Jenerali: Msekwa umeajiri wahuni wa kutosha, usifanye uhuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jenerali: Msekwa umeajiri wahuni wa kutosha, usifanye uhuni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkulima mimi, Aug 12, 2010.

 1. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  [​IMG]
  Na Jenerali Ulimwengu
  Agosti 11, 2010
  Raia Mwema


  KATIKA hali tuliyoishuhudia wakati wa kura za maoni ndani ya chama - tawala si rahisi kwa ye yote anayefuatilia masuala ya siasa za nchi hii kupuuza masuala yaliyojitokeza. Masuala haya ni mengi, na bila shaka tutaendelea kuyajadili kwa muda mrefu, lakini wiki tunaweza kuyagusia baadhi yake kabla hayajapoa.

  Kwanza, kama nilivyosema wiki jana, siasa za chama-tawala kunyata. Mambo tuliyoyashuhudia katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM yanakifu, yanachusha, yanatia kinyaa.

  [​IMG]
  Pius Msekwa

  Lakini ni zaidi ya hayo. Kuchusha pekee, ama kutia kinyaa, si jambo jema na wala si hali ya kupendeza. Mtu anaposema anaona kinyaa, labda athari kubwa inayoweza kumtokea ni kupata kichefuchefu na hatimaye kutapika. Kwa yale tuliyoyaona mwaka huu, si uongo kusema kwamba kama kuna watu miongoni mwetu ambao bado wana chembe za uungwana, wamepata kichefuchefu, na wengine labda walijisikia kutapika.

  Lakini kichefuchefu si sawa na kifo, na hutokea mtu aliyekolewa na kichefuchefu akafikia hata hatua ya kutapika na bado asife iwapo kutapika kwake hakutokani na maradhi yaliyo mwilini mwake bali ni kutokana na kichefuchefu kinachotokana na hali ya kuudhiwa na kuwa na kinyaa. Binadamu wanao uwezo mkubwa wa kushuhudia mambo ya kuudhi na bado wasife kutokana nayo.

  Hata hivyo, mambo hayo yanaudhi, yanakera. Isitoshe, baadhi ya yale tuliyoyashuhudia siyo tu yanaudhi, ila pia yanatisha. Yanatishia usalama wetu kama Taifa kwa sababu yanao uwezo wa kutupeleka mahali ambako hatukutarajia kwenda, mahali pa kutuhilikisha.

  Niliwahi kueleza kwamba tumeanza kutumia lugha nyepesi kuelezea dhana nzito. Nimekuwa nikijaribu kueleza kwamba kile tunachokiita ‘kero' mara nyingi si kero bali ni janga, ni hatari, ni saratani, ni ukoma. Rushwa, kama rushwa, ndani ya jamii haiwezi kuwa kero; ni janga kwa sababu inao uwezo wa kuua jamii nzima.

  Lakini, pia, rushwa ni kielelezo kimojawapo cha uoza, na vielelezo vipo vingi. Katika michakato ya uchaguzi, ni kweli, tumeshuhudia vitendo vya rushwa, kwa maana ya watu kugawa fedha na wengine kupokea fedha hizo kwa madhumuni ya kuathiri matokeo ya uchaguzi. Hiyo ni rushwa kama ile anayotoa mtu mwenye shauri mahakamani kumpa hakimu, au mtu mwenye tatizo la kiusalama kumpa askari polisi.

  Uoza wa aina hiyo umetokea sana katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama-tawala, na ni vyema kuukemea kwa nguvu zetu zote, na ni lazima kukataa na kutupilia mbali kauli za kipuuzi za watu kama wasemaji wa chama-tawala niliowasikia. Upuuzi ukisikika, tujifunze kuutaja kama upuuzi, na huu ni upuuzi.

