Jenerali 'Msauzi' Azungumza Kiswahili Msiba wa Mandela!

K-Boko

JF-Expert Member
Aug 3, 2013
697
218
Nilifurahi sana kuona Msemaji wa Jeshi la Afrika Kusini Brigedia Jenerali Solani leo akifanya mahojiano kwa Kiswahili alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya Mwandishi wa BBC-Swahili nchini humo Bw. Ali Mutasa kuelezea makabidhiano ya mwili wa Mzee Mandela toka kwa Jeshi la nchi hiyo kwenda kwa chama chake cha ANC kesho ili wauage mwili wa mwanachama huyo maarufu wa chama hicho kikongwe cha siasa kuliko vyote Afrika. Akasema, kwa kiswahili kinachoeleweka, kuwa mwili huo utarejeshwa kwa jeshi keshokutwa asubuhi, tayari kwa maziko siku hiyo hiyo kijijini Qunu. Akaongeza kuwa maziko ya Mzee Mandela aliyefariki dunia trh 5 mwezi huu yatasimamiwa na jeshi! (Sijui yule kamanda alikuwa Mazimbu enzi zile!? Kiswahili oyeee!!)

Source: BBC-Swahili Service News
 
Ni kweli hata mimi nimemwona nikashangaa, pengine alipata mafunzo na kusoma hapa Tz
 
Yule Brigedia Generali mara nyingi nimewahi kuona mahojiano yake hasa BBC Swahili anaongea kiswahili kizuri sana.
Na kama ulivyosema mleta mada nami nimeona hayo mahojiana yuko vema kwa upande wa kiswahili ambacho hapa nyumbani kinasuasua kila uchao.
 
Hasa vijana wa Bongo fleva, waharibifu wakubwa wa Kiswahili!
 
Nilifurahi sana kuona Msemaji wa Jeshi la Afrika Kusini Brigedia Jenerali Solani leo akifanya mahojiano kwa Kiswahili alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya Mwandishi wa BBC-Swahili nchini humo Bw. Ali Mutasa kuelezea makabidhiano ya mwili wa Mzee Mandela toka kwa Jeshi la nchi hiyo kwenda kwa chama chake cha ANC kesho ili wauage mwili wa mwanachama huyo maarufu wa chama hicho kikongwe cha siasa kuliko vyote Afrika. Akasema, kwa kiswahili kinachoeleweka, kuwa mwili huo utarejeshwa kwa jeshi keshokutwa asubuhi, tayari kwa maziko siku hiyo hiyo kijijini Qunu. Akaongeza kuwa maziko ya Mzee Mandela aliyefariki dunia trh 5 mwezi huu yatasimamiwa na jeshi! (Sijui yule kamanda alikuwa Mazimbu enzi zile!? Kiswahili oyeee!!)

Source: BBC-Swahili Service News
Hayo ndio matokeo mazuri ya ukombozi wa kusini mwa Afrika!

Ndoto ya Mwalimu imetimia, hao majenerali ni matunda mazuri ya sera ys kumkomboa mwafrika.
 
Wa-tz hawabebeki ni kama gunia la misumari. Hivi mnataka wasauzi watusaidie nini tusichokuwa nacho? Kama ni bahari sote tunazo, gesi sote tunayo, madini sote tunayo, ardhi ya kilimo tunawazidi, uranium tunawazidi, mnataka msaada gani kama sio laana?
 
Bingwa, hakuna popote katika hoja yangu nilipogusia habari ya msaada!
 
..ingefurahisha zaidi kama huko kwenye luninga tungeona BIDHAA zilizotengenezwa Tanzania.

..unajua wenzetu Wajapani au Wajerumani wakiangalia luninga toka nchi mbalimbali wanaona bidhaa[magari, mashine, etc etc] ambazo ni "med in" Japan au Germany.

..mpaka sasa hivi hakuna nchi yoyote ile zaidi ya Tanzania ambayo ime-adapt Kiswahili kama lugha yao ya taifa. hiyo ni pamoja na kujisifia sana kwamba tumewakomboa ndugu zetu wa kusini mwa afrika toka makucha ya ukoloni.

cc masopakyindi, @K-Boko
 
Yule Brigedia Generali mara nyingi nimewahi kuona mahojiano yake hasa BBC Swahili anaongea kiswahili kizuri sana.
Na kama ulivyosema mleta mada nami nimeona hayo mahojiana yuko vema kwa upande wa kiswahili ambacho hapa nyumbani kinasuasua kila uchao.
hapa kwetu tbc wana kipindi cha this week in perspective
 
Pale hakuna wasouth Africa; kuna wazungu wanaoishi South Africa ndo maana hawaipi promo TZ, lakini nadhani wazawa na viongozi waapreciate sana mchango wetu. JK ni kati ya viongozi wachache watakaopewa nafasi ya kutoa neno la buriani siku ya mazishi kwa niaba ya watanzani. Natamani angetumia kiswahili walau kidogo awakumbushe wapiganaji na ibaki kwenye kumbukumbu. Italeta ladha flan.
 
Back
Top Bottom