Krismasi ni sikukuu ya wote, tutoe kwa wengine na tushereheke pamoja. Merry X-Mas!

Wote sisi ni watoto wa baba mmoja Adam, na Mungu mmoja, God, Father, The Lord!. Siku yako ikifika, ukifika hukumuni, unaweza kushangaa kuwakuta Osama, Saadam na Ghadafi peponi, halafu Bush, Blair na Obama...ndio wanaogelea kwenye lile ziwa la jehanum ya moto wa milele!.
P
Peponi kwenda kufanya nini.... kuimba mapambio?
 
Makala ya Krismasi-.png

Hii ni update ya bandiko hili kwenye gazeti la Nipashe la leo.
P
 
Hahahahaha naona ushaanza kujinasibisha na uzanzibari.

Utakuwa wa pemba ama unguja?
No sijaanza kujinasibisha, mimi Zanzibar inanihusu, Mzee Mayalla (RIP) ndiye alikuwa top wa ile kampuni ya Kiitaliano ya Cogifer, na aliishi sana Zanzibar, sasa sisi watu wa Kanda ile, na hizo rangi za Kizanzibari.... usikute nina wadogo zangu wa kutosha tuu huko.

Mi mwenyewe niliwahi kukamatika mahali, almanusura nisilimu!.
Nikija nakuja Unguja!, Wapemba kwa siye Wabara, kazi ni ngumu sana wao kufungua mioyo!.
P
 
Kwa nini Ismail awe baba wa Waislamu wote na Isaka awe baba wa Wakristo
wote- Ibraham / Hagai wote walikuwa upande waislamu upande wakristo- hivyo hivyo kwa Ibarahim na Sara- kwa mimi Ismail na Isaka ni mtu na mdogo wake tu- mmoja ni baba yetu mkubwa mwingine mdogo - kwa dini zote.
 
Daah kumbe ismail ni mtoto wa nje ya ndoa na ndio baba wa uislamu

Aisee sikuwahi kujua hii
No Ismail sio mtoto wa nje ya ndoa, mama yake Hagai alikuwa ni mjakazi, baba mwenye nyumba akizaa na mjakazi bila idhini ya mke, ndipo mtoto anayezaliwa anakuwa ni mwanaharamu, lakini baba akizaa na mjakazi kwa ridhaa ya mkewe, yule mjakazi anakuwa ni mke mdogo, hivyo Ismail ni mtoto halali na ndiye mtoto wa kwanza wa Nabii Ibrahim.

Moja ya majukumu ya wajakazi ni kumsaidia mke, zamani kulikuwa na utamaduni wa wake wengi, hivyo baba analala zamu kwa zamu, ikifika zamu yako ukijijuta imedondokea zile siku, unakuwa huwezi, hivyo unamtoa mjakazi wako anakulindia zamu.

Ikitokea mjakazi akashika katika kule kulinda zamu, status ya mjakazi huyo inabadilika anageuka suriya, hivyo anakuwa sio mjakazi tena, na mtoto anayezaliwa anakuwa ni mwana halali, na hii imetokea sana hata kwa ma sultan wa Zanzibar!.
P
 
Kwa wanaofutilia biblia wanasema Yesu hakuzaliwa tarehe 25 December,mfalme wa Rumi ndo aliamua tarehe hiyo iwe kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu,lakini ktk bible Yesu hakusema tusherekee siku yake ya kuzaliwa, haya ni mapokeo kutoka kanisa la Rumi
It's true
P
 
Mkuu muda wa kuandika mautumbo marefu unautoa wapi?
Mkuu mliberali , kuna wengi wanafanya kazi mbalimbali, wakiwa free wakapata muda ndio wanaingia JF, sisi wengine kazi yetu ndio kuandika, hivyo hapa ndio niko kazini, kesho ni gazetini, mwisho wa mwezi, zinaingia!.
P
 
Kwa nini Ismail awe baba wa Waislamu wote na Isaka awe baba wa Wakristo
wote- Ibraham / Hagai wote walikuwa upande waislamu upande wakristo- hivyo hivyo kwa Ibarahim na Sara- kwa mimi Ismail na Isaka ni mtu na mdogo wake tu- mmoja ni baba yetu mkubwa mwingine mdogo - kwa dini zote.
Dini ni mwanzilishi, mwanzilishi wa Ukristo ni Yesu aitwae Kristo, ametokea uzao wa Ibrahimu kwa Isaka na Yakobo.

Mwanzilishi wa Islam ni Mtume Muhammad (SAW), ametokea ukoo wa Ibrahimu kupitia kwa Ismail. Hivyo Wakristu na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, hivyo Mungu pia ni mmoja, na dini zote mbili zinatumia sheria moja, sheria ya Musa.
P
 
Back
Top Bottom