  Sasa, ndani ya chama-tawala wametokea wahuni waliohamia huko na kisha wakapewa kibarua cha kutoa matamko ya kipuuzi mara kwa mara, maneno yenye mantiki iliyopinda na isiyoweza kumshawishi hata mgonjwa wa Mirembe. Hawa wanajulikana, asili yao inaeleweka, na kwa maana hiyo hawashangazi wanapotoa matamko yasiyokuwa na mantiki yo yote ila tu kujaza nafasi katika vyombo vya habari kwa sababu ni muhimu kwa wanajamii kujua kwamba chama-tawala kimejibu shutuma hii au ile.

  Lakini kwa kuwaendekeza wapuuzi kama hawa, na kuwazoea kama wasemaji wa mara kwa mara wa chama-tawala, ipo hatari kwamba hata watu wasiotarajiwa kutamka maneno ya kihuni kuingia katika mkumbo huo na kujisemea tu, alimradi wamesema. Mazoea huzaa hulka, na hulka huzaa utamaduni.

  Ndivyo ninavyomwangalia Pius Msekwa, makamu mwenyekiti wa chama-tawala, na jinsi anavyozungumzia janga kubwa la uoza ndani ya chama chake. Msekwa anasema kwamba, na anataka tuamini kwamba tatizo la rushwa haliwezi kuwekwa mlangoni kwa chama chake, kwa sababu ni tatizo la Taifa zima.

  Hapa kama kuna mtu amemwelea Msekwa, naomba anisaidie. Ni kweli tatizo la rushwa ni la Taifa zima, lakini kwa nini liseelekezwe kwa chama-tawala, chama ambacho, kama wanavyotamba wasemaji wake, ndicho kilichopewa dhamana ya kuongoza Taifa letu? Ni chama hicho kilichoomba, tena kwa nguvu za fedha na jeuri za aina nyingine, kipewe madaraka ya kuongoza nchi yetu, na hiyo dhamama kikapewa.

  Sasa, kama nchi nzima imejaa rushwa, kama alivyoeleza Msekwa kwa ufasaha mkubwa, sisi tumwulize nani kama si chama hicho? Lakini labda Msekwa, kwa kuathirika kutokana na ule upuuzi ulioingizwa ndani ya chama chake na wale wahuni niliowataja mapema, alisahau kwamba alikuwa anaulizwa swali kuhusu chama chake.

  Ni kweli, kama anavyosema Msekwa, rushwa iko polisi, iko mahakamani, iko hospitalini, iko vyuoni, iko kila mahali. Lakini ukweli huo hauwezi kuwafanya wadadisi wasimuulize Mkuu wa Polisi kuhusu rushwa katika jeshi lake, au wasimuulize Jaji Mkuu kuhusu rushwa katika mahakama zake, na kadhalika. Sijui Msekwa alitaka nani aulizwe kuhusu rushwa ya kutia kinyaa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama chake. Tumwulize Waziri wa Afya?

  Watu kama Msekwa wanatakiwa waache upuuzi kwani dhamana waliyo nayo ni kubwa mno, wakiendelea na upuuzi wao sote tutaathirika. Hii ndiyo sababu sichelei kumwambia Msekwa kwamba umri wake, uzoefu wake, historia yake, elimu yake na hadhi yake.. vyote hivi havimpi ruksa ya kuzungumza kihuni. Chama chake kimewapa ajira wahuni wengi ambao wanatosha kabisa kutuchekesha huku tukilia machozi.

  Hata hivyo, najua kwamba uhuni huu ukiachiwa ukaendelea, siku moja hata hicho kicheko katikati ya machozi kitakatika, na kilio kitakuwa ni cha moja kwa moja. Msekwa anataka kutuambia kwamba hata udanganyifu wa viongozi na watumishi wa chama chake si tatizo la chama chake?

