau na hii Amani yetu tuliyonayo....

Jeshini angalau hawa wenye cheo cha maj general hadi general wanaunafuu wa kuhudumiwa na jeshi ....na huwewa magari kila baada ya miaka 5.....lakini hawa wanaoanzia cheo cha Brigedia General hawapati huduma baada ya kustaafu ..ukweli ni kuwa kuna ninao wafahamu na wanavumilia taabu sana....ni vema serikali ikaliangalia hili mapema......,hasa kwenye JWTZ ambako kiwango cha ufisadi na rushwa kiko chini...hata kama ufisadi unafanyika ..wenye hiyo access ni wachache sana .....wengi hasa walio mipakani wanaishi kwa mishahara...ni tofauti kabisa na polisi ambao wanakamata watu ....na kuomba kitu kidogo.....

Majenereali wa miaka ya nyuma kina Sarakikya, Musuguri,Twalipo,na Kiaro.....na wenzao walikuwa chini yao hawakuwa na kashfa za ufisadi ....ni wazi hata hali ya ufisadi iliyoanza kujitokeza enzi za Mboma ....ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na huduma zisizoridhisha wanazopata wastaafu.....na kuwafanya walio kwenye service wajiandae kustaafu.........hata kwa kununua ndege mbovu,hewa,silaha mbovu,madawa feki.misamaha ya kodi..etc

Sasa kama hawa maaskari wajuu wakilalamika mnategemea hawa wa chini wasemeje????

Serikali haishindwi kuhakikisha kuwa kila askari anayestaafu anapata makazi stahili ya cheo chake........kama atakuwa akikatwa kidogo kidogo tangu anaingia jeshini ....ni wazi mpaka anamaliza atakuwa na nyumba.....hili limeonekana kuwa tatizo kuu la askari hasa wa chini ukizingatia wengi hawakai sehemu moja muda ,au wako makambi ya huko mipakani.......na mishahara yao huishia kwenye pombe kujiliwaza...Rwanda wamefanikiwa kuanzisha mradi wa nyumba nafuu kwa askari .....zinajengwa na jeshi [mfano wa jkt] na kila askari anakopeshwa.......

Tusijisahau!

Au ndo maana wanageukia siasa baada ya kustaafu?

Lakini wanakumbukwa sana kwenye ukuu wa wilaya, mkoa, na baadhi ya vitengo . Polisi ndo wanasahaulika kabisa wakistaafu.
 
Back
Top Bottom