Nilifurahi sana kuona Msemaji wa Jeshi la Afrika Kusini Brigedia Jenerali Solani leo akifanya mahojiano kwa Kiswahili alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya Mwandishi wa BBC-Swahili nchini humo Bw. Ali Mutasa kuelezea makabidhiano ya mwili wa Mzee Mandela toka kwa Jeshi la nchi hiyo kwenda kwa chama chake cha ANC kesho ili wauage mwili wa mwanachama huyo maarufu wa chama hicho kikongwe cha siasa kuliko vyote Afrika. Akasema, kwa kiswahili kinachoeleweka, kuwa mwili huo utarejeshwa kwa jeshi keshokutwa asubuhi, tayari kwa maziko siku hiyo hiyo kijijini Qunu. Akaongeza kuwa maziko ya Mzee Mandela aliyefariki dunia trh 5 mwezi huu yatasimamiwa na jeshi! (Sijui yule kamanda alikuwa Mazimbu enzi zile!? Kiswahili oyeee!!)
Source: BBC-Swahili Service News
Source: BBC-Swahili Service News