  Kama Msekwa na wakuu wengine wa chama-tawala hawaoni kwamba uingizaji wa kadi bandia za uanachama katika michakato ya ndani ya chama hicho si tatizo la chama, ni nini wanachokiona? Hujuma kama hii ingefanywa na chama kingine kinachotaka kukidhoofisha chama-tawala, ingeeleweka. Kwamba watu ndani ya chama hicho wanakihujumu kwa makusudi kabisa halafu wakubwa wake hawaoni kwamba kuna tatizo, ni uthibitisho kamili kwamba nchi hii imo mikononi mwa watu wa kutisha.

  Kumbukumbu zangu zinaniarifu kwamba mwaka 1977, katikati ya sherehe zilizotangulia muungano wa TANU na ASP kuunda CCM, Pius Msekwa alikuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM. Katika hafla mojawapo ya maadhimisho hayo, Msekwa alitoa tamko lililosema kwamba jina ‘Chama Cha Mapinduzi' halikuwa na maana kwamba kila mwanachama wake angetakiwa kuwa mwanamapinduzi.

  Hii bila shaka ilikuwa na maana kwamba mtu hakuhitaji kuamini itikadi yo yote ili kuwa mwananchama wa CCM. Lakini aliyekuwa rais wa ASP, Aboud Jumbe, alimkosoa Msekwa kwa kubainisha kwamba ili kuwa mwanachama wa chama kinachoitwa cha mapinduzi ni mantiki ya kawaida kwamba lazima mtu awe mwanamapinduzi. Leo nadhani kwamba mshindi katika ubishi huo wa miaka thelathini na tatu iliyopita ni Msekwa. Naamini ndiyo maana bado anakiongoza chama chake cha mapinduzi kisichokuwa na wanamapinduzi.

  Hata kama tutakubali kwamba sisi sote tu vipofu, si tumsikilize Bwana Issa bin Maryam, aliyetufundisha kwa kuuliza swali hili: Je, kipofu anaweza kumwomgoza kipofu mwenziwe? Si wote watatumbukia katika shimo?

  Itaendelea...
   
 2. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tunahitaji akina Jenerali wengi zaidi wa kuweza kuwaondolea uvivu viongozi wa CCM wanaofanya na kusema mambo ya ajabu kutetea uozo ulio kwenye chama hicho ambacho kwa sasa si chama tena bali gulio la wala na watoa rushwa! bila soni Msekwa kasahau kile kiapo cha wana CCM kinachosema 'RUSHWA NI ADUI WA HAKI; SITATOA WALA KUPOKEA RUSHWA.

  Kama Makamu wa Mwenyekiti wa CCM anaweza kutamka maneno hayo ni wazi chama hicho kimeishachafuka na kinatoa harufu ya uvundo wala si chama tena kinastahili kuchimbiwa shimo na kufukiwa ardhini!

  Pius Msekwa atamwambia nini Mwalimu Nyerere akitokea sasa hivi na kumuuliza ajieleze kuhusu kauli yako? ni aibu na fedheha kubwa wale wale waliokuwa wanajitia ni wafuasi na wasaidizi wa karibu na Mwalimu na siasa zake hivi sasa ndio wasaliti wakubwa!
   
 3. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  like fathers like sons
   
 4. K

  Kinombo JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2010
  Joined: Feb 24, 2007
  Messages: 332
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ''wameota mapembe'' wamejilimbikizia mali kifisadi .... tuliwasomesha Bure, sasa sisi kusoma ni shida hakuna mikopo, na wao wanazidi kutufisadi....muulize ni mwenyekiti bodi ngapi huyo????

  Yu wapi Salim Ahmed Salim???????????
   
 5. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  amesusa baada ya kushindwa fitna!
   
 6. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wakati mmoja wakati wa utawala wa Rais Daniel arap Moi balozi wa Uingereza nchini Kenya alisema alisema haya kuhusu mawaziri wala rushwa nchini Kenya "Wamekula mpaka wakavimbiwa na sasa wanatutapika katika miguu yetu"

  Msekwa na genge lake la wahuni wamekula rushwa mpaka sasa wanahalalisha kuwa ni sehemu ya utamaduni wa Taifa letu hivyo hashangazwi na Rushwa kukithiri CCM.

