Jemus Mbatia Shughurikia Rushwa inayotajwa kutolewa leo na kada Florian ama sivyo mupo CCM-C!!!!

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
Leo imetajwa kuwa kada wa NCCR ametoa Rushwa wakati Faustin Sungura anakemea Rushwa ya CCM:
Sasa yafaa Mbatia naye achukue hatua dhidi ya rushwa hiyo angalia hapa!!!!!!
[h=2]NCCR yapinga rushwa muda huohuo wakitoa rushwa hapohapo[/h]
Chama cha Siasa cha NCCR MAGEOUZI kimejikuta kikiwa katika hali ya kutoeleweka baada ya kuilalamikia Rushwa iliyopo katika chama Mwenzake CCM kwa kusema kuwa itawashugulikia viongozi wake walioingia madarakani kwa Rushwa baada ya miezi sita wakati huohuo NCCR ikatoa Rushwa kwa waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo leo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano huo, Makamu mwenyekiti wa Chama hicho Bw, Faustine Sungura, amesema kuwa hawapo tayari kuvumilia Rushwa kwa miezi sita kama ilivyo ahidiwa na Makamu wake Mangula.

Sungura amesema kuwa wanatoa siku saba kwa CCM kuhakikisha kuiagiza Serikali yake kuikomesha Rushwa na matendo yanayoendana nayo ndani ya siku saba kuanzia sasa.
"enzi za mwalimu Nyerere tulikuwa tunapata tabu sana kuwabaini wala rushwa tofauti na sasa ambapo wala Rushwa wote wanajulikana", amesema Sungura
Chakushangaza baada ya Makamu mwenyekiti kuongea na kuonyesha jinsi alivyokerwa na Rushwa iliyopo katika CCM, Afisa habari wa chama hicho Bw, Florian Lutayigwa alianza kuwagawia Baadhi ya waandishi waliokuwemo katika mkutano huo shilingi 5000 kila mmoja ambazo wengi tulitafsiri kwamba ni Rushwa ili waandishi wakaiandike habari hiyo kama ilivyo.
Na wakati akitoa pesa hizo alikuwa anawaambia waandishi hao kuwa wahakikishe wameandika story kwani kesho atanunua magazeti kuona kama habari imetoka.

IMG_0248.JPG
Hawa ni waandishi wa habari waliokuwemo kwenye mkutano huo


IMG_0270.JPG
Hapa Bw, Florian Lutayigwa akitoa pesa kwa waandishi waliohudhuria katika mkutano huo

 
Kama kweli ni rushwa kwa nini mliipokea? Nyie pia mnatakiwa kushughulikiwa. Vinginevyo wacha majungu.
 
Back
Top Bottom