Jeff Bezos arudi kwenye nafasi yake, Elon Musk Apoteza $14bn kwa siku moja

Sasa kama faida yake haijulikani, na utajiri wa huyo mtu ni shares anazomiliki kwenye kampuni zake, unajua PR ya kampuni ikitokea ikachafuliwa na watu wakakosa imani na hiyo miradi yake utajiri wake utaporomoka kwa kasi isiyo ya kawaida??

Wewe ni bidhaa gani ya huyo Kaburu Elon unaitumia?? Unakijua kinachoendelea WhatsApp sasa?? Matajiri wa kweli ni akina Carlos Slim akina Ortega
Kutumia bidhaa ya kampuni husika mantiki yako nini Apple ndio kampuni yenye Value kubwa mbona sijawai tumia kitu chao chochote, Dangote Group mbona sijawai tumia kitu chao,
 
Kwenye huo utajiri wa Hisa faida wanapataje sasa Kwa staili hiyo Donald Trump Kwa majengo aliyokuwa nayo anaweza kuwa tajiri mkubwa Sana Trump towers . Sasa Kwa mfano Elon musk faida si anapata akiuza magari ya umeme au inakuwaje
Mkuu Real Estate ni Industry Kama zilovyo zingine Trump Biashara yake kubwa Real Estate, kama waarabu matajiri visima vya mafuta, ila kuna kitu kinaitwa Software hiyo ni Asset yenye thamani kwasasa duniani kote Ghorofa ni furushi la mchanga tu.

Trump alivyo na maghoropha ndivyo Musk ana Gigafactory kibao za Tesla Motors jaribu kufuatilia YouTube ila mbali na kuwa na Gigafactories ana Market Cap kubwa ambayo anaweza iweka kwenye Liquidity kwa dakika na akanunua Ghorofa zote za Trump na kubaki na Change, Share zake na Gigafactory zake.

Dunia sio kumiliki mafutushi ya tofari now fuatilia lile furushi la michanga la Michael Jackson limeuzwa kwa hasara tu wakati ni bonge la furushi.
 
Kuikweli kabisa..utajiri wa hisa ni tofauti kabisa na utajiri wetu sisi waafrika.

Dangote kwa asset na cash aliyonayo, anaweza amawa hata ndani ya kumi bora ya matajiri wa Dunia.

Utajiri wa Elon na Jeff uko tied na ongezeko la thamani a hisa kwenye kampuni wanazoziongoza. Siutajiri wa cash...

Hisa its a tricky business.....zinapanda na kushuka muda wowote based on speculations tu. Na wakati mwingine ni ngumu kubadili hisa kuwa cash. Maana ili upate cash unayoitaji unapaswa kuuza hisa zako, na mtu kama Elon musk akisema auze hisa zake hata asilimia moja tu, italeta tetemeko kubwa kwenye thamani ya hisa zake. Investors watahofia kununua hisa maana wanahisi hata CEO wao hana confidence na soko la hisa za kampuni ndo maana anauza zake...so kila mtu atataka kuuza hisa zake...na mwisho wa siku thamani ya hisa zitaporomoka.

So unaweza ukawa tajiri wa hisa na ukafa na njaa ndani ...tumeona wamiliki wa hisa za vodacom. Kuna watu wanamiliki hisa za million 20, na wamekwama kuzibadili kuwa cash..maana hakuna anaezitaka. Na wakati mwingine thaman yake inashuka, unakuta hisa ya 1000 sasa ni 500 tu..ukiuza unapata nusu tu ya kile ulichowekeza....

Huu utajiri wa hawa jamaa ni utajiri wa mapicha picha.....mwache dangote...na akina Ambani wa india. Hawa jamaa wana mawe kweli kweli...sio hisa tunazochezewa nazo akili.
Kumbuka ELon musk ana viwanda vya kutengeneza magari ya umeme Germany, china , USA Kwa mtazamo wangu ni ngumu kufananisha Elon Musk na Dangote pia Jeff Bezoes na kampuni yake ya Amazon anasupply kupitia online marketing anatengeneza faida kuwazidi Akina Dangote . Pia Google yenye wafanyakazi zaidi ya laki mbili nafikiri inatengeneza faida kubwa Sana
 
Kama ninrahisi kuuza hisa kiasi icho waulize wenye hisa za voda au precision watakupa mrejesho. Kuna walionunua hisa kwa 1000/-, leo wanauza kwa 400/- na bado hazina wanunuzi.

Kwa tesla inaweza ikawa tofauti, kwa vile demand ya hisa zake sokoni ziko juu. Hisa moja ya tesla leo ni $854. Ila kitendo cha elon ambae ni co founder na CEO wa tesla leo kuamua kuuza only 5% ya hisa zake...huu uwamuzi utawashtua sana wanunuzi na kujiuliza either Elon mwenyewe haoni future ya kampuni au kuna shida gani. Itapoteza confidence za investor na thamani ya hisa inaweza ikashuka ikafika hata $100 kwa hisa...

Ni kama bongo tu ilivyokuwa, yaani Rostam share holder mkubwa wa Vodacom anauza hisa zake zote, wewe unaenda kununua..bila kujiuliza kwann largest shareholder ameamua kuachana na hii biashara...ameona nini, anataarifa gani ambazo zimempelekea kufanya haya maamuzi ambazo wewe huku chini huna.

Kwa wenzetu uwamuzi wa Rostam tu ungeporomosha sana thamani ya hisa za kampuni. Ila kwetu ilikuwa tofauti. Ndo hiki kinatokea...hisa za voda haziuziki.
mkuu tumekuelewa vizur
 
😂 😂 Mzee kwani ndio umeandika nini hapa kwani share sindio Liquidity yenyewe kwani unavyofikiri dhumuni la kampuni kuuza share zake Public ni nini sikupata Liquidity Mtaji mkubwa sindio Liquidity yenyewe hiyo

Unaandika manini Bob
Ngoja nikwambie kitu....trading inayofanyika kwenye stock exchange ni ya madalali tu..mimi na wewe...mimi mwenye hisa CRDB, nakuuzia wewe ambae huna. Nakupa hisa, wewe unanipa pesa. Pesa unayonipa haiingii CRDB. inaingia kwangu.

Mimi naweza nikawa nimenunua hisa za CRDB kwa shilingi 1000. Hizi hisa nimenunua moja kwa moja kwa CRDB wakati wanaregister kwenye soko la hisa.

Baada ya hapo, pale DSE ni mimi ma wewe ndio tunakuwa tunauziana. Natafuta dalali anitaftie mteja anunue hisa zangu kwa 1200. Maana napata faida ya 200 kwa kila hisa. Hii ni biashara kati yangu na wewe. Wewe unaweza kuamua kuuza kwa yoyote pia. Na pesa inaingia mfukoni kwako na. Sio kwa CRDB.
 
Hivi kijana unajua Liquid Asset ni nini au napoteza muda wangu na mamuch know wa JF ambao kwenye dunia ya kawaida mmejibanza kwenye flat za shemeji zenu??
 
Kama ninrahisi kuuza hisa kiasi icho waulize wenye hisa za voda au precision watakupa mrejesho. Kuna walionunua hisa kwa 1000/-, leo wanauza kwa 400/- na bado hazina wanunuzi.

Kwa tesla inaweza ikawa tofauti, kwa vile demand ya hisa zake sokoni ziko juu. Hisa moja ya tesla leo ni $854. Ila kitendo cha elon ambae ni co founder na CEO wa tesla leo kuamua kuuza only 5% ya hisa zake...huu uwamuzi utawashtua sana wanunuzi na kujiuliza either Elon mwenyewe haoni future ya kampuni au kuna shida gani. Itapoteza confidence za investor na thamani ya hisa inaweza ikashuka ikafika hata $100 kwa hisa...

Ni kama bongo tu ilivyokuwa, yaani Rostam share holder mkubwa wa Vodacom anauza hisa zake zote, wewe unaenda kununua..bila kujiuliza kwann largest shareholder ameamua kuachana na hii biashara...ameona nini, anataarifa gani ambazo zimempelekea kufanya haya maamuzi ambazo wewe huku chini huna.

Kwa wenzetu uwamuzi wa Rostam tu ungeporomosha sana thamani ya hisa za kampuni. Ila kwetu ilikuwa tofauti. Ndo hiki kinatokea...hisa za voda haziuziki.
Nimegundua mkuu tunahangaika kubishana na vitoto vilivyotoka chuo na vingine viko chuoni wanaishi kwa nadharia..

