Jee wenzangu alivyofanya mwanaume mwenzetu ni sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jee wenzangu alivyofanya mwanaume mwenzetu ni sahihi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ngekewa, Feb 29, 2012.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  KIJANA Priva Elian (29) anayeishi Useri wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, amefyeka sehemu zake za siri na kuziondoa, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kugombaniwa na wanawake wawili.

  Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walidai kijana huyo anayefanya biashara kati ya miji ya Rombo na Nairobi nchini Kenya, alifikia uamuzi huo baada ya wanawake wawili kumgombea.

  Walidai kuwa alifikia uamuzi huo Februari 27, mwaka huu saa 1:30 asubuhi baada ya kupandwa na ghadhabu kutokana na usumbufu mwingi aliokuwa akiupata kutoka kwa wanawake hao.

  Walieleza kuwa mara baada ya kuchukua uamuzi huo, alimwita mdogo wake ambaye hakutambulika jina na kumweleza kuwa achukue viungo hivyo na kuwapelekea wanawake hao ili wavigombee.

  “Hatujui alitumia kifaa gani kujifyeka kwani kinaonesha ni kikali sana, kwani baada ya kukata sehemu hizo nyeti, alimpa mdogo wake ili awapelekee wanawake hao kwani ndicho kitu muhimu kwao na siyo yeye,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo la kusikitisha.

  Kutokana na kuvuja damu nyingi, majeruhi huyo alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Huruma iliyopo wilayani humo akiwa amepoteza fahamu na hawezi kuzungumza.

  Gazeti hili lilimtafuta Mganga Mkuu wa Hosptali ya Huruma anapopatiwa matibabu majeruhi huyo, lakini simu yake ilipokelewa na daktari mwingine ambaye alikiri kupokelewa kwa mgonjwa huyo.

  “Nikweli tumempokea mgonjwa huyo jana na tulimwingiza katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), kutokana na hali yake kuwa mbaya sana iliyosababishwa na kuvuja damu nyingi, lakini kwa sasa amehamishwa na yupo wodini,” alisema daktari huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.

  Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Kilimanjaro, Ramadhan Ng’anzi, alithibitisha ajali hiyo na kwamba Polisi inafanya uchunguzi ili kubaini kuwa kama wanawake hao kama ni wake wenza wa majeruhi, au mmojawapo.


  NI JAMVI LETU SOTE KIKE KWA KIUME KARIBUNI:
   
 2. T

  Tall JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  IMEANDIKWA ,kama kiungo chako kimoja cha mwili kinataka kukukosesha ufalme wa mbinguni ni bora uking'oe kuliko uwe na viuongo vyote viwili na uukose ufalme wa mbinguni.
  Hata hivyo huyu hayuko upande huo inaelekea akili zake si timamu. Angekuwa na akili angejua kitendo chake kinaweza kumuua. KAMKOMOA NANI SASA??? WAPENZI WAKE AU YEYE?.
  Ufumbuzi wa matatizo ya kimapenzi unahitaji HEKIMA BUSARA na UTULIVU.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  kweli mapenzi yanaweza leta karaha
   
 4. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hana akili hata kidogo...
   
 5. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Duuuhh
  Anaroho ngumu ..
  ukijaribu tu kuweka meno wakati wa BJ
  Jamaa anaruka kama hana akili nzuri ..

  Hii ya ku fyeka kabisa inanisisimua .. :(
   
 6. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Naona hapa unatoa mauzoefu.
   
 7. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #7
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wampime na akili
   
 8. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #8
  Feb 29, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  yaani nikate nanii yangu????never...huyo jamaa kichwani hamnazo
   
 9. Don Mangi

  Don Mangi JF-Expert Member

  #9
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,206
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  nimeshasikia the same case huko huko rombo mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili, haya mambo mara nyingi yanahusiana na ushirikina, si kwa akili ya kawaida, kujitahiri mwenyewe tu jambo gumu kufanya. . .sembuse kuondoa asee. . .mf.
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  angefyeka wallet ningemwelewa!
   
 11. Gabinus son

  Gabinus son Member

  #11
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  'Aaaagh! huyu bonge la ****! Hv alifikir kuwa hao wanawake wanataka hiyo nanii yake! hv kweli kwa akiri yake timamu hajajua kuwa hao wanawake walikuwa wanataka pesa yake! Yaani mpaka leo hajajua kuwa hzo nanii zinauzwa hadi madukani mwanamke gan mjinga agombanie rungu nahuku zi mejaa tele Tz karb milion 20' EBWANA EE HUYO MPUMBAVU! NAINABIDI TUMWANDALIE UBATIZO MPYA 'KAMA ALIKUWA ANAITWA 'CHRISTIANI' BASI TUMWITE 'CHRISTINA' mana hana tena utambulisho' anaimbisha kambi...
   
 12. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #12
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  out of his crazy mind
   
 13. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #13
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  nalesukwa kabisa.ete kshaaaaa mndu su kabisa labda ngaro anwa( huyu ana kichaa kabisa labda kanywa gongo.inabidi afukuzwe rombo hafai kuitwa mwanarombo.
   
 14. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #14
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,128
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  kwani wanakagombania hako kakatiti au yeye na pesa zake mpuuzi kweli kweli.
   
 15. Eversmilin Gal

  Eversmilin Gal JF-Expert Member

  #15
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 783
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rombo mmetisha, wengine sababu ya tukio wanasema Useri ipo Kenya
   
Loading...