Jeetu Patel akana madai ya Waziri Sophia Simba kuhusu mgao ;Aomba aache mipasho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeetu Patel akana madai ya Waziri Sophia Simba kuhusu mgao ;Aomba aache mipasho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 8, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,627
  Likes Received: 5,790
  Trophy Points: 280
  MFANYABIASHARA nchini Jeetu Patel amesema asihusishwe katika malumbano ya kisiasa yanayoendelea baina ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba na mbunge Mama Kilango na mumewe Malecela.

  Kauli ya Patel inafuatia baada ya hivi karibuni waziri Simba kupitia kikao cha kamati maalumu inayoongozwa na rais mstaafu, Ali Hassani Mwinyi kutoa tuhuma za kuwa wawili hao walipewa Sh 200 milioni na mfanyabiashara huyo kwa ajili ya kufanyia kampeni na pia kufadhili harusi yao.

  Patel ambaye kwa sasa ana kesi katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kuchota fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Sh11 bilioni, alisema malumbano hayo hayamhusu.

  "Mimi sio mwanasiasa mimi ni mfanyabiashara siwezi kuingilia masuala ya siasa, kwa kweli mimi simo na wala siwezi kusema lolote kwa kuwa wanayoongea hayanihusu," alisema Patel alipozungumza na Mwananchi Jumapili jana.


  Akijieleza kwenye kamati hiyo, Simba alimtuhumu Malecela, ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza, kuwa wakati akiwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, Jeetu Patel alimpa Sh200 milioni kwa ajili ya kampeni zake.

  Malecela, ambaye wakati huo alikuwa makamu mwenyekiti wa CCM, aliondolewa mapema kwenye mbio za urais, ikiwa ni mara ya pili baada ya kuenguliwa tena mapema mwaka 1995.

  Hata hivyo, akijibu mapigo hayo juzi Malecela alisema tuhuma hizo zinatokana na waziri Simba kuwa mgonjwa wa akili, huku mkewe Anne Kilango, akimshangaa kwa kukalia tuhuma hizo kwa kipindi kirefu.

  Waziri huyo mwenye dhamana ya utawala bora akiwa na taasisi nyeti kama Takukuru na Idara ya Usalama wa Taifa, alisema Mama Kilango ni mnafiki na sio msafi kiasi cha kuwanyooshea wengine vidole wakati harusi na kampeni zake za ubunge zilifadhiliwa na mtuhumiwa huyo wa ufisadi. Alhamisi Patel, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo za waziri Simba kwamba alifadhili harusi ya Malecela na kampeni zake za urais, alionekana kustuka na kusema: "Haa...we nani kakwambia... Bwana ehee, mimi sijui lolote kuhusu hayo. pamoja na hayo alishauri asiusishwe na mipasho yoyote inayoendelea juu ya ccm...mi sijazoe mipasho nanukuu....
   
 2. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Tumechoka na hizi habari
  lete habari mpya........................................mfano, Jinsi gani CCM tatoka madarakani 2010. Au jnsi gani CCM tagawanyka 2010.
   
 3. F

  Fatma Member

  #3
  Nov 8, 2009
  Joined: Jul 25, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli 2mechoka kuckia habari za Sophia Simba, Mafisadi etc. - 2nataka kuckia vp mabadiliko ya Tanzania ye2 njema yatapatikana.

  Nchi za wenze2 zinaendelea kwa kushikamana ye2 ni kupashana na kuiba aaaaagh 2mechoka 2nataka mabadiliko na maisha mema kwa nchi ye2 na vizazi vye2
   
 4. October

  October JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hatujachoka jamani, ni muhimu kusikia hata ikiwezekana kupaza sauti ili watanzania wengi zaidi wajue uozo unaoendelezwa na wanasiasa wa nchi hii. waweze kutenganisha pumba na mchele, waweze kujua ahadi hewa na waweze kufuatilia mambo yanayowahusu.

  Moja ya sababu za ufukara wa nchi hii ni lack of information. Hii imewafanya watawla kuendeleza siasa zao za ajabuajabu zisizo na tija kwa wananchi huku wakijua kuwa wananchi hawajui lolote.
  Bila kuwa na information hawa jamaa wataendelea kutufanya kuwa mafukara wa kutupwa, sioni kwanini tuache kuzungumzia mambo haya wakati tatizo bado liko pale pale.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  SOPPPPPHHHHIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIAAAAAAAAAAAAAA SSSSSSSSSSSSIIIIIIIIMMMMBBBBBBBAAAAAAAAAA.....Monotonous!
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu si hata pale kisutu alikana hajakwiba hela za EPA!
   
Loading...