Pale DSE hawamjui dalali hata mmoja, hawajawahi kumiliki share kwenye kampuni yeyote wao wanadhani ukiamka na kuamua kuuza shares basi ni sekunde tu ushauza na kukamata pesa yako..

Huo mfano wa Vodacom nilitaka niutoe humu, watu zimewalalia mpaka Leo na dividend zenyewe hazieleweki alafu kuna wapuuzi humu wanachukulia mambo juu juu tu.

Mtu anakwambia share ni Liquid Asset, sasa huyo ana akili au matope..
 
Kutumia bidhaa ya kampuni husika mantiki yako nini Apple ndio kampuni yenye Value kubwa mbona sijawai tumia kitu chao chochote, Dangote Group mbona sijawai tumia kitu chao,
Wewe hujatumia, je huna rafiki, jirani au yeyote uliyekutana nae kwenye vidaladala vyenu mnavyopandaga uliyemwona akitumia??

Gari ngapi za Dangote unapishana nazo zikiwa zimesuka Tani 30 zinaenda kufata wateja ukiwa kwenye bodaboda yako ya bolt??
 
Ngoja nikwambie kitu....trading inayofanyika kwenye stock exchange ni ya madalali tu..mimi na wewe...mimi mwenye hisa CRDB, nakuuzia wewe ambae huna. Nakupa hisa, wewe unanipa pesa. Pesa unayonipa haiingii CRDB. inaingia kwangu.

Mimi naweza nikawa nimenunua hisa za CRDB kwa shilingi 1000. Hizi hisa nimenunua moja kwa moja kwa CRDB wakati wanaregister kwenye soko la hisa.

Baada ya hapo, pale DSE ni mimi ma wewe ndio tunakuwa tunauziana. Natafuta dalali anitaftie mteja anunue hisa zangu kwa 1200. Maana napata faida ya 200 kwa kila hisa. Hii ni biashara kati yangu na wewe. Wewe unaweza kuamua kuuza kwa yoyote pia. Na pesa inaingia mfukoni kwako na. Sio kwa CRDB.
Hata sielewi mantiki yako yaani uliyoeleza yanapingana vipi kwamba Mtaji wa kampuni unaRise kupitia kuuza Hisa.

Kwa Tesla hisa yake inathamani ya pesa kubwa na wanaonunua ni wengi WEWEEE nazungumzia wanaonunua hii ndio ina rise pesa

sasa sielewi trade Trade ni nini
 
Hivi kijana unajua Liquid Asset ni nini au napoteza muda wangu na mamuch know wa JF ambao kwenye dunia ya kawaida mmejibanza kwenye flat za shemeji zenu??
Wewe ulifaa kuendelea na reply zako fupi za matusi naona ukiandika ujazo hauna hoja
 
Nimegundua mkuu tunahangaika kubishana na vitoto vilivyotoka chuo na vingine viko chuoni wanaishi kwa nadharia..

Pale DSE hawamjui dalali hata mmoja, hawajawahi kumiliki share kwenye kampuni yeyote wao wanadhani ukiamka na kuamua kuuza shares basi ni sekunde tu ushauza na kukamata pesa yako..

Huo mfano wa Vodacom nilitaka niutoe humu, watu zimewalalia mpaka Leo na dividend zenyewe hazieleweki alafu kuna wapuuzi humu wanachukulia mambo juu juu tu.

Mtu anakwambia share ni Liquid Asset, sasa huyo ana akili au matope..
Naishia hapa na huu ubishi mpaka pale mutapojifunza HISA ni nini na aina zake.

maana napoteza nguvu mimi nazungumzia HISA za umiliki wa kampuni ninyi menleta ujinga wenu wa Hisa za voda sijui DSA huu si upuuzi.

Tunaongelea wamiliki wa Voda nyie munaleta wanunua Hisa za Voda DSE ni mpuuzi tu ataendelea ku-argu kwenye mada kama hii.
 
Sasa huyo Elon akitaka abadilishe hisa zake kuwa pesa unadhani atauzia wapi we takataka kama sio Stock Exchange Market??

Nyie watoto mna shida sana... Mimi Baba yangu alininunulia hisa TBL hisa moja ikiwa inauzwa sh. 400. Ndugu huna cha kunidanganya kwenye corporate world..
 
Back
Top Bottom