  HUKO NDIKO KUTAPIKIA MIGUU YA WATANZANIA KAMA MAWAZIRI WA KENYA WALIVYOTAPIKIA MIGUU YA WAFADHILI
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkulima mimi, ukiwa na watu kama Tambwe Hizza na hata Makamba katika Chama Chetu tawala, basi wala hatuhitaji Chadema kuanguka!
  Wao kuua chama tosha kabisa.Mismanagement ,ukosefu wa dira na kiujumla chama kuenda shaghala bagala kufikia hatua kuwa idara ya serikali, huo ndo mwanzo wa kifo wa chama.
  Chama kinaanza kutekeleza matakwa ya walio katika uongozi badala ya wananchi.
  Bahati mbaya hata Msekwa ameingia katika kundi la oppurtunists, waganga njaa uzeeni!
  Msekwa anafahamu chama kilitoka wapi lakini nina uhakika hajui kinakoelekea!!
   
 8. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2010
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Rushwa kila mahali ni Zao la CCM. Kwani Msekwa hajui kuwa CCM ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha kuwa rushwa polisi, mahakamani, n.k. hazipo? Hao watoa rushwa na wapokea rushwa wote si ni mawakala wa utawala wa CCM?? Wakati wa uchaguzi hawa wanatoa rushwa ili kuingia madarakani, wakishaingia madarakani wanageuka kuwa wapokea rushwa! Hawatoi tenda mpaka rushwa iingie mfukoni. Hawaajiri mpaka rushwa ziingie mifukoni. Wakuu wa hivyo vyombo vyote anavyosema msekwa vimejaa rushwa huteuliwa na kuingizwa pale na UONGOZI MKUU KABISA WA CCM. Wanaenda pale kutekeleza sera na malengo ya serikali ya CCM. Ikiwa sera na malengo yao ni kuhakikisha viongozi wa CCM wanatajirika kupitia malipo yasiyokuwa na mpangilio hilo watalifanya. Wakishafanya hayo nao watajimegea cha kwao; ni nani atawasema wakati yeye mwenyewe anajijua analipwa malipo yasiyo halali?

  Majaribio ya kuitenganisha CCM na kuzagaa kwa rushwa nchini ni sawa na majaribio ya Mbuni kujificha kwa kuchomeka kichwa chake kwenye mchanga!! Hizi rushwa za wakati wa uchaguzi ndo mama wa rushwa zote. Viongozi walioingia kwa rushwa watamzuia nani kula rushwa?? Ikiwa si wajibu wa viongozi kuzuia rushwa serikalini, ni wajibu wa nani??

  Oooooh, huu ni uhuni kama anavyouita huyu mwandishi. Serikali ya wahuni, inaongoza kihuni huni na kuongea kihuni tuu........samahani ila huu ndo ukweli wenyewe.
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Msekwa mtu ovyo kabisa, hii trick ya kusema "mbona fulani naye amefanya" is the oldest in the book. Two wrongs do not make a right.

  Traffic cop akikusimamisha kwa sababu una speed (or for any other offence for that matter) huwezi kumwambia "mbona yule naye ana speed ?"

  Swala si yule, swala ni wewe, sheria inaweza kushindwa kuwakamata wahalifu wote, lakini ikikukamata wewe, hata kama ni kwa ajili ya kutoa mfano tu, swali pekee lenye maana ni "umefanya hilo kosa au hujafanya ?". Hizo habari za "yule naye kafanya" hazikusaidii, pengine zitaonyesha tu kwamba unakubali kwamba umekosea.
   
 10. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Msekwa anasema rushwa haipo ccm tu ipo kila mahali. Ukiangalia msingi wa jibu hilo ni kuwa ccm wasiulizwe wao kuhusu rushwa ya uchaguzi kwani rushwa sasa ni utamaduni wa mtanzania sasa watanzania mnashangaa nini? Kipi kipya? Mawazo ya msekwa na alio waajiri nahisi tambwe ni miongoni mwa waajiriwa hayawezi hata kumshawishi mgonjwa wa mirembe.
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Aug 12, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  nakubaliana nae mzee ulimwengu kabisa.
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Asante sana jenerali unajua kutumia kalamu yako!
   
 13. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #13
  Aug 12, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Uko sahihi, nsakupa tano, uko juu.
   
 14. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwenye rangi nyekundu, ndugu zangu watanzania hii nchi ni yetu sote na wala si ya Marehemu JK Nyerere. Lakini cha msingi JK Nyerere alishakufa kwa hiyo tunatakiwakujenga hoja za kuwafanya viogozi wetu wawajibike kutoa maelezo kwetu sisi wananchi ambao tunaishi sasa na si kwa marehemu. Inamaana watanzania wote hawaathiriki na janga la rushwa bali ni marehemu pekee!!!!!!. Nafikiri hoja zetu tunatakiwa kuzijenga zisimame kwa nguvu na mantiki zinazobeba na si kutegemea kumtaja marehemu JK Nyerere kuwa ndo sehemu ya nguvu ya hoja.

  Ukiacha dosari hiyo kwnye mchango wako mimi pia naunga mkono hoja na ujasiri wa Ulimwengu.
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  IshaLubuva,

  Naelewa unachosema, na zaidi tunatakiwa kwenda kwa principles kuliko personalities.

  Nafikiri Ulimwengu anachojaribu kufanya ni kuonyesha kwamba Msekwa yuko wrong by any measure, ukichukua principles yuko wrong, hata ukichukua misimamo ya watu kama Nyerere anayeitwa "Baba wa Taifa" ambaye CCM haiishi kumtumia kama dira na kitu cha kutafutia legitimacy, Msekwa anakosea. Ningekuwa na matatizo na Ulimwengu kama angeanza kumsema Mekwa moja kwa moja kwamba kafanya vibaya kwa sababu hata Nyerere alikemea hili, lakini Ulimwenu hakufanya hivyo, amejenga hoja, ametumia basic principles, sasa katika kutafuta namna nyingine ya kuongezea criticism yake akamtumia Nyerere, hakuna ubaya.

  Kama vile ambavyo hatutakiwi kumtumia Nyerere kama juzuu la kila kitu, upande mwingine wa reasoning hiyo hiyo unatutaka tusiogope kumtumia Nyerere pale aliposema la maana, eti kwa sababu tu ni Nyerere alisema au amefariki. Cha kuangalia ni, je alilosema ni la msingi ? Lina maslahi kwa wananchi? Lina mafundisho ? In this case the answer to all these questions is a resounding YES, and Ulimwengu is strongly justified.

  Nisichopenda ni kujenga a Mao like cult of personality, kila kitu lazima kipate baraka ya Nyerere hata pale ambapo Nyerere hajasema kitu watu watafute some obscure quote, au hata pale Nyerere alipokosea tufuatishe tu, kwa sababu yeye Nyerere. Clearly the above case has none of these scenarios. Nyerere alipinga rushwa vibaya sana (angalau kwa maneno) na katika makala inayopinga rushwa sioni ubaya katika kuyatumia maneno yake kama dira.
   
 16. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kama nchi nzima imetapakaa rushwa baada ya CCM na kabla yake TANU/ Afro Shirazi kushika utamu toka tupate uhuru, ni sababu tosha kuwaambia wampishe mwingine ajaribu bahati yake maana kama wameshindwa kwa karibu nusu karne miaka mingine mitano hawataweza kufanya kitu. Kukubali kwao ni dalili kuwa wamechoka na hawana kipya. Wakae pembeni ili wavute pumzi wakati mwenye nguvu mpya anaingia kwenye mpambano dhidi ya rushwa na majanga mengine!

