Jela kwa kumtusi Kikwete na Ridhiwani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
MKAZI wa mjini Moshi, Kyefa Joachim Makundi (33), amepandishwa kizimbani akikabiliwa na mashitaka ya kumtukana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Mbali na shitaka hilo, mshitakiwa huyo amesomewa shitaka lingine la kumtukana Ridhiwan Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze anayemaliza muda wake.

Mshitakiwa huyo amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya mkoa Kilimanjaro, Joachim Tiganga na kusomewa mashitaka hayo na wakili wa Serikali Kanda ya Moshi, Agatha Pima.

Wakili Pima amedai mahakamani kuwa Oktoba 17 mwaka huu katika baa ya Harambee iliyopo katikati ya mji wa Moshi, mshitakiwa alitumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Kikwete na mwanae Ridhiwan.

Ingawa matusi hayo hayakuandikwa kwenye hati ya mashitaka, lakini wakili Pima amedai kitendo hicho ni kinyume cha kifungu 89(1) (a) cha kanuni ya adhabu kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Chini ya kifungu hicho, mtu yeyote anayetumia lugha ya matusi, kuudhi, au kudhalilisha dhidi ya mtu mwingine katika hali ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani anatenda kosa la jinai.

Adhabu inayotolewa kwa mtu anayepatikana na hatia katika kosa hilo ni kifungo cha miezi sita jela.

Hata hivyo, mshitakiwa amekana shitaka hilo ambapo mahakama imesema dhamana ilikuwa wazi ikiwa mshitakiwa atakuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh1.5 milioni kila mmoja.

Chanzo: Michuzi
 
Afunzwe adabu kama ana hamu sana ya kutukana huyu mangi mnywa mbege na viroba amtukane baba na mama yake
 
Wakili Pima amedai mahakamani kuwa Oktoba 17 mwaka huu katika baa ya Harambee iliyopo katikati ya mji wa Moshi, mshitakiwa alitumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Kikwete na mwanae Ridhiwan.

Haya walevi chungeni midomo yenu mkiwa kwenye baa.Siku hizi karibu na uchaguzi kaa mbali na baa na kiroba! Vinaweza sababisha mdomo ukakosa breki ukajikuta mahakamani
 
Vipi kuhusu kampeni zinazo endelea maana pale mwanzo kuna Chama kilikuwa kina toa maneno ya KUUDHI na KUDHALILISHA juu ya mgombea wa chama kingine lakini hawajachukuliwa hatua yoyote. Au wao wapo juu ya hii sheria???
 
IBRAHIM MGAYA

Basi kama ni hivyo sawa Nape Nauye aliyepata Fundisho na Mungu mwenyewe analugha ya matusi sana mbona hakamatwi? hiyo sheria ni ya mangi pekee yakee. Mkapa alitukana wananchi Pumbavu na Malofa Yuko juu ya sheria? Ndiyo maana watu wanakasirika juu ya chama tawala na serikali yake
 
Last edited by a moderator:
wacheni uonevu wenu, nchi hii ni ya ajabu sana, kwani edward lowasa ametukanwa mara ngapi na hili jamaaa lililopata ajali? matusi mmeyasikia kwa kikwete na riziwani tuu?

kwanini sijasikia mtu kakamatwa kwaajili ya kumtukana kipenzi cha watanzania edward lowassa?
 
IBRAHIM MGAYA

Basi kama ni hivyo sawa Nape Nauye aliyepata Fundisho na Mungu mwenyewe analugha ya matusi sana mbona hakamatwi? hiyo sheria ni ya mangi pekee yakee. Mkapa alitukana wananchi Pumbavu na Malofa Yuko juu ya sheria? Ndiyo maana watu wanakasirika juu ya chama tawala na serikali yake

Siku hizi ulofa limekuwa tusi! Mbona nyerere amelitumia sana neno hilo na watu walikuwa wanacheka tu, aliwaita wajinga, makaburu, wapumbavu, malofa lakini malofa walikuwa wanacheka na kupiga makofi au tafsiri ya maneno imebadilika siku hizi?
 
Hata Lowassa labda ugonjwa alionao ni PIGO Kwa sababu ya wizi aliowafanyia WATANZANIA.Leo WATANZANIA WANALALA GIZA KWASABABU YAKE NA ROSTAM AZIZ
 
Last edited by a moderator:
Siku hizi ulofa limekuwa tusi! Mbona nyerere amelitumia sana neno hilo na watu walikuwa wanacheka tu, aliwaita wajinga, makaburu, wapumbavu, malofa lakini malofa walikuwa wanacheka na kupiga makofi au tafsiri ya maneno imebadilika siku hizi?

Kama wewe ukiitwa Lofa unachekelea basi ujue sio kila mtu anapenda hivyo.
 
Back
Top Bottom