Jeffery Samson Mkuki: Msomi wa Chuo Kikuu anayehangaika kijijini bila ajira

Nadhani alikuwa na plan ya kupiga chini Ualimu ili ajaribu fani hii ya telecom.
Inasikitisha sana.Huyu jamaa Kama sikosei aliwahi ajiriwa kama mwl.wa Diploma ya Ualimu pale Singida.Wakati fulani tukiwa chuo alisha nambiaga hii story!!
 
JEOFREY SAMSON MKUKI KIJANA "MSOMI" WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ANAYEHANGAIKA KIJIJINI BILA AJIRA.

Alihitimu Elimu ya Chuo Kikuu (University Of Dodoma) Mwaka 2013 kisha akaelekea zake Dar Es Salaam kujitafutia Riziki na baadae akaamua kurudi Kijijini kwao alikozaliwa. Kule UDOM, Jeofrey alisomea (BSc.Telecommunications Engineering) na Vyeti vyake vyote kuanzia Kidato cha Nne hadi Chuo Kikuu anavyo huku Kijijini.

Kijana mwenzetu Jeofrey Samson Mkuki ni Mkazi wa Kitongoji cha Imiga, Kijiji cha Mkiwa, Kata ya Mkiwa, Wilaya ya Ikungi huko Mkoani Singida. Jeofrey Mkuki ni Yatima asiye na Wazazi wake wote wawili maana walishatangulia mbele za haki.

Wakati nafika Eneo anakoishi Jeofrey Mkuki huko Mkoani Singida, niliambatana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi anayeonekana Pichani upande wa kulia. Huko Kijijini, Jeofrey anaishi na Wadogo zake wawili ambao wanamtegemea na anajishughulisha na Vibarua vidogo vidogo ikiwemo kupakia Mizigo kwenye Magari na kuuza Mkaa karibu na Barabara Kuu ya Mwanza to Dar Es Salaam.

Kijana Jeofrey Mkuki ni Mtu mwenye Akili zake timamu na kwa mujibu wa Majirani zake na Viongozi wa Serikali wa Eneo anakoishi akiwemo Mheshimiwa Diwani wa Kata hiyo niliyeambata naye, wanadai hajawahi kupatwa na tatizo lolote la Kiafya, ingawa ukiutazama muonekano wake unaweza usiamini kama ni Kijana mwenye Elimu ya kiwango cha juu kiasi hiki.

Kwa mujibu wa maelezo yake yeye mwenyewe, Jeofrey anasema, "niliamua kurudi huku Kijijini kwa sababu, wadogo zangu hawa bado ni wadogo na kama unavyoona Wazazi wote hawapo, iliniuma sana nikaamua nirudi huku. Huko Mijini nilipata Ajira kwenye Mashirika ya Mambo ya Mawasiliano na nilikuwa nazunguka Mikoani, lakini kutokana na hii familia unayoiona, ndio hivyo tena Mheshimiwa, lakini natamani Siku moja niwe tofauti na hivi niliyake. Alieleza Mkuki.

Kijana Jeofrey Mkuki aliwahi kufundisha kama Mwalimu wa kujitolea wa Masomo ya Sayansi kama vile Basic Mathematics na Physics katika Shule ya Sekondari Senge maarufu kama Chifu-Senge iliyopo Singida Mjini Mkoani Singida. Nilipomuuliza kwa nini asiendelee kufundisha, Jeofrey alisema ni Maisha tu yamemvurugia mambo yake na akafikia hatua hii ingawa bado ana wazo la aina hiyo.

Aidha, Jeofrey Mkuki pia ni Mtaalam mzuri wa Computer na wakati nafika Kijijini kwao anakoishi huko Mkoani Singida, nimemkuta akiwa na Computer yake aina ya Laptop HP anayotumia kwa ajili ya Shughuli zake za binafsi.

Kwa Mawasiliano zaidi na Jeofrey Mkuki wa Singida unaweza kupiga Simu yake ya Mkononi 0746440462 au Email: mkukijs@gmail.com

Au unaweza kuwasiliana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi 0745865904.

Francis M. Garatwa,
Kiongozi wa Oparesheni ya Chama,
Jimbo la Singida Mashariki.
Ikungi, Singida - Tanzania.
12 June, 2019.

View attachment 1125671

View attachment 1125673

View attachment 1125675
[/QUOTEHapo kwenye akili timamu ndio Nina wasiwasi. Haiwezekani uwe na kazi halafu uache urudi kijijini kukaa na wadogo zako. Option nzuri ingekuwa kuwaleta mjini ulipopanga na kijijini ukafunga.
maamuzi yake ya kuacha kazi are more than wanting
 
Hapo kwenye akili timamu ndio Nina wasiwasi. Haiwezekani uwe na kazi halafu uache urudi kijijini kukaa na wadogo zako. Option nzuri ingekuwa kuwaleta mjini ulipopanga na kijijini ukafunga.
maamuzi yake ya kuacha kazi are more than wanting
 
Wanafunzi waliofungua UDOM walipata elimu ya hovyo kabisa
Hakuna kitu kama hicho kijana, mie no mmoja wao pioneers, niliosoma nao wengine ni Managers kwenye mashirika ya UN, regional administrative secretary, bankers, administrators wa NGOS, Sales Officers, usiishi kwa kukariri
 
Hakuna kitu kama hicho kijana, mie no mmoja wao pioneers, niliosoma nao wengine ni Managers kwenye mashirika ya UN, regional administrative secretary, bankers, administrators wa NGOS, Sales Officers, usiishi kwa kukariri
Kupata poor education haimaanishi kukosa kazi ,unatakiwa ujue kitu kama hichoo
 
Hakuna kitu kama hicho kijana, mie no mmoja wao pioneers, niliosoma nao wengine ni Managers kwenye mashirika ya UN, regional administrative secretary, bankers, administrators wa NGOS, Sales Officers, usiishi kwa kukariri
Ulisoma course gani?
 
Huyu kijana nimeona twitter watu wamepost kasoma Telecom eng lakini yupo bush hii inatoa picha gani? wengine wanadai pombe zimemuathiri
20190616_083446.jpeg
 
Back
Top Bottom