  Amandla.......
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Msekwa hapa si kwamba kakubali tu kwamba rushwa ipo CCM na nchi nzima, na CCM imeshindwa kumaliza tatizo la rushwa ndani yake na nchini kiujumla, bali ukisoma maana utajua kaipendekeza rushwa kama mfumo wa maisha, haoni ubaya wake.

  Basically Msekwa anasema "kilichoingia mjini hakina haramu". Anaitafutia rushwa legitimacy kwa sababu kila mtu anatoa/ pokea. Iwekeni katika sheria kabisa, mu i tax kabisa.

  Wapinzani mnasubiri mualiko gani rasmi kumrarua ?
   
 18. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kirangi mimi sijakosoa mawazo ya Ulimwengu wala ya mwanzishaji thread lahasha, mimi nimekosoa Boramaisha alivyompa marehemu Nyerere jukumu la kumfanya Msekwa aone kwamba rushwa ni mbaya. Na wala sijasema kwamba tusitumie nukuu za marehemu Nyerere pale ambapo tunaona kwamba zitasaidia kujenga hoja, nilichokisema ni pale mtoa hoja anaposema "kama Mwalimu angekuwepo ............" wakati tunajua fika kwamba hawezi kuwepo tena. Hata kwenye mahubiri ya kiimani huwa wachungaji hawasemi kwamba yesu angekuwepo bali yesu alisema .......; vivyo hivyo na kwa masheskh wanaponukuu Kurani.
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Nimekuelewa, mie nikafikiri umeandika pia kuhusu reference ya Ulimwengu ya Mwalimu. Sorry.

  Hilo jambo unalosema nimeliona, wengine wanataka Nyerere afufuke kuja kutuongoza, wengine "kama Mwalimu angekuwapo..." nyingi sana. Mwalimu anaishi bado katika ideas zake, kaandika essays kibao katoa speeches kibao, kwa hiyo kama uko interested na ideas unaweza kupata muongozo bila hata ya Mwalimu kuwa hai.

  It is interesting ulivyoleta parallel ya Mwalimu na Yesu, frankly it is tempting to draw a parallel between "What would Nyerere do" and "What would Jesus do" and conclude that the former is a carbon copy of the latter. Some of us would say this is an attempt to deify Nyerere. Let's face it, on some blatant black and white issues most probably a trend can be drawn and we can make a conclusion that Nyerere would be against corruption. Lakini mambo mengine utakuta watu wanajivika UNyerere bila aibu na kumsemea mzee wa watu kashajifia, kujifanya tunajua sana kila Nyerere angefanya ni kum simplify.

  Moreover, Nyerere kafariki miaka kumi iliyopita, vitu vinabadilika. I used to think Nyerere was some kind of a genius, but as I get older I realize the many ways he was fallible, he was the first to admit that.

  Hata huyo Yesu masihi angekuja leo na kutuletea habari za kutoa mapepo kutoka vichaa na kuyaingiza katika wanyama mamia waende kutumbukia mtoni (Matthew 8:28-34, Mark 5:1-20, and Luke 8:26-33) People for the Ethical Treatment of Animals wangemkwida. Kwa hiyo mara nyingine hata kutumia mifano ya manabii kunaweza kuwa out of context.
   
 20. fige

  fige JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TUMSAMEHE JAMANI BADO ANAWEWESEKA KWA FITNA ZA 2005,WAKATI ULE ANGALAO ALIKUWA NA UBONGO.
  SASA HIVI WAMEMDANGANYA NA KACHEO ALIKONAKO ANAWEWESEKA TU ,USIDANGANYIKE MZEE HUJAONA WENZIO WALIOSTAAFU WANAVYOSEMA NA KUTOA HOJA KWA KUJIAMINI mf Warioba
   
Loading...