Jeffery Samson Mkuki: Msomi wa Chuo Kikuu anayehangaika kijijini bila ajira

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,564
215,040
JEOFREY SAMSON MKUKI KIJANA "MSOMI" WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ANAYEHANGAIKA KIJIJINI BILA AJIRA.

Alihitimu Elimu ya Chuo Kikuu (University Of Dodoma) Mwaka 2013 kisha akaelekea zake Dar Es Salaam kujitafutia Riziki na baadae akaamua kurudi Kijijini kwao alikozaliwa. Kule UDOM, Jeofrey alisomea (BSc.Telecommunications Engineering) na Vyeti vyake vyote kuanzia Kidato cha Nne hadi Chuo Kikuu anavyo huku Kijijini.

Kijana mwenzetu Jeofrey Samson Mkuki ni Mkazi wa Kitongoji cha Imiga, Kijiji cha Mkiwa, Kata ya Mkiwa, Wilaya ya Ikungi huko Mkoani Singida. Jeofrey Mkuki ni Yatima asiye na Wazazi wake wote wawili maana walishatangulia mbele za haki.

Wakati nafika Eneo anakoishi Jeofrey Mkuki huko Mkoani Singida, niliambatana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi anayeonekana Pichani upande wa kulia. Huko Kijijini, Jeofrey anaishi na Wadogo zake wawili ambao wanamtegemea na anajishughulisha na Vibarua vidogo vidogo ikiwemo kupakia Mizigo kwenye Magari na kuuza Mkaa karibu na Barabara Kuu ya Mwanza to Dar Es Salaam.

Kijana Jeofrey Mkuki ni Mtu mwenye Akili zake timamu na kwa mujibu wa Majirani zake na Viongozi wa Serikali wa Eneo anakoishi akiwemo Mheshimiwa Diwani wa Kata hiyo niliyeambata naye, wanadai hajawahi kupatwa na tatizo lolote la Kiafya, ingawa ukiutazama muonekano wake unaweza usiamini kama ni Kijana mwenye Elimu ya kiwango cha juu kiasi hiki.

Kwa mujibu wa maelezo yake yeye mwenyewe, Jeofrey anasema, "niliamua kurudi huku Kijijini kwa sababu, wadogo zangu hawa bado ni wadogo na kama unavyoona Wazazi wote hawapo, iliniuma sana nikaamua nirudi huku. Huko Mijini nilipata Ajira kwenye Mashirika ya Mambo ya Mawasiliano na nilikuwa nazunguka Mikoani, lakini kutokana na hii familia unayoiona, ndio hivyo tena Mheshimiwa, lakini natamani Siku moja niwe tofauti na hivi niliyake. Alieleza Mkuki.

Kijana Jeofrey Mkuki aliwahi kufundisha kama Mwalimu wa kujitolea wa Masomo ya Sayansi kama vile Basic Mathematics na Physics katika Shule ya Sekondari Senge maarufu kama Chifu-Senge iliyopo Singida Mjini Mkoani Singida. Nilipomuuliza kwa nini asiendelee kufundisha, Jeofrey alisema ni Maisha tu yamemvurugia mambo yake na akafikia hatua hii ingawa bado ana wazo la aina hiyo.

Aidha, Jeofrey Mkuki pia ni Mtaalam mzuri wa Computer na wakati nafika Kijijini kwao anakoishi huko Mkoani Singida, nimemkuta akiwa na Computer yake aina ya Laptop HP anayotumia kwa ajili ya Shughuli zake za binafsi.

Kwa Mawasiliano zaidi na Jeofrey Mkuki wa Singida unaweza kupiga Simu yake ya Mkononi 0746440462 au Email: mkukijs@gmail.com

Au unaweza kuwasiliana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi 0745865904.

Francis M. Garatwa,
Kiongozi wa Oparesheni ya Chama,
Jimbo la Singida Mashariki.
Ikungi, Singida - Tanzania.
12 June, 2019.

1125671


1125673


1125675
 
Ajira ni janga la dunia. Ukisoma huku unategemea ajira tayari ushajiandaa kufeli

ni janga la dunia kwa hio tuwe comfortable tuache yanayoendelea kisa ni janga la dunia???embu tuweke comparison kati ya nchi na nchi?..lol....Elimu yetu haiwaandai watu kujiajiri....utajiajiri vipi wakati umekariri ma theories kwa lugha ya kigeni??? ajira ni tatizo..lakini relevant education inaweza ku offset tatizo la ajira.
 
Mpwa wangu alifaulu kwenda kidato cha V, shughuli ya kununua godoro, jembe, ndoo, sanduku ilikuwa mtihani. Aliwambia ndugu waache tu. aliamua kuwa mkulima.

Sasa hivi ana nyumba ya vyumba vitatu vya kulala ilijengwa kwa matofali ya kuchoma na kuezekwa kwa mabati, Ana mbuzi 100, shamba anapanda mahindi, mabamia yanampatia 10,000 kila siku asubuhi.
 
ni janga la dunia kwa hio tuwe comfortable tuache yanayoendelea kisa ni janga la dunia???embu tuweke comparison kati ya nchi na nchi?..lol....Elimu yetu haiwaandai watu kujiajiri....utajiajiri vipi wakati umekariri ma theories kwa lugha ya kigeni??? ajira ni tatizo..lakini relevant education inaweza ku offset tatizo la ajira.
Hakuna aliekwambia uwe comfortable. Jiongeze,ajira hamna ukiendelea kusubiri utateseka. Hio hio elimu isioandaa kujiajiri wengine wanajiajiri
 
ni janga la dunia kwa hio tuwe comfortable tuache yanayoendelea kisa ni janga la dunia???embu tuweke comparison kati ya nchi na nchi?..lol....Elimu yetu haiwaandai watu kujiajiri....utajiajiri vipi wakati umekariri ma theories kwa lugha ya kigeni??? ajira ni tatizo..lakini relevant education inaweza ku offset tatizo la ajira.
Mpwa wangu alifaulu kwenda kidato cha V, shughuli ya kununua godoro, jembe, ndoo, sanduku ilikuwa mtihani. Alimwambia ndugu wachezaji tu. aliamua kuwa mkulima.

Sasa hivi ana nyumba ya vyumba vitatu vya kulala ilijengwa kwa matofali ya kuchoma na kuezekwa kwa mabati, Ana mbuzi 100, shamba la ana panda mahindi, mabamiavyanampatia 10,000 kila siku asubuhi.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom