jeee TAKUKURU kumekucha au DANGANYA TOTO? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

jeee TAKUKURU kumekucha au DANGANYA TOTO?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtu wa Pwani, Dec 10, 2007.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Wabongo wenye Mshiko nje kuchunguzwa
  Serikali ya Bongo imeanza kuchunguza sehemu ya fedha za baadhi ya Watanzania ambazo zipo nje kuona kama zimepatikana kwa njia ya rushwa.

  Miongoni mwa nchi ambazo ufuatiliaji huo unafanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) chini ya Mikataba ya Kimataifa ni zile ambazo zipo katika mwambao wa Bahari ya Hindi na nyingine za Asia.

  Mbovu hizo zinachunguzwa chini ya mikataba hiyo ambayo ni pamoja na wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Rushwa, Mkataba wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, ambayo Tanzania imeridhia.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Philip Marmo,
  alilithibitishia kuhusu ufutiliaji wa fedha hizo.


  source darhorwire
   
 2. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2007
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Haya ni matunda ya kelele za vyama vya upinzani maana bila makelele haya hatungeweza kuwa katika hatua hii. Sasa naona nchi itatakasika. Pesa za mafisadi huko nje zitapatikana na bila shaka kuna mafisadi wengine hawakuwa wakifahamika sasa watafahamika.

  LAKINI JE BAADA YA KUFAHAMIKA KUNA HATUA ZOZOTE ZITACHUKULIWA? AU NI DANGANYA TOTO?: BILA SHAKA NI DANGANYA TOTO!!!!!!!
   
 3. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2007
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni danganya toto tu, wameona watu wamezidi kupigia kelele Rushwa na wameamua wafanye kitu ili wadanganyika tuone kwamba wapo na wameamua kushughulikia hilo tatizo. Watasema wanawachunguza lakini mwisho wa siku utaona kama kuna lamaana litaletwa mbele yenu.
   
 4. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2007
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Blah blah blah...... Mbona hatuwezi kuwa wazi na kusema "Mawaziri wenye mapesa nje kuchunguzwa?".... Eti WaTanzania kesho itakuwa Wananchi na keshokutwa jina lingine.... Tumechoka maneno, mambo matendo ndio tunangojea... Hivi, nakumbuka Spika alikuwa anafuatiatilia issue ya WaBunge kusema mali zao tangu walipingia madarakani, hii bado ipo au??
   
Loading...