Jee wenzangu alivyofanya mwanaumw mwenzetu ni sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jee wenzangu alivyofanya mwanaumw mwenzetu ni sahihi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ngekewa, Feb 29, 2012.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  KIJANA Priva Elian (29) anayeishi Useri wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, amefyeka sehemu zake za siri na kuziondoa, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kugombaniwa na wanawake wawili.

  Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walidai kijana huyo anayefanya biashara kati ya miji ya Rombo na Nairobi nchini Kenya, alifikia uamuzi huo baada ya wanawake wawili kumgombea.

  Walidai kuwa alifikia uamuzi huo Februari 27, mwaka huu saa 1:30 asubuhi baada ya kupandwa na ghadhabu kutokana na usumbufu mwingi aliokuwa akiupata kutoka kwa wanawake hao.

  Walieleza kuwa mara baada ya kuchukua uamuzi huo, alimwita mdogo wake ambaye hakutambulika jina na kumweleza kuwa achukue viungo hivyo na kuwapelekea wanawake hao ili wavigombee.

  “Hatujui alitumia kifaa gani kujifyeka kwani kinaonesha ni kikali sana, kwani baada ya kukata sehemu hizo nyeti, alimpa mdogo wake ili awapelekee wanawake hao kwani ndicho kitu muhimu kwao na siyo yeye,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo la kusikitisha.

  Kutokana na kuvuja damu nyingi, majeruhi huyo alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Huruma iliyopo wilayani humo akiwa amepoteza fahamu na hawezi kuzungumza.

  Gazeti hili lilimtafuta Mganga Mkuu wa Hosptali ya Huruma anapopatiwa matibabu majeruhi huyo, lakini simu yake ilipokelewa na daktari mwingine ambaye alikiri kupokelewa kwa mgonjwa huyo.

  “Nikweli tumempokea mgonjwa huyo jana na tulimwingiza katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), kutokana na hali yake kuwa mbaya sana iliyosababishwa na kuvuja damu nyingi, lakini kwa sasa amehamishwa na yupo wodini,” alisema daktari huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.

  Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Kilimanjaro, Ramadhan Ng’anzi, alithibitisha ajali hiyo na kwamba Polisi inafanya uchunguzi ili kubaini kuwa kama wanawake hao kama ni wake wenza wa majeruhi, au mmojawapo.


  NI JAMVI LETU SOTE KIKE KWA KIUME KARIBUNI:
   
 2. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mh....kali.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,234
  Likes Received: 414,667
  Trophy Points: 280
  huyu kijana ni kichaa.......................maumbile yake yana umuhimu kulikoni kuwa kwenye mapenzi na mtu yoyote yule........angeliwaambia ya kuwa hawahitaji akaendelea na hamsini zake..................
   
 4. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Lzm alivuta bange,siamin akili ya kawaida kwa mwanadamu aliyetimamu aaweza fanya ivo!!!
   
 5. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Mshahara wa zambi ni mauti. Yeye alifikiri ni sifa kutembea na wanawake wawili at a go?
   
 6. Zabibu

  Zabibu JF-Expert Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  uamuzi wake unasikitisha kwakweli
   
Loading...