Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Peter Makala alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi 4, mwaka huu, Saa 5:00 usiku.
Aliendelea kudai kuwa baada ya mshitakiwa kutekeleza azma yake alitaka kukimbia, lakini raia wema walimkamata na kumfikisha polisi.
Kibondo. Mahakama ya Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma, imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkimbizi kutoka Kongo, Charles Godfrey (22) anayeishi katika kambi ya wakimbizi ya Nduta kwa kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 15.
Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Peter Makala alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi 4, mwaka huu, Saa 5:00 usiku.
Aliendelea kudai kuwa baada ya mshitakiwa kutekeleza azma yake alitaka kukimbia, lakini raia wema walimkamata na kumfikisha polisi.
Baada ya kusomewa mashtaka, Hakimu wa Mahakama hiyo, Erick Marleye alimtaka mshtakiwa ajitetee, aliiomba mahakama imwonee huruma kwa kile alichodai kuwa ana watoto wadogo wanaomtegemea.
Hata hivyo, Mahakama baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo bila kuacha shaka, ilimhukumu adhabu ya kifungo cha miaka 30 gerezani.
Hakimu Maeleye alisema adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia za kunyanyasa watoto kingono.
Chanzo: Mwananchi