Jela miaka 20 kwa kusafirisha wahamiaji haramu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo, imemuhukumu kifungo cha miaka 20jela au faini ya Tsh Milioni 20, Hamis Halfani Juma(25) mkazi wa Tanga Mjini baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu.

Aidha katika mahakama hiyo wahamiaji haramu 199 kutoka Ethiopia wamehukumiwa vifungo vya miaka miwili hadi mitatu jela au faini ya Milioni Moja kila mmoja kwa kosa la kuingia nchini bila kufuata utaratibu.

Aidha Thomas Maduma(50) anatuhumiwa kutumia pikipiki yake November 12 kusafirishwa wahamiaji haramu kutoka Tanga hadi Chalinze ambapo shauri lake uchunguzi unaendelea.
 
Kupata million 20 maana yake yauzwe mashamba na nyumba kadhaa kwa hizi familia zetu.

Kwenye kikao cha familia watajiuliza ni faida ipi wataipata baada ya kuuza hivyo vyote na wewe kuludi mtaani.

Maamuzi ya wajomba na baba mdogo ambao huwaga ya kikauzu watasema muacheni aende maana tulishasema sana.

Hapo ndio mchezo umeisha.
 
Back
Top Bottom