Jeff Horn Boxer ingawa amemtandika Pacquiao lakini uwezo wake ni mdogo sana kucheza na Mayweather

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
18,208
22,789
Bondia Jeff Horn jana alimchakaza vilivyo Man Pacquaiao a.k.a mzee wa ngumi cherehani ,baada ya pambano akatamba kuwa anataka pambano na bondia Floyd Mayweather .

Lakini ukiangalia haraka haraka jinsi anavyopigana huyu jamaa ,anavyorusha ngumi zake kamwe hawezi kufikisha ngumi hata 50 usoni kwa Floyd .

Jana alim bahatisha Pacquiao kwa sababu Pac defence yake ni dhaifu sana ila ingekuwa ni Floyd aisee huyu dogo asingeambulia chochote kwa sababu ngumu nyingi alizopigwa Pac ni za kijinga sana ,yaani kwa kifupi Pac si mzuri kwenye ukwepaji wa makonde

Nikawa na Imagine Pac angekuwa ni Floyd na kwa jinsi jamaa anavyorusha ngumi na kuacha uso wazi ,aisee angedokolewa mara nyingi kichizi

Floyd ana tabia ya kukwepa ngumi na muda huo huo anakurushia konde la kushtukiza hivyo basi kwa jinsi anavyopigana huyu Jeff aisee akifanikiwa kukubaliwa na Floyd atapigwa kiurahisi sana .

Screenshot_2017-07-02-12-51-41_1.jpg
Screenshot_2017-07-02-12-55-40_1.jpg
 
Kumbuka age factor, Moneyman anaweza kupigwa tu kirahisi na huyu dogo Horn, usijeshangaa!
 
Kumbuka age factor, Moneyman anaweza kupigwa tu kirahisi na huyu dogo Horn, usijeshangaa!
Hawezi ndugu ,nipo radhi kuweka dau hata 5Million

Kwa jinsi anavyopigana huyu mdau hana uwezo hata chembe wa kumkalisha Floyd
 
Paq man ajikite kwenye siasa tu huko kwao aje kugombea uraisi,gloves atundike tu!!

Awe mjanja kama Vital Klitchko,ngumi mara nyingi ukitaka udumu na heshima yako inatakiwa uangalie nyakati.Pac alitakiwa pambano lake la mwisho liwe lile alilocheza na Mayweather atundike gloves afanye mengine asiwe kama Tyson kwenda kupigwa na mtoto mdogo Lewis huku Tyson heshima ikishuka Lewis heshima ikapanda pale pale Lewis akatangaza kustaafu boxing.hata Mayweather mwenyewe baada ya pambano na Pac japo hela anaitaka ila anaenda macho juu juu kama joka lenye makengeza kuchagua wa kucheza nae kama ikitokea akapatikana kwa7bu ya kuilinda title yake aliyoitengeneza muda mrefu maana ana miaka40 sasa ikitokea akapigwa atapata wapi mwengine wa kumtusua kama akipigwa na umri huo?
 
Pac ameniangusha sana@Hans inabidi afanye mazoezi sana kuna tatzo mahali chief

Ova
Pac hii gemu sijui alikuwa hajajiandaa?

Yaani kapigwa kirahisi sana na jamaa kama atakubaliwa na floyd halafu akawa anapigana kama alivyopigana na pac ,jamaa atapigwa na Floyd kirahisi sana
 
Awe mjanja kama Vital Klitchko,ngumi mara nyingi ukitaka udumu na heshima yako inatakiwa uangalie nyakati.Pac alitakiwa pambano lake la mwisho liwe lile alilocheza na Mayweather atundike gloves afanye mengine asiwe kama Tyson kwenda kupigwa na mtoto mdogo Lewis huku Tyson heshima ikishuka Lewis heshima ikapanda pale pale Lewis akatangaza kustaafu boxing.hata Mayweather mwenyewe baada ya pambano na Pac japo hela anaitaka ila anaenda macho juu juu kama joka lenye makengeza kuchagua wa kucheza nae kama ikitokea akapatikana kwa7bu ya kuilinda title yake aliyoitengeneza muda mrefu maana ana miaka40 sasa ikitokea akapigwa atapata wapi mwengine wa kumtusua kama akipigwa na umri huo?
Una akili sana kjana umenena
 
Itamchukua muda sana kupambana na mayweather.
Kwani mayweather anatarajia mwezi wa 8 kudundana na jamaa mwingine.
Conor MCGregor anaitwa.

Ila hilo ni suala la uamuzi tu ,kama akikubaliwa hata mwezi October pambano linaweza kuwekwa

Mbona Pac mwezi wa nne alichapana na Timothy Bradley na jana kachapana na huyo Hornet ,hivyo ni suala la uamuzi tu.
 
Connor sawa kabisa,
Kumbe inawezekana ok
Pia Pac anaweza kuomba rematch tena kama alipoulizwa akasema why not
 
mbona ni mpiganaji mzuri tu si mbaya ila kwenye Mpambano alikua anatumia kumpiga paq kichwa tena mara2 huku refaree akikausha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom