Jeffery Samson Mkuki: Msomi wa Chuo Kikuu anayehangaika kijijini bila ajira

Mtailaumu serikali lakini ukumbuke wafanyakazi wote wa serikali hawafiki laki saba, ukumbuke tupo watanzania zaidi ya milioni 55 na zaidi kila siku watu wanasoma hivo lazima tubadili mitazamo yetu kwanza na kubadili mfumo wa elimu yetu ili tusonge mbele zaidi maana duniani kote ni sekta binafsi ndio imeajiri watu wengi kuliko sekta ya umma hivo tupambane ili kuipigania sekta binafsi isianguke izidi kukua na kuleta mapinduzi kwenye maisha ya vijana wetu pia.
 
Kwema Mzee baba. Shuta shuta mwendo wa ngiri, hakuna kulala, ukipepesa kidogo wanakomba mboga na vyombo wanakuachia uoshe.

Si unaona vijana wanavyopigika za ugoko huko?
Si walikuwa wanasoma kwa kukariri

Ndomana wengine sisi ni viraka

Ova
 
Si walikuwa wanasoma kwa kukariri

Ndomana wengine sisi ni viraka

Ova
Ujanja mwingi, mbele kiza. Haraka haraka haina baraka. Mwendapole hajikwai.

Maisha ya kukariri hayajawahi kumuacha mtu salama.

Kuna masela hata six hawajashika na wanakula utamu wa maisha kama warina asali!

Huku tunatengeneza jeshi la mainjinia wasioweza kupata ajira, tena kwa mikopo mikubwa tu.
 
Mi naona huyo diwani ni msaada tosha, hebu amfanyie mpango basii hata awe mwenyekiti wa kijiji hapo senge village.
Kuna wahitimu wengine hawapati fursa hata ya kukutana na mjumbe wa nyumba kumi sembuse diwani.
 
Ujanja mwingi, mbele kiza. Haraka haraka haina baraka. Mwendapole hajikwai.

Maisha ya kukariri hayajawahi kumuacha mtu salama.

Kuna masela hata six hawajashika na wanakula utamu wa maisha kama warina asali!

Huku tunatengeneza jeshi la mainjinia wasioweza kupata ajira, tena kwa mikopo mikubwa tu.
Duh hii mistari hatari

Ova
 
Amesema alikuwa ameajiriwa na makampuni ya mawasiliano, akaacha ili kuja kukaa na wadogo zake. Sasa hapo anawasaidia kuliko kama ambavyo angewasaidia alipokuwa na kazi yake? Kama atakuwa mzima basi anakuzidi wewe!
Haya bwana.
 
Kosa lako mama Ndalichako,kuwapa elimu isiyowasaidia wahitimu...😥😥😥😥😥
Elimu yetu ina mushikeli sana. Iko kwenye kupata ufaulu mkubwa kuliko kuelimika. Hivi telecom engineer atakosaje kitu cha kufanya? Hata kufundisha hesabu na physics basi. Yaani game limekataa kabisa mpaka kurudi nyuma mazima?
 
Mpwa wangu alifaulu kwenda kidato cha V, shughuli ya kununua godoro, jembe, ndoo, sanduku ilikuwa mtihani. Aliwabia ndugu waache tu. aliamua kuwa mkulima.

Sasa hivi ana nyumba ya vyumba vitatu vya kulala ilijengwa kwa matofali ya kuchoma na kuezekwa kwa mabati, Ana mbuzi 100, shamba la ana panda mahindi, mabamia yanampatia 10,000 kila siku asubuhi.
inspirational huyu ni tajiri kuliko wenye masters kibao
 
JEOFREY SAMSON MKUKI KIJANA "MSOMI" WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ANAYEHANGAIKA KIJIJINI BILA AJIRA.

Alihitimu Elimu ya Chuo Kikuu (University Of Dodoma) Mwaka 2013 kisha akaelekea zake Dar Es Salaam kujitafutia Riziki na baadae akaamua kurudi Kijijini kwao alikozaliwa. Kule UDOM, Jeofrey alisomea (BSc.Telecommunications Engineering) na Vyeti vyake vyote kuanzia Kidato cha Nne hadi Chuo Kikuu anavyo huku Kijijini.

Kijana mwenzetu Jeofrey Samson Mkuki ni Mkazi wa Kitongoji cha Imiga, Kijiji cha Mkiwa, Kata ya Mkiwa, Wilaya ya Ikungi huko Mkoani Singida. Jeofrey Mkuki ni Yatima asiye na Wazazi wake wote wawili maana walishatangulia mbele za haki.

Wakati nafika Eneo anakoishi Jeofrey Mkuki huko Mkoani Singida, niliambatana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi anayeonekana Pichani upande wa kulia. Huko Kijijini, Jeofrey anaishi na Wadogo zake wawili ambao wanamtegemea na anajishughulisha na Vibarua vidogo vidogo ikiwemo kupakia Mizigo kwenye Magari na kuuza Mkaa karibu na Barabara Kuu ya Mwanza to Dar Es Salaam.

Kijana Jeofrey Mkuki ni Mtu mwenye Akili zake timamu na kwa mujibu wa Majirani zake na Viongozi wa Serikali wa Eneo anakoishi akiwemo Mheshimiwa Diwani wa Kata hiyo niliyeambata naye, wanadai hajawahi kupatwa na tatizo lolote la Kiafya, ingawa ukiutazama muonekano wake unaweza usiamini kama ni Kijana mwenye Elimu ya kiwango cha juu kiasi hiki.

Kwa mujibu wa maelezo yake yeye mwenyewe, Jeofrey anasema, "niliamua kurudi huku Kijijini kwa sababu, wadogo zangu hawa bado ni wadogo na kama unavyoona Wazazi wote hawapo, iliniuma sana nikaamua nirudi huku. Huko Mijini nilipata Ajira kwenye Mashirika ya Mambo ya Mawasiliano na nilikuwa nazunguka Mikoani, lakini kutokana na hii familia unayoiona, ndio hivyo tena Mheshimiwa, lakini natamani Siku moja niwe tofauti na hivi niliyake. Alieleza Mkuki.

Kijana Jeofrey Mkuki aliwahi kufundisha kama Mwalimu wa kujitolea wa Masomo ya Sayansi kama vile Basic Mathematics na Physics katika Shule ya Sekondari Senge maarufu kama Chifu-Senge iliyopo Singida Mjini Mkoani Singida. Nilipomuuliza kwa nini asiendelee kufundisha, Jeofrey alisema ni Maisha tu yamemvurugia mambo yake na akafikia hatua hii ingawa bado ana wazo la aina hiyo.

Aidha, Jeofrey Mkuki pia ni Mtaalam mzuri wa Computer na wakati nafika Kijijini kwao anakoishi huko Mkoani Singida, nimemkuta akiwa na Computer yake aina ya Laptop HP anayotumia kwa ajili ya Shughuli zake za binafsi.

Kwa Mawasiliano zaidi na Jeofrey Mkuki wa Singida unaweza kupiga Simu yake ya Mkononi 0746440462 au Email: mkukijs@gmail.com

Au unaweza kuwasiliana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi 0745865904.

Francis M. Garatwa,
Kiongozi wa Oparesheni ya Chama,
Jimbo la Singida Mashariki.
Ikungi, Singida - Tanzania.
12 June, 2019.

View attachment 1125671

View attachment 1125673

View attachment 1125675
Alafu bodi hapo bado wanamdai,dah life hili halieleweki kabisa.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom