Jemus Mbatia ajivue nafasi ya Mwenyekiti Taifa baada ya Kuteuliwa na Kikwete CCM!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jemus Mbatia ajivue nafasi ya Mwenyekiti Taifa baada ya Kuteuliwa na Kikwete CCM!!!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Emil Mwangwa, May 3, 2012.

 1. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Maalimu Seif Wa CUF aliambiwa kujivua nafasi ya Katibu Mkuu Taifa baada ya kuteuliwa na serikali sasa Mbatia anaponaje???
  Kama Mbatia atabaki kuwa Mwenyekiti Taifa hii ina maana gani kwa Mipango ya kupambana na CCM???

  CDM waliweka msimamo kushirikiana na NCCR baaada ya kesi ya Kawe kuisha je Watashirikianaje na Mbatia ambaye tayari ni mteule wa Kikwete??/
  Je Mbatia anaweza kumupinga bosi wake Kikwete na kumukosoa ??

  Je Mbatia Kuongoza NCCR kwa nafasi ya juu ni kuimarisha upinzani???
   
 2. Jackal

  Jackal JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 2,203
  Likes Received: 1,309
  Trophy Points: 280
  Mbatia ni Mbunge na hajawa waziri,kwa hiyo ana report kwa raisi au kwa Bunge ambapo mwakilishi wa wananchi?   
 3. Y

  Yasser5 JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamn kwna mbatia kawaje ?
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Mbatia siyo mwakilishi wa Wananchi, ni mteule wa Rais na ataendelea kuripoti na kufuata Sera na Maslahi ya Rais ndani ya Bunge, hili wala haliitaji Degree kulifahamu.
   
 5. +255

  +255 JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Jemus = James
   
 6. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 2,172
  Trophy Points: 280
  Huyo aliyemteua mliwa Kiboga kulikoni tena au ndio Mwendo wa Mla Huliwa?
   
 7. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  mbatia ni mwenyekiti taifa nccr anawawakilisha wanachama nccr kwenye upinzani na kukosoa utendaji wa rais .!!!
  Je mbatia anaweza kukaa meza moja wakapanga mikakati ya kumukosoa kikwete kama wapinzani???
  Mbatia hawezi kuvujisha siri upinzani kwa kikwete ambaye ni mteule wake???

  Hapo mwanachama wa nccr hawana mwenyekiti!!!
   
 8. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  [h=2]e NCCR-Mageuzi na CUF nyingine?[/h]  [​IMG][​IMG]


  • [​IMG][​IMG]


  Kuteuliwa kwa mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia kuwa mbunge ni muendelezo wa siasa za kulipana fadhila hasa baada ya wahusika kuwa makapi. Mbatia licha ya kushindwa kwenye uchaguzi, anadhihirisha uvumi uliowahi kuwapo kuwa ni pandikizi la CCM kwenye upinzani. Ingawa si shurti kwa rais kujieleza anapomteua mtu wake, uteuzi wa Mbatia unaacha maswali mengi kuliko majibu. Je NCCR-Mageuzi ni CUF au hata TLP nyingine na Mbatia ni Shariff Hamad au Augustine Mrema mwingine ambaye yuko radhi akitoa chama kafala kwa sababu ya ulaji binafsi? Je hapa rais hajaanza kuuathiri upinzani?
   
 9. Emil Mwangwa

  Emil Mwangwa Senior Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  [h=2]teuzi wa Mbatia zaweza kuwa Mbinu Chafu za CCM[/h]
  Ni vigumu kuona kama kweli kuna faida ya kuwa na mbunge kama Mbatia. Ameteuliwa baada ya kuwa ameshindwa kuwa mbunge kwa mbinu zote, kwenye box la kura na hata mahakamani.

  Sasa angalia msimamo wa kisiasa hapa nchini. Kwa kiwango kikubwa CHADEMA kimegeuka kuwa chama kikubwa cha upinzani. CUF wamerudi nyuma na nahisi watarudi zaidi na zaidi. Msimamo huu ukieendelea hadi 2015 mchuano wa Uchaguzi utakuwa ni kati ya CCM na CHADEMA. Bahati mbaya sana CCM inaporomoka wakati CHADEMA inapanda kwa nguvu ya kutosha. Labda hapo baadaye yaje mengine.


  Mbinu nzuri ya kuizuiya CHADEMA isiwe na kasi ya kubwa ni kuongeza nguvu ya Vyama vingine vya siasa ili ikifika 2015, Mchuano usiwe ni CCM v/s CHADEMA. Katika uteuzi huu sasa naona mbinu ya makusudi kabisa ya kulazimisha NCCR nayo ipate nguvu. Sijui kama ni zoezi la manufaa maana sioni kama Mbatia ni mtu awezaye kuvuta mpiga kura au hata kuongeza ufanisi wa NCCR yenyewe.


  Nadhani, kwa upande wa Rais Kikwete Mbinu nzuri ingekuwa ni kumuteua Mwana CHADEMA kuwa mbunge au hata Waziri (kama akikubali) ili kupunguza uadui. Ukisha punguza uadui inakuwa vigumu kushambuliwa na CHADEMA tena, Lakini kwa hilo la mbatia, it is a washout.
   
Loading...