Jeetu Patel: Kwanini hajakamatwa?

Mpanda Merikebu

Senior Member
Dec 27, 2007
170
2
Wana JF nisaidieni tafadhali,

Mpaka sasa, imedhihirika (na ushahidi upo) kuwa mabilioni yameibiwa huko BoT. Pia imedhihirika kuwa wizi huo ulitokea chini ya uangalizi wa Ballali. Lakini, tumejulishwa kuwa watu walioiba walikuwa ni wamiliki wa makampuni kadhaa. Kinara wao akiwa Jeetu Patel mwenye kampuni zaidi ya kumi na kuhusika kuiba zaidi ya Sh. Bilioni 90. Na hivi karibuni, gazeti la serikali limenukuliwa likisema baadhi ya haya makampuni ya Patel, yalifunguliwa siku moja na kwa sababu moja.

We all know that if it walks like a duck, looks like a duck and quacks like a duck then it must be a duck. The same apply on Jeetu's issue. The question is, if we know Jeetu is the mastermind, why isn't he under arrest, in prison or even officially named as a suspect? He is just walking like free person and the no government official has mentioned him as a person of interest?
 
Wewe Mpenda Merikebu,

Unauliza kuhusu huyu baniani kukamatwa?, Kwani Mkapa amekamatwa?.

Heri huyu baniani alikuwa anafanya biashara na BOT na kulipwa hizo pesa, sasa mkapa kuchukua $274 million (karibu shs bilion 300)na kununua mgodi kwanini asikamatwe kwanza?.
 
Nilmesema hata hapo awali JK ametoa ati 6 months for upelelezi...hiyo ni loophole kwa ajili ya mafisadi wajitayarishe ku cook the books na kujijengea ngome nzito....na ujue kuwa Jeetu kwa sasa hayupo tena nchini bila shaka anafanya transfer za hayo mapesa ya walala hoi wa bongo na kuyapeleka huko Cayman Island na kwingineko...WAHENGA WALISHAMALIZA.."MBUZI WA MASIKINI HAZAI PACHA"
 
Wewe Mpenda Merikebu,

Unauliza kuhusu huyu baniani kukamatwa?, Kwani Mkapa amekamatwa?.

Heri huyu baniani alikuwa anafanya biashara na BOT na kulipwa hizo pesa, sasa mkapa kuchukua $274 million (karibu shs bilion 300)na kununua mgodi kwanini asikamatwe kwanza?.

Mtambo,

Mtaka yote kwa pupa hukosa yote. Wizi huu ulifanyika kwa usanii mkubwa na lengo ni kuwakamata wahusika wote. Ukimwanzia huyu ponjoro, ndipo mengine yatajulikana. Kwa mfano, kutakuwa na uwezekano mkubwa kujua alipata wapi kiburi cha kufanya wizi mkubwa kama huo. Hii inadhihirisha kuwa alikuwa na some "Godfathers" ambao walikuwa wakimlinda. The same applies to Ballali, mwacheni aje, serikali impe some sort of immunity, kisha atoe data zote.

Mkapa ni mwivi mwerevu ambaye ukimwendea kichwa kichwa hutampata ng'o!
 
Nilmesema hata hapo awali JK ametoa ati 6 months for upelelezi...hiyo ni loophole kwa ajili ya mafisadi wajitayarishe ku cook the books na kujijengea ngome nzito....na ujue kuwa Jeetu kwa sasa hayupo tena nchini bila shaka anafanya transfer za hayo mapesa ya walala hoi wa bongo na kuyapeleka huko Cayman Island na kwingineko...WAHENGA WALISHAMALIZA.."MBUZI WA MASIKINI HAZAI PACHA"

Mwanatanu,

Kwanza nianze kwa kusema kuwa nimeimind bendera yako. Nakubaliana nawe kabisa kuwa miezi sita ni mingi sana kupika vitabu, kuchapisha risiti, mafaili kupotea, watu kuuawa na fedha kuhamishiwa visiwa vya Cayman ili mradi Watanzania tupigwe bao kwa mara nyingine. Hii ndio sababu ya kuanzisha hii thread...kutoa changamoto kwa wana JF wenzangu kuishinikiza serikali ianze kuchukua hatua mapema kabla ushahidi haujatibuliwa.
 
Mpanda merikebu,tumekupa hoja nzuri na maswali mazuri. Kama nilimsikia Luhanjo vizuri "RAIS AMEUNDA TUME KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA HILI KUJIRIDHISHA NA TAARIFA HIYO HILI KUWEZA KUCHUKUA HATUA SAHIHI KWA WATUHUMIWA" Swali-yaliyosemwa na kampuni iliyofanya uchunguzi wa awali na mkaguzi wa serikali yalikuwa na mashaka? tunajiridhisha nini wakati kila kitu kiko wazi? kwanini awe Balali pekee yake? wakurugenzi,mhasibu na waziri alyeidhinisha fedha hausiki? Ya mkapa na yona,yalikuwa halali? Mpanda merikebu,maswali ni mengi lakini majibu yake huwa ni marahisi toka kwa wanasiasa
 
John Nolan, yule mwekezaji wa Ireland aliyataka kuighilibu Serikali ya Mkapa imruhusu kufungua mashamba ya prawns ambayo yangeiharibu kabisa Delta ya Rufiji, alipata kusema kwamba; Tanzania ndiyo nchi pekee duniani ambayo Mzungu, Mhindi au Burushi anaweza kuingia akiwa na dola tano tu mfukoni na kuondoka miaka mitano baadaye akiwa milionea! Kweli wajinga ndiyo waliwao
Source: http://www.raiamwema.co.tz/08/01/23/mbwambo.php

Nina hasira sana wakuu basi tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom