Jela inapokuwa na manufaa kwa jamii

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,587
215,184
Kuna bwana mmoja Mtanzania ni fundi huko Ulaya. Ana kampuni yake ndogo na van la kazi. Huwa anaajiri cash in hand wengi kutoka Romania na Poland. Ifundi wa huyu bwana ni:

1. Fundi bomba, hutengeneza mabomba yaliyoharibika na pia kufunga mashine za kufulia.

2. Fundi umeme na gas, hutengeneza heaters na boilers hasa kipindi cha baridi huitwa hata usiku.

3. Brick layer, kama unahitaji kujenga conservatory au kupandisha ukuta wa fence.

Nilipata kumuuliza ujuzi huu aliupata wapi. Alinijibu aliingia Ulaya akiwa kijana na alipata matatizo yaliyopelekea kufungwa jela. Akiwa jela alijifunza ufundi wote huo.

Unasoma certificate, ukifaulu vizuri unaanza kufanya kazi. Nusu ya mshahara unapewa kama pocket money. Ukitaka kuendelea na diploma unaweza.

Yeye aliamua kusoma certificate ya vitu vitatu tofauti. Aliniambia kuwa mfungwa kumekuwa na mafanikio ambayo mtaani aingeyapata.

Nilitafakari jinsi jela inavyoweza kubadilisha maisha ya watu.
 
"Gereza sio kaburi hebu jikaze mtoto wa kiume,kulia lia sio vizuri unakufuru mswalie mtume,mwanao kaja kukuona unapaswa utulie,ana mengi ya kitaa tulia akusimulie,hapa ni mafunzoni so umekuja kujifunza,hapa sio kifungoni,usisikie ya wajinga eti jela ni jeraha......."

-Spack & Tundaman
Nipe ripoti.
 
Hata Tanzania hapa Kuna mtu namjua alifungwaga ila katoka na sahivi ni fundi viatu mzuri sana!
Yaani kiatu anakiunda mwanzo mwisho

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Ile miaka 18 ya kufunga mikanda baada ya vita ya Kagera. Jirani yetu kijijini kijana wao alifungwa Maweni Tanga. Yule bwana alitoka jela na ujuzi wa kutengebeza sabuni.

Enzi zile mnara wa mbuni unaupata kwa balozi wa nyumba kumi. Jamaa alitengeneza pesa mpaka kuwa pedeshee. Alikufa kwa ngoma enzi zile hakuna ARV’s.
 
Ile miaka 18 ya kufunga mikanda baada ya vita ya Kagera. Jirani yetu kijijini kijana wao alifungwa Maweni Tanga. Yule bwana alitoka jela na ujauzito wa kutengebeza sabuni.

jamaa alitoka jela na nini?!

Nna rafiki yangu mmoja alifungwa Brazil Miaka
Alipotoka aliamua kurudi bongo, jamaa ni mtaalam wa kujenga majiko na ku design "kitchens" hatari

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata hapa Tanzania watu wanatoka na ujuzi wa fani tofauti tofauti.
Inategemea umefungwa gereza lipi,kuna magereza ya Kilimo kama haya ya Mkoa wa Morogoro (Wami,Idete,Kiberege).
Mzee wangu alifungwa jela Ukonga ,mwishoni mwa miaka ya sitini alijifunza ufundi wa kushona nguo (cherehani) huko.
 
Wakupe hiyo fulsa uache kushinda jf tu

State agent
Kuna bwana mmoja Mtanzania ni fundi huko Ulaya. Ana kampuni yake ndogo na van la kazi. Huwa anaajiri cash in hand wengi kutoka Romania na Poland. Ifundi wa huyu bwana ni:

1. Fundi bomba, hutengeneza mabomba yaliyoharibika na pia kufunga mashine za kufulia.

2. Fundi umeme na gas, hutengeneza heaters na boilers hasa kipindi cha baridi huitwa hata usiku.

3. Brick layer, kama unahitaji kujenga conservatory au kupandisha ukuta wa fence.

Nilipata kumuuliza ujuzi huu aliupata wapi. Alinijibu aliingia Ulaya akiwa kijana na alipata matatizo yaliyopelekea kufungwa jela. Akiwa jela alijifunza ufundi wote huo.

Unasoma certificate, ukifaulu vizuri unaanza kufanya kazi. Nusu ya mshahara unapewa kama pocket money. Ukitaka kuendelea na diploma unaweza.

Yeye aliamua kusoma certificate ya vitu vitatu tofauti. Aliniambia kuwa mfungwa kumekuwa na mafanikio ambayo mtaani aingeyapata.

Nilitafakari jinsi jela inavyoweza kubadilisha maisha ya watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom