Jela miaka 30 kwa wizi wa nazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jela miaka 30 kwa wizi wa nazi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 26, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280

  Jela miaka 30 kwa wizi wa nazi


  Imeandikwa na Kennedy Kisula, Lindi; Tarehe: 26th January 2011 @ 06:18

  MKAZI wa kijiji cha Kiwalala wilayani Lindi mkoani hapa, Salumu Ally (25) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 baada ya kuthibitika kufanya kosa la unyan'ganyi wa nazi kwa kutumia silaha.

  Hukumu hiyo ilisomwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Dunstan Ndunguru jana, baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili.

  Awali Wakili wa Serikali, Mwahija Hamad alisema mshitakiwa Salumu Ali mkazi wa kiwalala alifikishwa mahakamani Octoba, 10 mwaka jana na kupatikana na hatia ya kumjeruhi kwa kutumia silaha, Somoe Issa (42).

  Alidai mshitakiwa alimjeruhi Issa Septemba, 26 mwaka jana saa nane mchana kwa kutumia kisu sehemu za paja, shingoni na usoni.

  Hamadi alidai baada ya hapo mshitakiwa alimbinya Issa sehemu za shingoni mpaka alipoteza fahamu kutoka saa 8.00 mchana mpaka saa 2.00 usiku alipozinduka.

  Baada ya hapo mshitakiwa anadaiwa alichukua nazi 25 shambani mwa mlalamikaji baada ya kudhani kuwa alishafariki lakini wananchi walitoa taarifa kituo kidogo cha Polisi na msako ulianza na baadaye mshitakiwa alikamatwa.

  Naye Hakimu Ndunguru alisema Mahakama inamtia hatiani kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha na adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanataka kutenda kosa kama hilo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  Who said the aw was ass knew what he was talking about.......................
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  In this one I can only say,

  The Prosecutor is insane and the Magistrate is mad. This should have been a charge of attempted murder and not theft.

  If you read between lines there is no theft ( legally speaking) the intention was to kill, the act of taking the coconuts came when he thoght that the guy was dead. He had no premeditated mind of stealing.
   
 4. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  hii kali.
  Sasa mtu kama Liumba wa benki kuu na mabilioni alioiba kachukua mvua mbili tu!
  Chenge kaua and he's free.
  Mramba na Yona soon watakua huru.
  Rage kaiba na kaachiwa na sasa mbunge.
  Jamaa eti nazi sijui kaiba hayo madafu kapigwa mvua 30......nasikia kizunguzungu wangemwachia aende zake tu:coffee:
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  We should not just focus on NAZI as NAZI....THE Law regarding robbery with violence imposes a mandatory minimum jail term of 30 years regardless of the value of the property...hata ingekuwa pipi ya senti 5!..Kinachojalisha uzito wa adhabu ni huko kutumia nguvu..maana hiyo nguvu igeweza kusababisha kupoteza maisha.

  Mnaoshangaa adhabu hebu jiulizeni kama mtu "anaiba nazi" kwanini atumie nguvu kama hiyo nazi haina thamani?
   
 6. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  What about the mandatory minimum sentence for manslaughter?
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Manslaughter na robbery with violence ni makosa mawili tofauti...ingredients za kuthibitisha kosa ni tofauti na hata adhabu ya kosa inabidi iwe tofauti.Kwa vile mwizi wa nazi aliyetumia nguvu hajasababisha kifo kwa bahati mbaya huwezi ku substitute tu kienyeji . na kufanya manslaughter ili ati umpatie adhabu ndogo!
  Kila kosa la jinai lina sehemu mbili 1. Nia ya kutenda kosa ( mens rea) na 2. kitendo ( actus reus)..
  Nia ya kuiba kwa kutumia nguvu na kusababisha kifo kwa bahati mbaya ni tofauti.Manslaughter unaweza kufungwa hata mwezi kwa maana hukukusudia kutoa roho ya mtu.Kwenda kuiba kisha ukatumia nguvu ina maana una nia mbaya ya kudhulumu mali ya mtu na hapo hapo kumdhuru hata ikibidi umtoe roho..haya ni maelezo mepesi ya kusaidia kuona tofauti...
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ndio maana tunaomba katiba mpya matukio kama haya ni ya kionevu kabisa mafisadi wanaachwa wezi wa nazi wanakamatwa
   
 9. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nimekuelewa na nakubaliana na wewe. Still naona kuna double standards kubwa when it comes to carrying out a mandatory sentence kwa makosa mbalimbali.
  No wonder mtu kama Vladmir Putin hana subira hata kidogo ktk maamuzi ya kisheria kama haya. Ama ndio maana nchi kama China ukikutwa na hatia kwenye grand corruption unakula risasi, mwisho wa habari.
  Huyu mwizi wa nazi angefungwa kule China, lakini Liyumba saa hizi angekuwa marehemu
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  WOS, my concern was not nazi as nazi, kindly read the story slow line after line. Unakaba mtu mpaka unadhania amekufa, yule uliyemkaba yuu mahututi kwa masaa zaidi ya nane. Baada ya kuona umeaccomplish ( mistakenly though) unachotaka ndio unaenda kuchukua nazi.

  Ukiangalia mlolongo mzima intention haikuwa kuchukua nazi intention ilikuwa ni kuua, ndio maana nikasema hapo kama prosecutor angekuwa na proper legal mind angemcharge yule bwana na attempted murder na wala sio robbery with violence.

  Robbery with violence unaanza kuonyesha dhamira ya kuchukua akikataa ndio unatumia nguvu, ona defination yake kisheria:

  Any person who steals anything and, at or immediately before or immediately after the time of stealing it, uses or threatens to use actual violence to any person or property in order to obtain or retain the thing stolen or to prevent or overcome resistance to its being stolen or retained is guilty of robbery.

  Chukulia mfano huyo mtuhumiwa angekuwa na bastola alafu aitumie kwa mwenye mali na mwenye mali awe ameumia vibaya na amedhaniwa amekufa wakati kiukweli hajafa na jamaa anachukua nazi na kuondoka unadhani angeshtakiwa kwa kosa la wizi wa kutumia nguvu nadhani angeshtakiwa kwa attempted robbery.

  Ndio maana nasema prosecutor bure kabisa.
   
Loading...